JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

ABDULKARIM HAJJ MUSSA, MWINYI MCHENI OMARI NA JULIUS NYERERE KATIKA KUIJENGA TANU KILWA

Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar akifahamiana vyema na Julius Nyerere.

Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar na Mwinyi Mcheni Omar ni kati ya ya watu waliomuunga mkono Nyerere na kasaidia sana katika kuiingiza TANU Kilwa Mtoni.

Abdulkarim akimpakiza Mwalimu kwenye pikipiki yake BSA 500 wakienda kote sehemu za Kilwa kuhamasisha watu kujiunga na TANU kudai uhuru wa Tanganyika.

Katika harakati hizi Nyerere alikuwa akifikia na kulala nyumbani kwa Mwinyi Mcheni Omari na mikutano yote ya ndani ya TANU ikifanyika katika nyumba hiyo.

Taifa lina deni kubwa sana kwa wazalendo hawa.

Hapo chini ni picha ya pikipiki aliyokuwa akipada Baba wa Taifa na nyumba almbayo alikuwa akifikia na kulala pamoja na kufanya mikutano ya ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…