Ikulu iliyotelekezwa iko Nsele, kilomita 40 nje ya mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kinshasa... Muonekano wa jumla wa jumba lililochakaa la rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire ya zamani), Mobutu Sese Seko mnamo Mei 15, 2017 huko Nsele, takriban kilomita 40 nje ya Kinshasa. Sese Seko alifukuzwa na vikosi vya waasi wakiongozwa na Laurent-Desire Kabila mwaka 1997 baada ya miaka 32 ya utawala kamili. Alikufa nchini Morocco miezi mitatu baadaye Mei 1997
Kipa wa zamani mwenye umri wa miaka 81, Sebastião Luiz Lourenço aliokoa penalti ya Pele mnamo Mei 12, 1971 wakati timu yake Sao Bento iliposhindwa na Santos kwenye Mashindano ya Paulista.
Amekuwa akihifadhi mpira tangu mwisho wa mchezo huo. Ndiye kipa pekee aliye hai aliyedaka kiki ya penati kutoka kwa Pele. Yeye na Pele walianza kucheza kwa wakati mmoja, akiwa na umri wa miaka 15.