Huyu ndiye aliyefunga goli ambalo lilitupeleka kwenye mashindano ya AFCON nchini nigeria mwaka 1980
Jina lake anaitwa AGUSTINO PETER MAGALI jina la kimpira aliitwa PETER TINO
ALIZALIWA MWAKA 1956 mjini dar es salaam akiwa mtoto wa tano katika watoto tisa wa familiya ya mzee PETER AGUSTINO MAGALI
FAMILIYA YAO ILIKUWA FAMILIYA YA SOKA
mkongwe peter tino alianza kucheza mpira kwenye timu za mitaaa hapa dar es salaam mwaka 1967 alianza na timu ya bonde fc baadaye young kinya zote za kariakoo
Alichezea timu nyingine nyingi za mitaani mwaka 1974 alichezea timu ya urafiki na kupewa ajira
Baadaye alijiunga na timu ya mwatex ya mwanza akukaa sana akajiunga na kurugenzi ya arusha
Baadaye alijiunga na african sport ya tanga huko ndiko alipoanza kujulikana
Alichaguliwa timu ya taifa kwa mara ya kwanza 1977akiwa na africa sport
Alichezea timu ya africa sport mpaka mwaka 1980 alipojiunga na pan afrika
Alidumu pan kwa miaka minne
Baadaye alijiunga na majimaji mwaka 1984
Wakati anamalizia mpira wake ajiunga na timu ambayo anayoipenda yanga
Alistafu mpira mwaka 1991akiwa yanga
Alichezea timu ya taifa kuanzia mwaka 1977 mipaka mwaka 1985
Sent using
Jamii Forums mobile app