JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Washukiwa wa Mau Mau Wakamatwa

Nairobi, Kenya, Julai 21 (Reuters)-Vikosi vya Uingereza vilikamata washukiwa wanane wa Mau Mau na kugundua kiasi kikubwa cha vifaa vya matibabu karibu na Hoteli ya Brackenhurst. Limur, mapumziko maarufu ya nchi. kwa Wazungu wa Nairobi maili 20 kaskazini magharibi mwa hapa. Taarifa rasmi pia ilisema vikosi vya usalama vya Uingereza viliwaua magaidi 11 wa Mau Mau katika saa 24 zilizopita.
28544cc58e337c08f1c18cdc6d08594c.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi wa wanamuziki wa super matimila wakiwa nchini AUSTRALIA mwaka 1992
Kutoka kushoto COSMAS THOBIAS CHIDUMULE
KATIKATI YUSSUFU SUBWA huyu ndiye kaka yake RASHIDI IDDI CHAMA alikuwa anapiga drum
Mwisho mkongwe MJUSI SHEMBOZA
WAHENGA KARIBUNI
PICHA KWA NIABA YA Mjusi Shemboza
FB_IMG_1688530401690.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kwenye picha ndiye alikuwa mbunifu na mchoraji wa ramani wa soko la kariakoo mzee huyo ambaye kwa sasa ni marehemu BEDA JONATHAN AMULI
ALIZALIWA TAREHE 27-5-1938
Na alifariki tarehe 10-7-2016
Soko lilianza kujengwa mwaka 1971 na kampuni ya mecco
Jiwe la msingi liliweka 1973 na makamu wa kwanza wa rais na rais wa zanzibar marehemu ABOUD JUMBE MWINYI
SOKO LIMEFUNGULIWA MWAKA 1975 NA RAIS MWALIMU NYERERE
Soko mpaka linamalizika limeghalimu milioni 23.3 enzi ya mwalimu
FB_IMG_1688537324729.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ndiye aliyefunga goli ambalo lilitupeleka kwenye mashindano ya AFCON nchini nigeria mwaka 1980
Jina lake anaitwa AGUSTINO PETER MAGALI jina la kimpira aliitwa PETER TINO
ALIZALIWA MWAKA 1956 mjini dar es salaam akiwa mtoto wa tano katika watoto tisa wa familiya ya mzee PETER AGUSTINO MAGALI
FAMILIYA YAO ILIKUWA FAMILIYA YA SOKA
mkongwe peter tino alianza kucheza mpira kwenye timu za mitaaa hapa dar es salaam mwaka 1967 alianza na timu ya bonde fc baadaye young kinya zote za kariakoo
Alichezea timu nyingine nyingi za mitaani mwaka 1974 alichezea timu ya urafiki na kupewa ajira
Baadaye alijiunga na timu ya mwatex ya mwanza akukaa sana akajiunga na kurugenzi ya arusha
Baadaye alijiunga na african sport ya tanga huko ndiko alipoanza kujulikana
Alichaguliwa timu ya taifa kwa mara ya kwanza 1977akiwa na africa sport
Alichezea timu ya africa sport mpaka mwaka 1980 alipojiunga na pan afrika
Alidumu pan kwa miaka minne
Baadaye alijiunga na majimaji mwaka 1984
Wakati anamalizia mpira wake ajiunga na timu ambayo anayoipenda yanga
Alistafu mpira mwaka 1991akiwa yanga
Alichezea timu ya taifa kuanzia mwaka 1977 mipaka mwaka 1985
FB_IMG_1688626782269.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo imetimia miaka sita tangu mwanamuziki SHABANI DEDE KAMCHAPE atutoke duniani
Dede alifariki tarehe 6-7-2017 kwenye hospital ya muhimbili
Na kuzikwa kisutu
Dede alizaliwa mwaka 1955 kule bukoba
Alipigia bendi tabora jazz,baadaye Dodoma international ndiyo iliyomtambulisha
Alijiunga na juwata mwaka 1979 alitunga na kuimba vibao vingi vizuri kimoja wapo fatuma nasafiri
Alikaa msondo kwa muda akajiunga na sikinde mwaka1982 huku alitunga vibao vizuri sana na kuimba, moja ya vibao mashuhuri ni taraka rejea
Mwaka 1984 alienda bima huku pia alitamba sana tena sana
Baadaye akarudi msondo akatunga nyjmbo kimwaga na sauda na nyingine kaimba
Akatoka msondo akaenda OSS YA NDEKULE akaimba nyimbo nyingi na akatunga wimbo nyumba ya mgumba aina matanga
Baadaye akarudi bima ya kina marehemu eddy sheggh
Akarudi mlimani park akaimba vibao vingi na kutunga alikaa sana sikinde kama kiongozi
Baadaye akarudi bendi yake ya zamani msondo ngoma mpaka umauti unamkuta
FB_IMG_1688627401350.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom