Jumba la cinema la cameo ilikuwepo mtaa wa jamhuri baina ya mtaa wa kitumbini na mtaa wa fupi kulia kwenye kona ilikuwa hoteli ya royal alikuwepo mzee mahmoud alikuwa marufu wa kuchoma mishkaki na seek kabab kama mnakumbuka
The old Post Office, the building is still standing there, as a historical site, wonder when City fathers are going to demolish it like other old historical demolished buildings.....
Huyu ni marehemu PHILLIP NDUNGURU.
Phillip Ndunguru, moja ya msukumo mkubwa wa wachoraji makatuni nchini Tanzania. Phillip Ndunguru alikuwa miongoni mwa wachora vibonzo waanzilishi wa Afrika Mashariki. Mwishoni mwa mwaka wa 1980 Ndunguru alikuwa mwandalizi mkuu wa jarida la Sani. Baada ya jarida hilo kuisha mwaka wa 1981, Ndunguru alikuwa msanii aliyejiajiri. Mwaka wa 1983 alienda kufanya kazi jijini Nairobi katika gazeti la Kenya Times, huko alianza kuchora kibonzo maarufu KAZI BURE.
Kwa kusikitisha mwaka wa 1986 akiwa na umri wa miaka 24 tu, Phillip Ndunguru aliaga dunia. Vibonzo vyake bado vinakumbukwa na vilichapwa tena baada ya kifo chake. Kama ulisoma jarida la Sani, Kazi Bure gonga chias.. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, Shirika la Ndege la Jumuiya pia lilikufa, Tanzania tukaanzisha Air Tanzania Corporation (ATC) tukiwa na Ndege hizo Boeing 767, Boeing 737, Fokker Friendship 50 na Twin Otter.
Zote hizo kwa sasa hazionekani Tanzania isipokuwa hiyo kubwa zaidi 767 ililala Uwanja wa Ndege kwa miaka mingi ikiwa mbovu.
Katika safari ya kupigania uhuru historia haikuwataja baadhi ya wanaharakati hata wakiwemo kina mama, haya wahenga wenye taarifa nzuri watutajie hawa kina mama na wazee kadha wa kadha wenyeji wa kariakoo hawajulikani kwenye historia
Mzee Nassoro Rajabu, dereva wa kwanza wa Mwalimu kabla na baada ya uhuru.
[emoji3591]Kabla Uhuru alimuendesha kuanzia 1953 - 1961, baada ya Mwalimu kuapishwa akamuendesha tena 1962 - 1985.
[emoji3591]Kabla uhuru, gari haikuwa yake alikuwa ameajiriwa na muhindi kama dereva Tax tu.
[emoji3591]Serikali ilimuajiri 1962 kumuendesha Mwalimu na hata Mwalimu alipostaafu 1985, akamuendesha Rais Mwinyi kwa miaka mitatu.
[emoji3591]2017, alihojiwa na na kituo cha Global Tv maisha yake yalikuwa duni sana, chakula chake cha tabu sana na hata hakuwa na godoro na kulaza mbavu zake.
Hali ilivyokuwa jijini Dar es salaam miaka ya 1980. Wakazi wa jiji hapo wakijiandaa kuvuka barabara huku kukiwa na foleni kubwa ya Daladala ambazo nyingi wakati huo zilikuwa ni ISUZU ELF kama unavyoona pichani. Mabasi ya UDA yalikuwepo, lakini ilikupunguza adha ya usafiri wakati huo, watu binafsi pia waliruhusiwa kusafirisha abiria.
Ingawa recodi zake si nyingi sana, lakini dada huyu recodi ya 'Kupanda na kushuka', 'Dunia lukumba lukumba' na 'Tama ililuwa fisi' zilipendwa sana miaka ile ! anaitwa Lady Isa.
MJUE YUNGE MWANASALI KATIKA HISTORIA YA SOKA KABUMBU.
Yunge Masunga Sali ndiyo Yunge Mwanasali huyu, alikuwa ni Mtoto wa Mtemi MWANASALI (Masunga Sali) wa USONGO.
Katika kitabu Cha R.G.Abrahams(1st edition 1981) kiitwacho NYAMWEZI TODAY, A Tanzania people in the 1970's (page-126 ) ameandika kuwa Yunge Mwanasali ndiyo Nahodha wa kwanza wa timu ya Taifa ya Tanganyika ya mpira wa miguu.
"Yunge Mwanasali, for example, was captain of Tanganyika's first international football.
Mnamo mwezi julai 1997 huko London uingereza Oska kambona aliutoka umma wa watanzania baada ya kuugua kwa muda, Kambona amebaki katika historia Ya vijana wa wakati ule akijumuishwa na Vijana wengine jasiri wa wakati huo Kama Chifu Said Fundikira na wengine wengi walio kua mstari wa mbele katika siasa na maendeleo ya Taifa.