JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

The giant of Kandahar , photographed Afghanistan 1923
FB_IMG_1694216992268.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUMKUMBUKE MWANAMUZIKI PEPE KALLE

Mnamo Novemba 30, 1951 katika Jiji la LeopordVille kwa sasa{KINSHASA} huko Kongo ya Mbelgiji kwa sasa {Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo} alizaliwa mtoto aliyepewa jina la Kabasele Yampanya.

Alikuwa mtunzi, mwimbaji wa muziki wa soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba. Pepe Kale aka Tembo Jitu la Miraba Minne alikuwa bingwa wa miondoko ya soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba, ambayo ilikuwa maarufu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Watanzania wengi tutaendelea kumkumbuka mwanamuziki huyu hasa wakati alipokuja nchini mwetu na kutikisa majiji ya Arusha, Dar es Salam na Mbeya.
Wakati wa ujio wake hapa Tanzania, Pepe Kalle ambaye sauti yake ilikuwa nyembemba na nyororo, alifuatana na wanamuziki akiwemo mipiga wa gita la besi Lofombo na waimbaji akina Papy Tax, Dilu Dilumona na Djo Djo Ikomo.
Pepe Kalle aliyefariki Novemba 28, 1998 kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 47.
FB_IMG_1694227132494.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu anaitwa Shaban Baraza
Alikuwa beki imara sana enzi yake akichezea timu ya Simba
Wahenga waliopata kumuona akicheza wanasema alikuwa beki imara sana
Alijiunga na Simba akitokea timu ya Mashujaa ya Morogoro yeye na Adamu Sabu na Hassan Mlapakolo
Aliwahi kwenda kucheza soka uarabuni
FB_IMG_1694254588315.jpg
FB_IMG_1694254591528.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sultan masudi ndiye aliibuka mshindi ktk shindano la kumtafuta mtu aliye na sura mbaya zaidi Tanzania miaka hiyo ya 1990, akifuatiwa na Dr. remmy ongara huku Mshindi wa tatu akiwa ni Mzee Jangala.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa aliyekuwa mshindi wa Pili yaani Dr remmy ongara akalalamika kuwa huyu masudi amependelewa!

Kwani amefanya uchunguzi amegundua masudi anatoka ktk familia iliyo na ugonjwa wa ukoma!
Hivyo hakustahili kumshinda yeye

Na Mzee Jangala pia alikata rufaa kuwa iweje yeye aonekane mrembo na kushinda nafasi ya tatu?
FB_IMG_1694276594178.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanganyika, Kigoma July 19, 1960

Kundi la kwanza la Wabelgiji 465 walipowasili Kigoma kutoka Congo baada ya kufukuzwa Congo ilipopata Uhuru wake June 1960.

Hapa pia kulikuwa na Waitaliano, Waingereza na Wagiriki, wote walipanda treni hii hadi Dar es Salaam Ukonga ambapo kulijengwa makazi ya muda ya wakimbizi hao wakizungu.
FB_IMG_1694529774148.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hii Bendi ya ORCHESTRA MCA INTERNATIONAL ilitia fora sana enzi zake.
Kuna nyimbo kama,
1.Kasora yangu sijaijua
2. Moyo wangu
3. Baba na mama
4. Mkasa wa Eggy
5. Mla kunde
6. Maisha kigeugeu.

Nilinunua hii kaseti kama ukumbusho kwa duka moja mjini Mombasa kwa jina MUSIC LAND tarehe 11/4/ 1997 kwa shilingi 150/- pesa za Kenya.

Wimbo wa mkasa wa Eggy unanikumbusha mbali. Una haya maneno:

Ninakumbuka mkasa ulionipata kwa kumpenda Eggy. Nilimpenda Eggy kupita uwezo jamaa. Nilikuwa dalali wa penzi bila kujali karaha. Kumbe nilikuwa naramba asali kwa ncha ya kisu bila kujitambua. Utamu ulikidhiri sikuona wala kusikia. Mapambo nilimpamba ya kila aina, niliweka koga ya mapenzi nikajiona niko pekee kumbe tuko wawili ndani ya nyumba. Akatupangia kila mtu na wakati wake nikajisia vibaya.
Haya yote yalitokea kwangu. Mapenzi hatari huu wimbo wanikumbusha mbali wanaume tunapitia masaibu. Vijana wa zamani mpo toeni kauli zenu, yalinikuta mwenzenu.
FB_IMG_1694659784449.jpg
FB_IMG_1694659780904.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAND:_Orchestra Mlimani park.
WIMBO_Nalala kwa tabu, (1981).
MTUNZI:_ Cosmas Chidumule.
WAIMBAJI:_ Gurumo, Bichuka, Hamisi Juma.
SOLO GITAA:_ Joseph Mulenga.
RIZIM GITAA:_Abdalha Gama.
BASS GITAA:_Selemani Mwanyiro.
TUMBA:_ Ally Jamwaka.
DRUMS:_ Abibu Jeff.
SAXOPHONE:_ King Michael Enoch.
TANNER SAXOPHONE:_ Juma Town, na Yusuph Bernard.
TRUMPET:_Machaku Salum, Ibrahim Mwichande, na Bornfasy Charles.

MASHAIRI YAKE:
Mwenzenuuu, usiku huwa silali, natesekaa usingizi kweli sipati nabaki nahangaiikaaaa.....
Kuyasema yoteee, ninayaoona siweziii, yasije yakaletaaa udadisi kwa watu bureeee.....
Shahidi yangu ni mama watotooo, yeyee anajuaaa...kwani huwa uniona ninavyo angaikaaaa...x2.
Dah! Nisimalize uhondo.

NB: Watu watajiuliza mbona Cosmas Chidumule hakuimba katika wimbo huu?
Ni kweli Cosmas hakuimba katika wimbo huu, bali yeye alishiriki kutunga. Wakati wimbo huu kabla haujapelekwa studio, Cosmas alishalipa kisogo kundi la Mlimani park na akatimkia zake Vijana jazz band.
Karibuni WAHENGA.
FB_IMG_1694792171131.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom