JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Miaka 20 iliyopita sio haba!..wakati hii nyimbo inatoka that time ndio unakutana na Bitozi Mtaani ana ka-plasta Usoni bila jeraha,kavaa Jeans pana unaweza fikiri kachomeka miguu kwenye Mapipa....Chini Bonge la buti kana kwamba kasimama juu ya Mawe...hapo Shati kubwaaa Kama Tanuru la vigae linapepea na ana tooth peak Mdomoni ingawa Hajala.

Warembo walikuwa wanasumbua sometimes, yaani Unam-dedicate songi la DILEMMA halafu ana-complicate mambo utadhani Mzabuni anaandaa BOQ ya kujaribu supply ya kitimoto nchini Iran!...lakini zote ni Mbwembwe tu!..Nelly ft Kelly Rowland ."Dilemma"....time flies!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni trekta aina ya Massey furguson
135 tumezitimia sana kulimia na unaweza kuitumia vyovyote utakavyo kama kupalilia, kupiga dawa,kufagia barabara n.k nilianza kuziona tangu miaka ya 70 na hadi sasa zipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani wafadhili ndiyo wanakaa kwenye bechi alafu wachezaji wanakaa chini
Hawa ni wafadhili wa timu ya Yanga mwenye miaka 80 wakiwa kwenye bechi la timu
Marehemu Mohamedi virani akiwa na meneja wa timu Vinod Asar enzi hizo
Marehemu Mzee virani alikuwa mfadhili mkubwa sana kwa Yanga


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MTAA WA VERSAILLES (sasa hivi ni Azikiwe Street)- 1918. Kaiserhof Hotel (New Africa Hotel) ni hiyo upande wa kulia na Hermann von Wissmann Monument (now Askari Monument) iko mbele. Hii hoteli ilikuja kubadilisha na kuwa hospitali ya kutibu askari majeruhi wa kijerumani na waTanganyika (Picha ya 4- ukiangalia utaona bendera ya msalaba mwekundu ikipepea). Mwaka 1920 baada ya Uingereza kupewa Tanganyika waliichukua hoteli na kuibadilisha kuwa hoteli tena na kuuita New Africa Hotel (Picha ya 3).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha namba moja hiyo ni daraja la zamani la WAMI mwaka 1960 na picha ya pili ni daraja hilihilo miaka kadhaa iliyopita, naiona Islam Coach ikivuka hapo. Daraja hilo bado liko imara sana mpaka hii leo, halitumiki hivi sasa kutokana na kuwa kwenye mteremko mkali na kona kali na pia ni jembamba sana kiasi cha kutoweza kuruhusu magari kupishana yakiwa darajani na hivyo kusababisha ajali za mara kwa mara ukichukulia kwamba sasa hivi tuna magari mengi sana brabarani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi zillitwa marula bus huko Kenya
 
Hii ndiyo Kivukoni ya enzi hizo, ni vumbi tupu hapo, PANTONI hapo bado saana. Mpiga picha alipiga picha hii akiwa hapa eneo la kivukoni ambapo siku hizi kuna stendi ya mabasi ya Mwendokasi na daladala. Kwa mbali unaweza kujionea sehemu ya Bandari ya Dar es salaam, Kanisa la Roma Mt Joseph na kanisa la Lutheran la Azania Front.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…