JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Leo miaka 10 toka mwamba huyu wa utangazaji Julius Omang’ere Nyaisangah afariki. Nyaisangah alikuwa mmoja wa watangazaji hodari sana mwenye sauti na matamshi laini na matamu sikioni kwa msikilizaji.

Endelea kupumzika kwa amani brother ukiwa na timu rtd- Nadhir Mayoka, Hendrix Michael Libuda, Idd Mchatta,Ahmed Jongo, Siwatu Luwanda, Salama Mfamao, Hassan Mkumba, Juma Ngondaye, Nelly Kidela, David Wakati, Omar Jongo, Sarah Dumba, Batty Kombwa,Halima Mchuka, Suleiman Hegga na wengineo.

Pia wasalimie team IPP MEDIA wote huko Mwenyekiti Reginald Mengi, Rodney, John Ngahyoma, Misanya Bingi, Moses Justine-Papaa Mo, Isaac Muyenjwa Gamba, Robert Mbando, Baba T, Rehema Mwakangale, Oscar Mirindo, DJ Rankim Ramadhan, Dj Rico na wengineo. Nyote tunaendelea kuwakumbuka kwa mchango wenu mkubwa kwenye tasnia hii.View attachment 2797632

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulimwita uncle J na club leo shoooooooo....

Sent from my Hope10 Pro using JamiiForums mobile app
 
Ahmed kipozi, mwanalindanda mwanakawekamo... Dominic chilambo, aibas Stephen, Andrew maiko libuda, bananasi mluge......thekioni kitojo, na nkk

Sent from my Hope10 Pro using JamiiForums mobile app
 
Basi hili linaitwa "FITINA JIRANI" Dar mpaka Kyela. Mnazi mmoja hiyo na hapo bado jamaa wanaendelea kupakia mzigo, Kitonga pale na zile kona za Iyovi watu wanalala nalo hilo utadhani linapinduka, lakini waapi, yaani ilikuwa kazi kweli kweli, na safari yenu mnafika salama salimini. Kipindi hiki ndiyo kipindi ambacho watu wengi walikuwa hawapendi kusikia habari za Mlima Kitonga.View attachment 2797656

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama vile ilivokuwa salanda

Hahaha

Harafu dereva mpaka alewe ndiyo avuke milima hiyo

Sent from my Hope10 Pro using JamiiForums mobile app
 
S.L.P 752 ,Arusha..........taja yenu
FB_IMG_1701151481112.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA DUNIA INGEKUWA NA UKUBWA WA JUPITER BAS INGEKUWA NGUMU KWETU SISI KUTOKA NJE YA DUNIA YETU

Pengine kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa mara mbili au tatu ya ukubwa wake wa sasa basi ingekuwa ni ndogo kwetu sisi wanadamu kutoka nje ya dunia yetu

Acha nikwambie embu tuchukulie kwa ukubwa wa sayari yetu ambapo huanza kujihesabu kuwa tupo nje ya dunia yetu pale tunapokuwa tupo umbali wa kuanzia km 100 kutokea usawa wa bahari ambapo kwa kasi ya 40,000 kilomita kwa saa ndio inayohitajika .

Ambapo kwa ukubwa wa rocket zetu na kwa kiasi cha nishati kinachobeba basi ni sawa na ni salama kabisa kuwezesha wanadamu na mizigo kwenda nje ya dunia yetu .

Sasa unadhani ingekuwaje kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa kama sayari ya jupiter na je unadhani safari za kwenda anga za mbali zingewezekana kweli

Kwa jambo hilo lisingewezekana kabisa kwa sababu kadhaa ambapo moja wapo ni sababu ya umbali na kani kubwa ya uvutano ambayo dunia yetu ingekuwa nayo na tunafahamu kuwa kadri gimba linavyokuwa na ukubwa mkubwa basi ndio kani ya uvutano nayo inavyozidi kuwa kubwa sana

Sayari ya jupiter ina kani ya uvutano wa 24.76 m/s² ambapo ili uweze kutoka nje ya sayari hiyo ya jupiter basi hutahitaji rocket au chombo chenye kasi ya 214,200 kilomita kwa saa ambapo ni kasi kubwa sana kabisa .

Na kama tukitaka kuweza kupata kasi kama hiyo basi inatubidi tuwe na rocket kubwa sana pengine ni mara 10 ya rocket ambazo tulizokuwa nazo kwa sasa jambo ambalo lisingewezekana

Ni wazi kabisa ilituweze kusafiri kwa kasi kubwa sana basi kiasi kikubwa cha nishati ndio kitakapokuwa kinahitajika , sasa kwa ukubwa huo wa rocket na kwa maumbo yetu haya ya wanadamu sidhani kama tungeweza kufanikiwa kwa hilo .

Sasa kama gimba litakuwa kubwa sana basi nafasi ya kuwa na wingi wa matabaka mazito ya anga hewa ambapo ni ngumu sana kwa chombo kuweza kukatisha katika maeneo hayo kasi kubwa inahitajika ili kuweza kukatisha katika maeneo hayo .

Pengine ingekuwa ni hadithi kwa sisi kuweza kutoka nje ya dunia yetu kama ingekuwa na ukubwa kama wa sayari ya Jupiter .

#AstronomyKiswahiliView attachment 2814456

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe tumedanganywa kuwa,baadhi ya vyombo kutoka duniani huenda huko kufanya uchunguzi na kurejea je vinatokaje huko?
 
Miaka ya 1970. Kina mama na watoto wao wakiwa wameshuka kutoka kwenye PANTONI. Hapo ni upande wa Kigamboni. Nadhani watakuwa wanakwenda Kimbiji ama Gezaulole hawa. Watu ni wachache sana, ni wa kuhesabu. Nakumbuka hizi baibui ndiyo yalikuwa mavazi makuu ya wanawake wa pwani kwa wakati huo.
FB_IMG_1701737744078.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daktari Bingwa wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo, Profesa James Shaba amefariki dunia jumanne Desemba 5, 2023.

Profesa Shaba ndie profesa wa pathology wa kwanza Afrika ya mashariki na kati.

Profesa Shaba ndie aliyefanya uchunguzi wa mwili wa waziri mkuu wa zamani wa Tanzania 'postmortem' Hayati Edward Sokoine, pale hospitali ya taifa Muhimbili.

Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 45 kutokana na ajali ya gari iliyotokea Dakawa - Morogoro.

Pumzika kwa amani Profesa
20231208_133311.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom