KAMA DUNIA INGEKUWA NA UKUBWA WA JUPITER BAS INGEKUWA NGUMU KWETU SISI KUTOKA NJE YA DUNIA YETU
Pengine kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa mara mbili au tatu ya ukubwa wake wa sasa basi ingekuwa ni ndogo kwetu sisi wanadamu kutoka nje ya dunia yetu
Acha nikwambie embu tuchukulie kwa ukubwa wa sayari yetu ambapo huanza kujihesabu kuwa tupo nje ya dunia yetu pale tunapokuwa tupo umbali wa kuanzia km 100 kutokea usawa wa bahari ambapo kwa kasi ya 40,000 kilomita kwa saa ndio inayohitajika .
Ambapo kwa ukubwa wa rocket zetu na kwa kiasi cha nishati kinachobeba basi ni sawa na ni salama kabisa kuwezesha wanadamu na mizigo kwenda nje ya dunia yetu .
Sasa unadhani ingekuwaje kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa kama sayari ya jupiter na je unadhani safari za kwenda anga za mbali zingewezekana kweli
Kwa jambo hilo lisingewezekana kabisa kwa sababu kadhaa ambapo moja wapo ni sababu ya umbali na kani kubwa ya uvutano ambayo dunia yetu ingekuwa nayo na tunafahamu kuwa kadri gimba linavyokuwa na ukubwa mkubwa basi ndio kani ya uvutano nayo inavyozidi kuwa kubwa sana
Sayari ya jupiter ina kani ya uvutano wa 24.76 m/s² ambapo ili uweze kutoka nje ya sayari hiyo ya jupiter basi hutahitaji rocket au chombo chenye kasi ya 214,200 kilomita kwa saa ambapo ni kasi kubwa sana kabisa .
Na kama tukitaka kuweza kupata kasi kama hiyo basi inatubidi tuwe na rocket kubwa sana pengine ni mara 10 ya rocket ambazo tulizokuwa nazo kwa sasa jambo ambalo lisingewezekana
Ni wazi kabisa ilituweze kusafiri kwa kasi kubwa sana basi kiasi kikubwa cha nishati ndio kitakapokuwa kinahitajika , sasa kwa ukubwa huo wa rocket na kwa maumbo yetu haya ya wanadamu sidhani kama tungeweza kufanikiwa kwa hilo .
Sasa kama gimba litakuwa kubwa sana basi nafasi ya kuwa na wingi wa matabaka mazito ya anga hewa ambapo ni ngumu sana kwa chombo kuweza kukatisha katika maeneo hayo kasi kubwa inahitajika ili kuweza kukatisha katika maeneo hayo .
Pengine ingekuwa ni hadithi kwa sisi kuweza kutoka nje ya dunia yetu kama ingekuwa na ukubwa kama wa sayari ya Jupiter .
#AstronomyKiswahili
View attachment 2814456
Sent using
Jamii Forums mobile app