JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Kwa wale wahenga kama Mimi mnakumbuka ngoma ya mdundiko
Ngoma ambayo ilitikisa sana jiji la Dar es salaam kwa kuzoa watu hasa kina mama na watoto
Ngoma hii kabla ya kuitwa mdundiko ilikuwa inaitwa mganda ngoma maarufu sana enzi zile kwa sisi wazaramo,ila kutokana na mapigo yake kubadilisha ndiyo ukaitwa mdundiko
Kwa Mimi ambaye niliishi maeneo ya Ilala nawakumbuka wapigaji wa ngoma hii yaani wale waliopiga ngoma kubwa
Mzee kwaile
Mzee ng'obwe
Mzee maleft
Hawa ndiyo walikuwa maarufu sana makazi yao yalikuwa Buguruni
Baadaye ngoma ya vanga ambaye nayo ikaitwa mkinda nayo walipiga mdundiko
FB_IMG_1702360264923.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwafrika Coach hiyo enzi zake, ISUZU MV118 ya Iringa mpaka Makete. Isuzu MV118 ndiyo gari lililoweza kuleta usumbufu sana kwa SCANIA 93 enzi hizo kabla ya ujio wa VOLVO B7, sababu hata kwenye milima ilikuwa na nguvu sana. Nadhani mnakumbuka ile Isuzu ya LIKUNGU, MATEMA BEACH na baadaye LUCKY STAR ya Dar Mbeya.
FB_IMG_1702596291164.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni Askari monument miaka ya 60, Gorofa la IPS bado kabisa kujengwa lakini naliona hapo mbele lile jengo ambalo sasa hivi kuna Benki ya NMB, hapo kwenye miti, aisee kuna majengo mengine hapa mjini ni ya zamani sana. Jengo hili hapo kwenye kona ndiyo baadaye palikuja kujengwa jengo la IPS, wengi mnalijua.
FB_IMG_1702794080320.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
National Stadium 1968. Tanu Youth League tuna march gwaride na wengine wanafanya halaiki. Nilikuwa Form I , St Josephs. Soda za kupigania na hakuna opener ,unafungua kwa meno. Fujo namna yake mpaka Mzee Kibira aliyekuwa Regional Education Officer anasema " Sasa nimechoka, nyinyi watoto hamusikii kabisa" katika accent ya Kihaya[emoji23][emoji23][emoji23]
FB_IMG_1702973104610.jpg
FB_IMG_1702973108076.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom