stori nyingine ujue zinamfanya mtu aoenekane mjinga halafu hatujui kama ni kweli... Eti kapewa mtonyo na wana usalama, ee bana mshkaji anataka kukutoa roho, akasema huyo mwana akitaka kuniua hakuna wa kumzuia. Halafu yakaishia hapo, hakufuatilia, kaendelea kuishi nae kama mwana kama kawaida. Alikua mjinga kiasi gani?
Hivi ukiambiwa ee bana, mkeo anataka kukuua, utasema aaaah, huyu nalala usingizi pembeni yake akitaka kuniua huwezi kumzuia, halafu unaiachia hapo hapo, huulizi imekuaje, tunafanyaje, unaua stori, unaendele na maisha??? Then he was a damn douchebag.
Kiongozi,
Naomba nikueleze kidogo maana ya maneno ya Rais Thomas Sankara mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Wanausalama kuhusu mpango ule ovu wa rafikiye Blaise Compoure dhidi yake
Alisema "Hata kama akitaka kuniua(Compoure)hakuna wa kumzuia" hii ina maana mbili
1. Alimuamini sana rafikiye Compaore kiasi cha kutohisi wala kudhani kuwa angeliweza kupanga njama mbaya za kumdhuru na hata kumuua.
2. Kutokana na ukaribu wao Rais Sankara aliamini ikiwa Compaore angelitaka kumuua ama kumdhuru basi asingelishindwa kutokana na ukaribu waliokuwa nao wawili hao hivyo kupelekea kumjua Rais Sankara ndani nje. Ni sawa na mtu aje akuambie mkeo anampango wa kukuua, utajua fika tu hata akitaka kuniua ni rahisi sana kwa kuwa mnaishi pamoja unalala nae na kukupikia(akitaka kukudhuru ni rahisi sana)
Lakini nikurejeshe kidogo nyuma
Rais Sankara sio kiongozi pekee aliyepelekewa taarifa za kuuawa na kuzipuuza
Alasiri ya tarehe 07/04/1972
Wana Usalama walimfuata Rais Mzee Karume wakamwambia "Mzee leo hali huko nje sio salama, kuna taarifa wanajeshi wameiba silaha toka ghala la silaha Jeshini kwa hivyo Mzee tunakuomba usitoke Ikulu kwenda kukote" Wakijua Mzee Karume kila alasiri baada ya kazi hupenda kutoka kwenda maskani Makao Makuu ya Afro Shiraz Party pale Kisiwandui kucheza dhumna na kupiga soga huku akinywa kahawa na Rafiki zake akiwemo Sheikh Thabit Kombo(Katibu Mkuu wa Afro Shiraz).
Mzee Karume alijibu kuwaambia wana Usalama wake "Famil llah"(Namuachia Mungu) huku akionekana kuzipuuza taarifa zile.
Huku akisahau kuwa "Kambale akikwambia Mamba anaumwa basi usibishe" kwa kuwa wanaishi wote majini.
Mzee Karume akatoka zake licha ya tahadhari aliyopewa, alifika Maskani ya Chama Kisiwandui na kujumuika na rafiki zake huku wakicheza dhumna, kunywa kahawa na kupiga soga, ghafla wanajeshi wawili waasi Captain Humud na mwenzake wakaingia maskani Kisiwandui na kuanza kumshambulia Mzee Karume kinyama hadi mauti yake na kujeruhi rafiki zake akiwemo Sheikh Thabit Kombo.
Waswahili tuna msemo wetu "Kilichompata Mamba na Kenge pia kitampata"
Nihitimishe kwa kusema Kilichompata Rais Mzee Karume mwaka 1972 ndio Kilichompata Rais Sankara mwaka 1987.