JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Hivi vitu mkuu,hivi ni vitu adimu sana..tena saana.
๐Ÿ™๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿพ

Na sema nimechoka tu kuandika ndo maana kasi ikepungua na majukumu yanabana. Ila nna picha za historia nyingi sana
 
[emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488]

Na sema nimechoka tu kuandika ndo maana kasi ikepungua na majukumu yanabana. Ila nna picha za historia nyingi sana
Usisite mkuu pindi upatapo wasaa!Asante sana.
 
So 2 June 1953 ndo ilikua Coronation ya Bibi Eliza

View attachment 1521373
Hio hapo juu ni sherehe zilizofanyika UK

Ila pia kulikua na sherehe zilizofanyika katika nchi zote zilizokua chini ya Ufalme wa UK

View attachment 1521376
Sherehe zilifanyika pale mbele ya Boma Arusha
View attachment 1521379
Wananchi wakitoka kwenye Rehearsal ya Coronation Day. Hii ni May 1953
haya kweli mabeberu 1953 ni kama walikuwa wameshamalizana na kila kitu kwenye masuala ya maendeleo
 
1596554164130.png
 
Watu wengi wanaijua Karimjee Hall tu. Hawajui kwanini iliitwa hivyo.
View attachment 1519983
Karimjee Hall ya sasa




View attachment 1519987
Familia ya Yusufali Karimjee

--Yusufali Karimjee (1882โ€“1966)

Alijulikana pia kama โ€˜Lion of Zanzibarโ€™. Alikua boonge la mfanyabiashara.Alifanya biashara toka Bongo,Hanover(Germany) hadi Japan, na alioa mwanamke wa Kijapani. Kupitia kwa mwanae Abdulkarim walitoa zawadi ya huo ukumbi kwa Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1955

--Abdalla Mohamedali Karimjee (1899โ€“1978)

Mdogo wake na Yusufali ambaye alijulikana pia kama "Sisal baron of Tanga" na alishatunukiwa na malkia OBE (Officer of the British Empire) mwaka 1961. Mwaka 1924 alisafiri kwa pikipiki toka Bongo mpaka South Africa kwenda ku"negotiate" mkataba wa kusambaza mafuta na kampuni ya Caltex

Alikuja kuwa Mbunge baadae bunge la Tanganyika(Legislative Council) na pia alihudhuria kutawazwa kwa Queen Elizabeth II mwaka 1953.Princess Margaret alishawahi kuja kumtembelea kwake Tanga mwaka1956.Alioa pia mke wa pili Mjerumani

--Tayabali Karimjee (1897-1987)
Mdogo wa mwisho wa Yusufali. Huyu alizaliwa na kusoma Zanzibar na alikua rafiki wa karibu wa Sultan. Pia Sultan alimteua kuwa Mbunge(Legislative Council Zanzibar) ila alisusia Bunge na kutoka nje ya Bunge baada ya kupitishwa Clove Monopoly Bill ya 23 Julai 1937. Akiwa na msimamo kwamba hio sheria inawanufaisha zaidi Wazungu.

--Abdulkarim Karimjee(1906 โ€“1977)

Mtoto wa Yusufali Karimjee, alikua Naibu Meya wa Dsm mwaka 1952 na 1956 na pia Meya wa Dar es Salaam mwaka1954 na 1957.Ila 1959 alichqguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanganyika kuelekea Uhuru(Tanganyika Legislative Council).Na baada ya Uhuru ndo akawa Spika wa kwanza wa Bunge la Tanganyika huru wakati huo vikao wanafanyia Karimjee Hall kabla Bunge halijahamishiwa Dodoma. Wakati huo wabunge walikua wanateuliwa tu na walikua 29 tu. Baadae wakaja wabunge wa kuchaguliwa kwa kura na wakaongezeka kufikia 81.

1961โ€“70, amekua Makamu mkuu wa University College of Dar es Salaam, Mkurugenzi wa National Development Corporation (NDC) na National Bank of Commerce (NBC) pia ndio Muanzilishi wa Tanganyika National Library.

View attachment 1519989
Karimjee Hall, March 19610
hii familia nahisi inajua historia ya nchi hii kuliko
 
Nilisoma Historia Primary School tu ila baada ya Hapo ni Ufundi(Mazengo na kina Ngwea) na Science kwenda mbele

Ni Hobby tu[emoji16][emoji16]
Aiseee
Kweli ni hobby.

Nilitaka nianze kulisingizia somo bure[emoji1787][emoji1787]
Kumbe umesoma na Ngwea eeh!?!
Wadogo zangu nyie wa 1980's

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom