JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Screenshot_20211213-133232.jpg
 
RIP Nicco Ye Mbajo

Tasnia ya Bongokomiki imepata pigo baada ya mmoja kati ya wachoraji wakongwe nchini Mzee Nicco Ye Mbajo kufariki dunia. Mzee Mbajo amefariki dunia usiku Jumamosi kuamkia Jumapili ya juzi jijini Dar es salaam.

Jina la Nicco Ye Mbajo linaweza kuwa geni kwa baadhi ya wapenzi wa Fasihi kutokana na kuwa kimya kwa kipindi kirefu kidogo lakini kazi za ubunifu wake hazijawahi kuacha kujulikana na mpenzi yeyote wa majarida ya kiswahili nchini.

Sidhani leo kama yupo Mtanzania yeyote mpenzi wa kusoma majarida ya Kiswahili nchini asiyelijua Jarida la SANI ambalo nathubutu kusema ndiye Baba wa Majarida yote ya burudani na vikaragosi nchini tangu mwanzoni mwa miaka ya 80.

Jina la SANI lilikuwa ubunifu wa muunganiko wa kifupi cha majina mawili ya mwanzo ya waasisi wa Jarida hilo ambao ni marehemu Saidi Bawji na Nicco Ye Mbajo, yaani SA (Saidi) na NI (Nicco). Marehemu Nicco ye Mbajo ndiye alikuwa mchoraji wa kwanza kabisa wa SANI.
Amezikwa Jana tarehe 27/11/2021 makaburi ya kinyerezi, bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.View attachment 2015154View attachment 2015155
Eeeeeh bwana weh....shikamoo sani
 
Back
Top Bottom