JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Screenshot_20220101-174841.jpg
 
Huyu ndiye SHEKILANGO na namna alivyopoteza maisha

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri inaitwa 'Shekilango Road',
Baranara Hiyo inaanzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki,
Ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.
Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango,
Imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango,
Aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala,
Wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.
Hussein Shekilango Ni mtu wa Tanga alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kupitia Jimbo la Korogwe Mjini Mkoani Tanga Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975,
Kabla ya kuwa mbunge SHEKILANGO alikua Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).
Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala),
Akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.
Unaweza kujiuliza kumbe na sisi Tanzania Bara tulikua na cheo Cha makamo wa pili wa Rais,
Jibu Ni ndio,enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Rais,
Rais wa Zanzibar alikua makamo wake wa kwaza wa Rais na Waziri mkuu wa Tanzania Alikua anaitwa makamo wa pili wa Rais,
Lakini alikua anafanya majukumu ya Uwaziri Mkuu,
Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini,
Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa,
Na Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979,
Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Iddi Amin wa Uganda,
Na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani.
Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani,
Huku sababu ikiwa ni kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ndugu Godfrey Binaisa.
Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri,
Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa,
Huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji.
Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda,
Ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.
Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda,
Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria,
Sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.
Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo,
Hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe.
Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.
Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.
Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule,
Huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni,
Ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971.
Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.
Katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo,
Rais Nyerere wakati huo alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha.
Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.
Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa,
Ambapo Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha,
Vifo hivyo vilomsikitisha Sana Nyerere huku wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.
Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi,
Huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa.
Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.
Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu,
Mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha kwa uchapa kazi wake.
Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.
Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa,
Iliamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Screenshot_20220102-072917.jpg
 
Austro-Hungarian officer showing his basic equipment (revolver, gas mask, grenades etc.), Galicia-Eastern front, 1915.
FB_IMG_1641116752740.jpg
 
Mapinduzi yalikula watu wake! Baadhi ya vichwa hapo "vilipotea" katika mazingira ya kutatanisha na wasijulikane wapo wapi au angalau yalipo makaburi walimozikwa hadi leo

Miongoni wa waathirika hao ni pamoja na Abdulaziz Twala, Mdungi Ussi(hayupo pichani) na Abdallah Kassim Hanga
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]kumbukumbu nzuri
 
Charles Njonjo alizaliwa 1918.
Huku Kenya anajulikana kama na jina The Duke of Kabete. Mwana wa Chifu Njonjo alikua Attorney General wa Kwanza Kenya wakati Kenya ilipojinyakulia Uhuru. Inasemekana alikua na nguvu (authority) mingi kwa serikali ya Kenyatta. Alikua ya uwezo ya kufunga mtu jela bila ata kesi kusikizwa.
Inajulikana pia ndiye aliyepigania Moi kuwa Rais baada ya kifo ya Kenyatta akieleza kuwa katiba ya Kenya lazima ifuatwe kinyume na watu wa kabila yake ya wakikuyu walio kuwa karibu sana na Jomo Kenyatta. Charles Njonjo alikua amependezwa na maisha ya ulaya hata hakuwa anajipanga kuoa. Inasemekana Mzee Jomo Kenyatta ndiye aliyemsukuma na kuoa mwanamke mwenye asili ya uingereza 1971 akiwa na miaka karibu 50.
Alipofikisha miaka 100 apo 2018, aliulizwa siri ni nini ya kuishi muda huo kiutani akajibu usioe mapema. Njonjo alaumiwa na wengi kusambaratisha Jumuiya ya Africa Mashariki. Amekua akiishi maisha ya chini na ndiye amekua the only surviving person kwa serikali ya Uhuru ya Kenyatta.
Inasemekana ameaga tu ivi punde akiwa na miaka 101.
Screenshot_20220103-094606.jpg
Screenshot_20220103-094554.jpg
Screenshot_20220103-094542.jpg
 
Pio Gama Pinto.
Alizaliwa 1927 na Kufa 1965. Alikua mwandishi wa habari, mwanasiasa na mpigianiaji Uhuru wa Kenya. Pio Gama Pinto alikua mwenye asili ya kihindi. Wazazi wake walikua wafanyakazi wa Serikali ya kikoloni ya Kenya. Alipelekwa India kwa masomo ambapo alianza kupigania haki za wanafunzi wa wafanyakazi wa chuo hicho.
Alirudi Kenya kwa mwanzo wa kipindi wa kupigania Uhuru na alikua akiandika articles (riwaya) za kueleza ubeberu wa ukolono. Mwaka wa 1954 miezi tano tu baada ya kutoa mkewe Emma, Pinto alitiwa mbaroni na kufungwa kwa kujihusisha na maswala ya MAUMAU. Alikaa kizimbani hadi 1961 alipoachwa huru na kujiunga na Kanu. Wakati Kenya ilipopata Uhuru 1963, Pinto alichaguliwa kama Mbunge wa Parklands kwa sasa Westlands Nairobi. 1965 alipigwa risasi kwa Gate ya Nyumba yake akiwa na mmoja wa binti wake na kuaga dunia. Alikua mtu wa kwanza mwenye high profile kuuawa baada ya Kenya kujinyakulia Uhuru.
Sababu yake kuuawa Kulingana na Ujasusi ni kujihusisha na siasa ya communist bali wengi huhusisha kifo chake na serikali ya awamu ya kwanza kwa kuzingatia haki haswa swala ya ardhi.
Baada ya kifo ya Pinto, Mkewe Mjane Emma Pinto alihamia kuishi Canada na mabinti wake watatu. Emma Pinto aliaga 2020.
Screenshot_20220104-072815.jpg
 
Pio Gama Pinto.
Alizaliwa 1927 na Kufa 1965. Alikua mwandishi wa habari, mwanasiasa na mpigianiaji Uhuru wa Kenya. Pio Gama Pinto alikua mwenye asili ya kihindi. Wazazi wake walikua wafanyakazi wa Serikali ya kikoloni ya Kenya. Alipelekwa India kwa masomo ambapo alianza kupigania haki za wanafunzi wa wafanyakazi wa chuo hicho.
Alirudi Kenya kwa mwanzo wa kipindi wa kupigania Uhuru na alikua akiandika articles (riwaya) za kueleza ubeberu wa ukolono. Mwaka wa 1954 miezi tano tu baada ya kutoa mkewe Emma, Pinto alitiwa mbaroni na kufungwa kwa kujihusisha na maswala ya MAUMAU. Alikaa kizimbani hadi 1961 alipoachwa huru na kujiunga na Kanu. Wakati Kenya ilipopata Uhuru 1963, Pinto alichaguliwa kama Mbunge wa Parklands kwa sasa Westlands Nairobi. 1965 alipigwa risasi kwa Gate ya Nyumba yake akiwa na mmoja wa binti wake na kuaga dunia. Alikua mtu wa kwanza mwenye high profile kuuawa baada ya Kenya kujinyakulia Uhuru.
Sababu yake kuuawa Kulingana na Ujasusi ni kujihusisha na siasa ya communist bali wengi huhusisha kifo chake na serikali ya awamu ya kwanza kwa kuzingatia haki haswa swala ya ardhi.
Baada ya kifo ya Pinto, Mkewe Mjane Emma Pinto alihamia kuishi Canada na mabinti wake watatu. Emma Pinto aliaga 2020.View attachment 2067734
+254 wapo vizuri kwenye mambo ya kutangulizana kwa nguvu RIP Prof Saitoti and John Michuki
 
Back
Top Bottom