JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Uzi mzur

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
Anaitwa Céline Dion Amezaliwa Charlemagne,Quebec"Canada Mwaka 1968 Ni Mwimbaji Na Mtunzi Wa Nyimbo Mashuhuri Za Pop Kutoka Nchini Canada Alianza Kuimba Mnamo Mwaka 1980 Anatunzo 243
World's Best Female Artist, Best Live Act World's Best Entertainer of the Year "World's Best Song N.k
Kwasasa Anasumbuliwa Na Kansa.
FB_IMG_1661217204275.jpg
 
George Justus Morara. Alizaliwa 1936. Alichaguliwa kama mbunge wa Mugirango Magaribi na raia wa sehemu hiyo 1969. Kwa wakati huo alikua mbunge mwenye umri mdogo kwa wabunge wote waliochaguliwa.
Ni miongoni wa walio faidika na programme ya Mboya kuelekea kusoma ulaya. Morara ni miongoni wa wale waliohuzunishwa na Kifo ya mboya.
Mwaka wa 1970 inasemekana alizuru nchi ya Zambia na alipokua Lusaka, alikutana ana kwa ana na Nahashon Njenga aliyempiga Tom Mboya risasi na kumuua. Aliporudi Kenya alisema bila uoga kuwa Nahashon Njenga hakunyongwa kama vile mahakama iliamuru na serikali ilimtorosha Zambia. Aliipa serikali muda wa Masaa 48 Nahashon akaletwe Kenya akahukumiwe. Siku iliyofuata alizuru Mji wa Kakamega ulioko eneo ya Magaribi mwa Kenya. Alipokua kwa gari akirudi nyumbani kwake Mugirango, gari Lake iligongwa na gari ya polisi ya kenya ikiegemea mahali alipokua ameketi. Alikufia papohapo.
Wengi huona hii Nyota ingine kuu ilizimwa na serikali.View attachment 2054009
Ila nakumbuka jina la muuaji huyo lilikuwa Isaak Njenga Njoroge.
 
Kuna kampuni zamani ilikuwepo ilikuwa inaleta vifaa mbalimbali toka UK ilikuwa inaitwa saida tujenge chetu,walikuwa wanaleta vitu quality

Ova
Hao walikuwa ni STC kwa kirefu State Trading Corporation na walitumia hili la Saidia Tujenge Chetu kama kaulimbiu yao ya biashara. Ni moja ya Mashirika ya awali Sana ya Umma baada ya Azimio la Arusha.
 
Haya mambo yalikuwa yanaleta ubishi sana kwa wapiga Kura. Badala ya kuchagua mtu wapo waliochagua ama picha ya nyumba au jembe. Wengi wa huko vijijini walipendelea jembe kwani maisha Yao yalitegemea hilo. Wa mijini tukachagua nyumba kwani maisha bila nyumba mijini ilikuwa balaa. Baadae tukaletewa picha za kuku na yai. Tatizo likabaki palepale. Watu wakiulizana kuwa kati ya yai na kuku nani kamzaa mwenzie?
 
Back
Top Bottom