JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Mwaka 2005 ndo tunaama kariakoo na kuamia airport na chanika. Mtaani hapo tuna gorofa letu. Mkataba unaisha 2025 linakua la kwetu. Hahah New Billionaire 2026 [emoji23][emoji23]. RIP Mama na Baba maana waliupiga mwingi sana zama zao [emoji41]
Big up sana kwao.. Wapumzike kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Big up sana kwao.. Wapumzike kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
Nmekumbuka mbali sana. Miaka iyo TV Analogy ipo kwetu tu Mtaa mzima wanangalia ngumi za mike iron tyson alfajiri kibarazani kwetu. Watu kibao 😂. Dah huu uzi utunzwe. Nikioata mda ntashare picha za home ntumba ya udogo ila nje imepigwa simenti. Juu ya dali miti mikubwa kama ya chooni.
Sisi kizazi cha yanga na ccm. 😂😂 nyumba za udongo za kariakoo
 
Nmekumbuka mbali sana. Miaka iyo TV Analogy ipo kwetu tu Mtaa mzima wanangalia ngumi za mike iron tyson alfajiri kibarazani kwetu. Watu kibao [emoji23]. Dah huu uzi utunzwe. Nikioata mda ntashare picha za home ntumba ya udogo ila nje imepigwa simenti. Juu ya dali miti mikubwa kama ya chooni.
Sisi kizazi cha yanga na ccm. [emoji23][emoji23] nyumba za udongo za kariakoo
Sisi kizazi cha yanga na ccm. [emoji23][emoji23] nyumba za udongo za kariakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kushoto Mjusi Shemboza katikati Da Tunu(Marehem)na kulia ni Agrey Ndumbalo(Marehem) ndani ya Vijana Social "Vijana Day" enzi zileeeee
FB_IMG_1695264762048.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MSALA WA UTEKAJI NDEGE 1982


Februari 26, 1982, Bongo ilitikisika baada ya kutokea taarifa kuwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) imetekwa. "Bongolanderz" nchi nzima walipogwa butwaa. Lilikuwa ni tukio la kwanza la aina yake kuwahi kutokea katika nchi hii na kuzua mijadala kote duniani.

Pichani ni mateka waliorejea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dsm Machi 4, 1982 baada ya kimuhemuhe kikubwa. Mateka hao walipokewa kama mashujaa na ndugu zao, viongozi wa CCM na serikali ambapo vikundi vya ngoma vya Bora, JKT & NHC vilitumbuizam

Miongoni mwao ni vijana watano walioteka ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Tanzania (ATC) aina, Boeing 737 ikiwa mjini Mwanza.

Huo ulikuwa ni utekaji wa kwanza wa aina yake tangu ATC lilipoanzishwa Ijumaa ya Machi 11, 1977 baada ya kuvunjika kwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki (EAA) Januari 1977 na kisha kufa rasmi Jumanne ya Februari 1, 1977.


Utakaji wa ndege hiyo ulikuja siku moja baada ya kutekwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kuwait, Alhamisi ya Februari 25, 1982. Ndege hiyo ilitekwa katika ardhi ya Beirut, Lebanon ikirejea kutoka Libya. Ilikuwa na abiria 150.

Pamoja na kwamba utekaji wa kwanza wa ndege katika anga la Tanzania ulifanyika mwaka 1972 na mwingine ukafanyika mwaka 1979, huu wa Februari 1982 ulikuwa wa kipekee kabisa na—ingawa ulikuwa ni utekaji uliohusiana na siasa—Serikali ya Tanzania haikutaka ijulikane hivyo.

Msala ulivyokuwa

Saa 11:00 jioni ya Ijumaa ya Februari 26, 1982, baada ya kuagana na ndugu, jamaa na marafiki, abiria kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza waliingia katika ndege ya ATC iliyokuwa na jina la Kilimajaro ubavuni mwake.

Kwa wasafiri wengi, Uwanja wa Ndege wa Mwanza haukuwa na sifa nzuri kutokana na kukosa usalama kiasi cha baadhi ya marubani kuutaja kama “kituo cha basi”.

Kulikuwa na makundi ya kawaida ya watu uwanjani hapo kama ilivyokuwa siku zote kwa wasafiri wa Mwanza—Dar es Salaam. Wengi wao walikuwa ni wale wenye asili ya India, Waarabu na wazawa wachache. Pamoja na kwamba mambo yote yaliyonekana kuwa ya kawaida, kulitokea jambo dogo ambalo liliifanya safari ya ndege hiyo isiwe ya kawaida.

Boeing 737 ilipaa angani saa 11:20 ikielekea Dar es Salaam na ilitarajiwa kuwa ingetumia dakika 90, kutembea umbali wa takriban maili 500 kufika, lakini ikageuka kuwa safari ya juma zima na umbali wa kiasi cha maili 9,500—tena wakati wote abiria na wafanyakazi wa ndege hiyo wakiwa chini ya ‘mtutu wa bunduki’.

Dakika tano tu baada ya ndege hiyo kupaa angani, vijana wanne walisimama ghafla kwa wakati mmoja. Mmoja wao alijipenyeza kwa kasi hadi chumba cha rubani, kisha akaelekeza ‘bastola’ yake kwenye kichwa cha mmoja wa marubani, Kapteni Deo Mazula, na kumuamuru awapeleke Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Mussa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na nduguye Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Ilikuja kujulikana pia kuwa kiongozi wao alikuwa ni Mussa Memba.

Wakati huohuo, watekaji nyara wengine, huku wakipunga ‘bastola’ bandia zilizotengenezwa kwa vigogo vya miti na ‘mabomu’ ya kutupwa kwa mkono, waliwatangazia abiria kuwa wao ni viongozi wa ‘Vijana wa Harakati za Mapinduzi Tanzania’ na kwamba shabaha yao ni “kuhakikisha kuwa Rais Julius Nyerere anajiuzulu”.

Wakati hayo yakitokea, Mwalimu Nyerere alikuwa Ikulu jijini Dar es Salaam akijiandaa kurejea nyumbani kwake baada ya kupokea risala kutoka kwa chipukizi waliomuahidi kuwa wataendelea “kuwa watiifu, wakakamavu na wenye bidii kwa kuwa tunafahamu mchango wetu unahitajika sana katika ujenzi wa nchi”.

Hadi wakati anaondoka ofisini kurejea nyumbani kwake akiwa amefurahishwa na risala iliyosomwa na mwenyekiti wa Taifa wa chipukizi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahenga wenzangu mnamkumbuka kikosi hiki
Je mhenga mwaka 1976 ulikuwa darasa la ngapi mwaka huo?
Wale waliopata Bahati ya kukiona kikosi hichi hongereni sana
Kutoka kushoto Aloo Mwitu
Marehemu Jumanne Hassani Masiment
Mohamedi Kajole Machela (RIP)
ABDALLAH Mwinyimkuu (RIP)
Saudi Salum
Meneja wa timu Abdrahaman Hamisi (Muchacho)
Waliochumaa kutoka kushoto Shaban Baraza
Athmani Juma (RIP)
Ally Aluu
Omari Mahadhi (RIP)
Martin Kikwa (RIP)
ABDALLAH Kibadeni
Abbas Dilunga (RIP)
Mohamedi Bakari Malima Tall
FB_IMG_1695371152536.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
!! Oliver mamaa,, mwanakwetu eeh,,sikiliza Oliver nikupashe,,yanayonisibu moyoni juu yako Oliiver oyo yoo mama eeh«Nilipokutana nawe japo mara ya kwanza,,tabasamu lako limeshtua penzi langu,,tangu siku ile hutoki moyoni mwanguu Oliiver ,»Nataraji jibu lako kutovunja moyo wangu,, tafadhali tafadhali likubali ombi languu Oliiver oyo yoo mama eeh«»pamoja mimi na wewe,,tuwakabili wazazii,,kwa kutaka zao radhii.,tupate zao baraka Oliiver oyo yoo mama eeh,«»Tukikubaliwa uwe mke wangu,,ntakuvisha pete ,,pete ya harus ,,usitie shakaa OLIVER OHOO.«»Dah kwa mistari hii ya BITOZ WA ENZI HIZO WA MITAA YA KARIAKOO,,ZAHIR ALLY ZORO (DISASTER) Tausi mrembo lazma ang'ate kucha huku akiangalia chini sio mchezo enzi hizo,,pesa haikuwa na nafasi kubwa kama penzi la moyooniii
FB_IMG_1695371598158.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wale wahenga wanakumbuka
nakala ya Hemedi kimwanga

CELINA i moja ya nyimbo Alizovutia mno kwenye miaka ya sabini kiasi cha watu kudai kwam ba ulikuwa ni wimbo wa "dikedi yaani wimbo bora kwa kipindi cha miaka kumi "cash"

Ni kweli kabisa; kwani urunzi wake uliwagusa wengi, mipigo yake hali kadhalika. Mtunzi naye, haya Joseph Mulenga aligusa pale am- bapo kila binadamu huguswa kiasi cha kuufanya wimbo huu uonekane kana kwamba mi dira kwa wale wazee wenye tabia mbaya; tabia ya kuingilia ndoa za wana wao.

Kama kawaida, nami leo nausawiri wimbo huu ih usakafishe ujumbe ambao tayari ulikuwa umewafikia watu, tangu wana hadi wazazi na jamii nzima kwa ujumla.

Lakini kabla hatujaanza usawiri wake, hebu kwanza tuangalie mashairi yake yanavyosema: Naja najua, una mawazo. Lakini tutafanyaje ikiwa wazazi wako wameamua hivyo. Nia yangu na mudinumuni vangu. Ilikuwa tufunge ndoa na tuishi sote kama mke na mume Celina. Nimejitahidi jadri ya uwezo wangu eeeh. Wazazi wako waliniwekea vikwazo vingi; Celina.

Naam; hali nd'o hiyo mwakwetu. Ukisema huo ni Uswahili, wengine wanasema unatukana Ukisema ni "ukalamba"; wengine wanadai un akashifu. Ilimuradi mambo ni shagalabaghala.

Lakini ukweli wenyewe ndivyo ulivyo. Kwanini wapenzi waingiliwe katika mapenzi yao? Ah, msemo wa Sunna Muana Kambi, Usimwingilie alopewa, hata ukijanya chuki hawezikukumegea

Naam; hata nami nakubali. Vipi umwingilie yule alopewa haki yake na Rabuka! Usongombingo ulioje huo! Wajuaji wanasema, ukiona mtu anamwingilia mwenzake basi ujue ana lake. Kuna jambo ambalo limemkera kiasi kwamba hapendi mwenzake huyo afaidike.

Vitabu vitukufu vinasema. kwamba ndoa ina hadhi sawa na nyumba ya Mungu; yaani L'Kaaba. Mtu mwenye nia nzuri ya kufunga ndoa, amepewa uzito wa kui- heshimu nyumba hiyo. Sasa anapotokea binadamu kuvunja ndoa hiyo au kuzuia isifungwe kwa hiyana, sijui mtu huyo anakuwa

katika upande gani! Kwa sababu, kulingana na vitabu hivyo hivyo vitukufu, wale waliokusudia kuivunja L'Kaaba wakati huo, Mwenyekiti Mungu aliwashushia videge vidogo vilivyokuwa vimebeba vigololi vya moto kutoka Jehanamu. Unayajua matokeo yake mwak-

Kama unayajua si vibaya

t

Celina

kokukumbusha, lakin kama huyajul: kaa chonjo niknete Basi wale adufuki walio w wakienda kubomoa nyumba hin Al-Kahar, Al-Qudus na buha hu Wata'ala wakiwa na Tenby wakubwa, walidondoshes golob hivyo vya moto vichwani mwa bapo kwapo, waligeuka masivu tan- gu wao waliokuwa kweuve Terobo

Rekodi niliyoisikia

Na Hemed Kimwanga

hadi Tembo wao..

Hiyo ilikuwa imebakia pima elfu tu za nyayo za miguu wailikie nyumba hiyo na kutimiza azma yao. Lakini kama isemwavyo kwenye vitabu hivyo vitukufu kwamba Mwenyezi Mungu ni mweza wa kila jambo liwe juu ya ardhi an ndani yake, juu ya mbingu au ndani yake, ndivyo hawakufanikiwa. ilivyokuwa;

Upo hapo, awakwetu? Sasa vipi wewe mwenzangu mimi uzuie ndoa au uvunje ndoa ya wawili walopen- dana au wawili wapendanao?

Ah, msemo wa bibi yangu yangu mama Lumwanga, mvunja ndoa and doa. Naam; hata nami nakuba- li. kama walovunia L'Kaaba

wadigroka wajin, Nuys

Na kata ans doe ambapo kines meyama

Lakins Морева kupiga moyo Knapovuruges Waswahili Wakage hao, Ikeridhi aki hakuna Hivyo, chochote kinaweza kufany wa na mtu huy

Ndipo hapo mwenzeta bayo Mulenga akasema hivi wakati alipokuwa na bendi ya Miomon Park Orchestra, No two sabab ekuwa hiyo, son: sababu ya kuto ka ujue kwa ajili yang Ston sababu ya kutaka ujchinje kwa ajili yangu

Maneno hayo ni mazuri sana fakini kama tulivyoona hapo mwan kwamba "mapenzi yane nguvu kuliko nguvu" usione ajabu mu akalanya chochote kile ndani kivuli cha penti

Unaambiwa penzi linamithilika na vipito vya maji ya mito ambazo hupoza koo lililochoka na kuhahe Awu kiu. Penzi hupoca ghadhahu zu mfu ukawa ni kama nyeku aliyek fa Penci iamsha nguvu za no kuwa kuno kwamba ni wa asili au sharubat mbao binadamu ameumbiwa kuumilik kwa ajili ya ufalme wake

Upo hapo, Mwakwetu? Kama hivvo ndivyo, basi ndugu yangu usichete na penci. Penzin kaci ma kuti ni mtu. Kwahiyo, kwa kifupi. penzi ni uhutadamu alioumbiwa masharti yote na Mola wetu Jalia sisi sote tuweze kuiona njia njema ya kwenda kwake hiyo siku ya siku.

Ingawaje Waswahili husema. hakuna anayekusakana ndani ya nyumba bila ya napishi mazuri, wazazi wetu angalie i tena upya ku husu kuingilia mapenzi ya wanent

Baadhi ya sisi wazazi ni wakoro Ii sana. Tunapenda sana kuingilia mapenzi ya wanetu kwa ngao ya radhi. Aghalabu tumesahau kabisa kuwa enzi tuliyonayo ni ya kisasa. Zile nyakati anthapo mwanamke alisubiri kupe swa na ma asiyemta hata wakaishi na kuzaa watoto japo kwa kikembe sasa zimekwisha

Kadhalika zile nyakati ambapo wazazi walikuwa wakioza binti zao kwa wana wa matajiri au wana wa fulam ni zo zimepita. Nyakati hize mi zile ambapo vijana hawakawa

FB_IMG_1695412987906.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAREHE 8/5/1980, BAND YA ORCHESTRA BIMA LEE ILIINGIA STUDIO YA TBC NA KUFYATUA KIBAO KINACHOKWENDA KWA JINA LA “UHURU WA ZIMBABWE” KILICHOTUNGWA NA BELESA KAKELE.
HAPA NI KABLA YA UJIO WA WANAMUZIKI, JOSEPH MULENGA, ABDALAH GAMA, SULEIMAN MWANYIRO NA SHAABANI DEDE KAMCHAPE KUTOKEA MLIMANI PARK, NA KUASISI MTINDO MPYA WA MAGNETO TINGISHA KATIKA BAND HIO YA BIMA LEE.

NIFUATE SASA:

BAND:_ Orchestra Bima Lee.
WIMBO:_ Uhuru wa Zimbabwe. 1980
MTUNZI:_ Belesa Kakele.
WAIMBAJI:_ Belesa kakele, Roy Bashekanako, Jumbe Batamwanya, na Omary Kayanda.
SOLO GITAA:_ David Mazanda.
SEC/SOLO:_ Joseph Zengula.
RIZIM GITAA:_ Duncan Ndumbalu.
BASS GITAA:_ Rajabu Urembo.
TUMBA:_ Said Mohamedi.
SAXOPHONE:_ Omary Kayanda.
KINANDA:_ Kassim Magati.

MASHAIRI YAKE:

Ohooo, tufurahi leo Zimbabwe sasa iko huruuu, kama....mtu kulilia chakeeee, mwishoee mungu hamnyimi mtuuu...ndoto za walowezi kulilia ardhiii...za mwafrika zimefika mwishoooo.

FB_IMG_1695550444750.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom