JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Dar 1931,Kushoto ni Railway station
FB_IMG_1700021065389.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matema Beach SCANIA 113K HP310, A.K.A BUSTAR, Injini Nyuma, ifuate upotee, Ilikuwa haikamatiki enzi zake hasa kwenye milima, ikitangulia imetangulia, ni hatari tupu. Ni kampuni chache sana ndizo zilipata kumiliki Toleo hili la Scania, baadhi ni MATEMA BEACH, ABOOD, KISWELE NA AIR MSAE. Karibu sana.View attachment 2797612

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeona hapo "LOVE IN ACTION"
 
KAMA DUNIA INGEKUWA NA UKUBWA WA JUPITER BAS INGEKUWA NGUMU KWETU SISI KUTOKA NJE YA DUNIA YETU

Pengine kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa mara mbili au tatu ya ukubwa wake wa sasa basi ingekuwa ni ndogo kwetu sisi wanadamu kutoka nje ya dunia yetu

Acha nikwambie embu tuchukulie kwa ukubwa wa sayari yetu ambapo huanza kujihesabu kuwa tupo nje ya dunia yetu pale tunapokuwa tupo umbali wa kuanzia km 100 kutokea usawa wa bahari ambapo kwa kasi ya 40,000 kilomita kwa saa ndio inayohitajika .

Ambapo kwa ukubwa wa rocket zetu na kwa kiasi cha nishati kinachobeba basi ni sawa na ni salama kabisa kuwezesha wanadamu na mizigo kwenda nje ya dunia yetu .

Sasa unadhani ingekuwaje kama dunia yetu ingekuwa na ukubwa kama sayari ya jupiter na je unadhani safari za kwenda anga za mbali zingewezekana kweli

Kwa jambo hilo lisingewezekana kabisa kwa sababu kadhaa ambapo moja wapo ni sababu ya umbali na kani kubwa ya uvutano ambayo dunia yetu ingekuwa nayo na tunafahamu kuwa kadri gimba linavyokuwa na ukubwa mkubwa basi ndio kani ya uvutano nayo inavyozidi kuwa kubwa sana

Sayari ya jupiter ina kani ya uvutano wa 24.76 m/s² ambapo ili uweze kutoka nje ya sayari hiyo ya jupiter basi hutahitaji rocket au chombo chenye kasi ya 214,200 kilomita kwa saa ambapo ni kasi kubwa sana kabisa .

Na kama tukitaka kuweza kupata kasi kama hiyo basi inatubidi tuwe na rocket kubwa sana pengine ni mara 10 ya rocket ambazo tulizokuwa nazo kwa sasa jambo ambalo lisingewezekana

Ni wazi kabisa ilituweze kusafiri kwa kasi kubwa sana basi kiasi kikubwa cha nishati ndio kitakapokuwa kinahitajika , sasa kwa ukubwa huo wa rocket na kwa maumbo yetu haya ya wanadamu sidhani kama tungeweza kufanikiwa kwa hilo .

Sasa kama gimba litakuwa kubwa sana basi nafasi ya kuwa na wingi wa matabaka mazito ya anga hewa ambapo ni ngumu sana kwa chombo kuweza kukatisha katika maeneo hayo kasi kubwa inahitajika ili kuweza kukatisha katika maeneo hayo .

Pengine ingekuwa ni hadithi kwa sisi kuweza kutoka nje ya dunia yetu kama ingekuwa na ukubwa kama wa sayari ya Jupiter .

#AstronomyKiswahili
FB_IMG_1700047626042.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MUNAMKUNBUKA YULE MWANAMKE ALIYEKWENDA KUMUOKOA RAMBO KWENYE MOVIE YA FIRST BLOOD II??

BASI NDIYO HUYU HAPA ASEE ANAITWA JULIA NICKSON, KUSHOTO NI ALIVYOKUWA MWAKA 1985 WAKATI MOVIE INATOKA NA KULIA NI ALIVYO SASA NI TAKRIBAN MIAKA 38 IMEPITA LAKINI ONA CHUMA HICHO BADO KIBICHI KABISAA UTAFIKIRI NI MIAKA 21 HIVII.

ANASIFIKA KWAKUWA NA UWEZO MKUBWA WA MARTIAL ARTS KANAPIGA HAKO KAONE HIVYO HIVYO TUU TOO BAD HAKUPEWA MUDA WA KUTOSHA KATIKA ILE MOVIE MAANA ALIKUFA MAPEMA BAADA YA KAMANDA WA KIVIETNAM KUMMIMINIA RISASI ZA KIFUA, NOMA SASA HII MOVIE HUKU KIBONGO BONGO NA KIAFRICA RAMBO TULIMTAMBUA KWA MSURURU WA MOVIES HIZI ZA FIRST BLOOD I& IV.

NAAAM.
FB_IMG_1700078681217.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Special Sleeping Coach enzi zake, Dar Njombe Songea na pia Dar Lindi Nachingwea Mtwara miaka ya 90. Aliyebuni hizi ngao sidhani kama alijua kuwa zitakuja kuwa na matumizi mengi sana zaidi ya lile la kuweka ulinzi mbele kwenye gari, kwani zilitumika kwa mambo mengi sana, kama kukalia si unawaona hao vijana wa zamani hapo mbele, kuanikia nguo, kupakilia madebe ya mahindi, kupakilia baiskeli, vitanda na vitu vingine vingi tu....
FB_IMG_1700109297197.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Special Sleeping Coach enzi zake, Dar Njombe Songea na pia Dar Lindi Nachingwea Mtwara miaka ya 90. Aliyebuni hizi ngao sidhani kama alijua kuwa zitakuja kuwa na matumizi mengi sana zaidi ya lile la kuweka ulinzi mbele kwenye gari, kwani zilitumika kwa mambo mengi sana, kama kukalia si unawaona hao vijana wa zamani hapo mbele, kuanikia nguo, kupakilia madebe ya mahindi, kupakilia baiskeli, vitanda na vitu vingine vingi tu....View attachment 2815059

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dar es Salaam 1910 - Mitaa ya Posta Mpya na Askari Monument. Monument ya Hermann von Wissmann iko hapo kati ya picha halafu Hoteli ya Kaiserhof (sasa ni Hoteli ya New Afrika) iko upande wa kushoto na Kanisa la Azania Front kwa mbali. umemcheki babu anasukuma mkokoteni kwa kutumia punda
FB_IMG_1700194529249.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Malorry yakisafirisha mizigo yenye usiri mkubwa(top secret cargo) kuipeleka ndani kambi ya kijeshi yenye usiri mkubwa sana ndani ya marekani maarufu kama Area 51 [emoji3518][emoji3518] mwaka 1962 hapo Groom Lake, Nevada mizigo hiyo imetengenezwa na kampuni.ya Lockheed…..[emoji851][emoji851][emoji851][emoji1783]

#EnziZìle...
FB_IMG_1700292158769.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom