JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Mjengo wa kijerumani ulioondolewa kupisha mjengo mpya wa bank of South Africa na baadaye kutaifishwa na kuwa National bank of commerce(Sokoine drive)Dar es salaam.
FB_IMG_1704840661257.jpg
FB_IMG_1704840666323.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni mwaka 2009 nikiwa na CHELEA MAN pamoja na PNC wakiwa wamoto kabisa kutoka kundi la TIP TOP CONNECTION chini ya BABU TALE tukiwa tumemaliza kupiga show katika wilaya ya KONGWA-DODOMA,Baada ya kumaliza show tulileteana mzozo mkubwa na CHELEA MAN wakati wa kugawana mapato kitu ambacho kilisababisha kila mtu harudi kivyake hotelini lakini kulivyokucha asubuhi CHELEA MAN akanipigia cm Ili tuende tukayamalize na ndipo tulipoaamua kuyamaliza na kila mtu akachukua chake kwahyo hiyo picha tulipiga baada ya kuyamaliza,daaa inanikumbusha mbali sana..View attachment 2861619

Sent using Jamii Forums mobile app
So wewe ndo nani hapo? Uliyevaa raba nyeupe?
 
Hizi TDK, SONY, MAXELL NA PHILIPS ndo' zilikuwa tapes(zikiitwa kanda au kaseti) za kisawasawa kwa miaka mpaka mwishoni mwa '80 kabla ya ujio wa kaseti za Goldstar na brand nyingine.
Kaseti hizo zilikuwepo za dakika 60 na dakika 90.
FB_IMG_1704877596561.jpg
FB_IMG_1704877592537.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
SPLENDID HOTEL, Acacia St, Dar 1950s

Hii ni Hoteli ya Prince of Wales ambayo baadae ilikuja itwa Hoteli ya Splendid ilikuwa mtaa wa Acacia St. (Picha ya 1 ilipigwa mwaka 1950 na ya 2 ilichukuliwa mnamo 1961).

Acacia St sasa ni Samora Ave. Hoteli hii ilibomolewa na kujengwa jengo la Extelecoms Bldg. Hoteli maarufu ya Maggot unaweza kuiona upande wa kushoto (jengo jeupe picha ya 2). Laiti kama majengo ya kikoloni yangehifadhiwa leo yangekuwa na thamani kubwa na ingekuwa hazina kubwa kwenye utalii.
FB_IMG_1704937867340.jpg
FB_IMG_1704937870817.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ni miaka ya 70 mwishoni wakati huo barabara ikiitwa Independence Avenue. Wakati wa Ukoloni barabara hii iliitwa Acacia Avenue, baada ya Uhuru ikaitwa Independence Avenue, na Baadaye ikaitwa Samora Avenue kwa kumuenzi Mwanamapinduzi Samora Machel wa Msumbiji aliyefariki dunia 1986 kwa ajali ya ndege, jina linalotumika mpaka leo hii.
FB_IMG_1704938096078.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Askari Monument mwaka 1950. Hizo barabara mbili hii ya kushoto kipindi hicho iliitwa Acacia Avenue siku hizi inaitwa Samora Avenue na barabara hii ya kulia kipindi hicho iliitwa Windsor Street na sikuhizi inaitwa MAKUNGANYA Street, pembeni yake hapo mwanzo tu, siku hizi kuna wachonga Mihuri wengiii, ukipita hapo wanakukaribisha upate huduma yao, na jengo hilo hapo kulia kwenye kona ni jengo la HAJI Brothers, bado lipo na hivi sasa linatumiwa na Benki ya Posta Tanzania..
FB_IMG_1705358760791.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
WASWAHILI

We were taught in school that Kiswahili came about by mixing Arabic with various Bantu languages. However, that was not true. When the Arabs and Europeans arrived at the East African coast they found the Waswahili/Wangozi people speaking Kingozi/Kiswahili. Kiswahili/Kingozi was an old language with many dialects.

Kiswahili is a local language that originated in Lamu, Kenya. The grammar is a 100% bantu which makes it an African language. The source of Kiswahili was Kingozi language that was spoken by Wangozi. Wangozi today are known as Waswahili and they are organized in form of clans which they call 'Mbari'. The 10 Waswahili clans and 41 sub-clans. The clans and sub-clans are as follows:

1. MBARI ZA WAKILINDINI

Mbari ya Mwinyi Nguti wa Mwinyi Mwinzagu
" Mwinyi Humzi
" Mwinyi Kombo wa Dani
" Mwinyi Kae wa Pembe
" Mwinyi Hudumzi

2. MBARI ZA WATANGANA

Mbari ya Mwinyi Muli
" Mwinyi Mjaka
" Mwinyi Umbwi
" Mwinyi Ngwisa

3. MBARI ZA WACHANGAMWE

Mbari ya Mwinyi Kitue
" Mwinyi Mgosi
" Mwinyi Mfaki
" Mwinyi Koba
" Mwinyi Ngovo

4. MBARI ZA WAMVITA

Mbari ya Mwinyi Kutani
" Mwinyi Kae
" Mwinyi Hunziali

5. MBARI ZA WAMALINDI

Mbari ya Banu Shasha
" Banu Mbwana

6. MBARI ZA WAJOMVU (au WAJUNDA)

Mbari ya Mwinyi Faki
" Mwinyi Chande wa Shamaniya
" Mwinyi Usi Muhija
" Mwinyi Uledi wa Ndau
" Mwinyi Jaa wa Mwinyi Nguti

7. MBARI ZA WAMTWAPA

Mbari ya Mwinyi Nyali (au Mbari ya Ng'ombeni)
" Mwinyi Jimve
" Mwinyi Goziadi
" Mwinyi Rakwe
" Banu Muyaka
" Banu Shemapwe

8. MBARI ZA WAKILIFI

Mbari ya Mwinyi Shoka
" Mwinyi Kiwanda
" Mwinyi Mkomati
" Mwinyi Gome

9. MBARI ZA WAPATE

Mbari ya Wa-Pate
" Wa-Amu
" Wa-Kitau
" Wa-Twaka
" Wa-Tikuu
" Wa-Kipungani
" Wa-Barawa
" Wa-Shela

10. MBARI ZA WAGUNYA (au WABAJUNI)

Mbari ya Washaka
" Wa-Uziwa
" Wa-Ungama
" Wa-Ozi
" Wa-Sada

These clans speak different Kiswahili dialects depending on where they are found, especially in Kenya, Comoros, Mozambique, Somalia & Tanzania. The dialects are:

1. Shikomor spoken Comoros

2. Kiamu, Kipate & Kingozi are spoken in Lamu,

3. Chijomvu, Kimvita, Kingare, Kimrima, Kiunguja, Mambrui, Chichifundi, Chwaka & Kivumba are spoken in Mombasa,

4. Kipemba, Kitumbatu, Kimakunduchi, Mafia, Mbwera, Kilwa (extinct) & Kimgao are spoken in Pemba.

Oldest Kiswahili/Kingozi dialects include:

1. Kimwani which is spoken in the Kerimba Islands and northern coastal Mozambique

2. Chimwiini which is spoken by the ethnic minorities in and around the town of Barawa on the southern coast of Somalia.

3. Kibajuni which is spoken by the Bajuni minority ethnic group on the coast and islands on both sides of the Somali–Kenyan border and in the Bajuni Islands (the northern part of the Lamu archipelago) and is also called Kitikuu and Kigunya

4. Socotra Swahili (extinct) and

5. Sidi in Gujarat, India (possibly extinct)

As speakers of Kiswahili language we are owed this information. We should not be speaking a language whose origin we don't clearly know.
FB_IMG_1705657988558.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ulikuwa hujui,

Picha inaonesha Mwaka 1972, Dar es Salaam Rais Jaffery Nimeiry wa Sudan akikagua wachezaji wa Taifa Stars waliokuwa vifua wazi. Kapten Abrahaman Juma akimtambulisha kwa Omary Zimbwe, Mohamed Chuma, Kitwana Manara na Abdalla KIbadeni. Rais J. K. Nyerere alikuwa Jukwaa Kuu. Inasemekana, Jezi za Taifa Stars zilikuwa zimepelekwa kwa Mganga wa Kienyeji ili ishinde siku ya mechi. Meneja wa Taifa Stars alizifuata lakini bahati mbaya hakumkuta Mganga nyumbani kwake, Kwakuwa alikwenda na basi la timu, ilibidi wachezaji waende uwanja wa Taifa kwa miguu toka Hosteli ya Jeshi la Wokovu, Kurasini. Meneja wa taifa stars alikuwa ni Chambanga H. Dyamwale mnamo 1972. Kutokana na fedheha hiyo kubwa, inasemekana Rais Nyerere alisusa kukanyaga tena mpirani.

Tulianza na mkosi toka zamani [emoji41][emoji119][emoji460]
IMG-20240120-WA0000.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom