Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaitwa Theresa ShayoKilimanjaro Hotel 1969.
Fashion show.
Huyo mbantu sijui atakuwa nani?View attachment 2896433
Sent using Jamii Forums mobile app
Type writer hiyoNani anajua kitu hiki na alikiona lini mara ya mwisho?
View attachment 2898324
Hawa majamaa walikuwa wazalendo kwa Tanganyika kuliko sisi wabantuWatu wengi wanaijua Karimjee Hall tu. Hawajui kwanini iliitwa hivyo.
View attachment 1519983
Karimjee Hall ya sasa
View attachment 1519987
Familia ya Yusufali Karimjee
--Yusufali Karimjee (1882–1966)
Alijulikana pia kama ‘Lion of Zanzibar’. Alikua boonge la mfanyabiashara.Alifanya biashara toka Bongo,Hanover(Germany) hadi Japan, na alioa mwanamke wa Kijapani. Kupitia kwa mwanae Abdulkarim walitoa zawadi ya huo ukumbi kwa Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1955
--Abdalla Mohamedali Karimjee (1899–1978)
Mdogo wake na Yusufali ambaye alijulikana pia kama "Sisal baron of Tanga" na alishatunukiwa na malkia OBE (Officer of the British Empire) mwaka 1961. Mwaka 1924 alisafiri kwa pikipiki toka Bongo mpaka South Africa kwenda ku"negotiate" mkataba wa kusambaza mafuta na kampuni ya Caltex
Alikuja kuwa Mbunge baadae bunge la Tanganyika(Legislative Council) na pia alihudhuria kutawazwa kwa Queen Elizabeth II mwaka 1953.Princess Margaret alishawahi kuja kumtembelea kwake Tanga mwaka1956.Alioa pia mke wa pili Mjerumani
--Tayabali Karimjee (1897-1987)
Mdogo wa mwisho wa Yusufali. Huyu alizaliwa na kusoma Zanzibar na alikua rafiki wa karibu wa Sultan. Pia Sultan alimteua kuwa Mbunge(Legislative Council Zanzibar) ila alisusia Bunge na kutoka nje ya Bunge baada ya kupitishwa Clove Monopoly Bill ya 23 Julai 1937. Akiwa na msimamo kwamba hio sheria inawanufaisha zaidi Wazungu.
--Abdulkarim Karimjee(1906 –1977)
Mtoto wa Yusufali Karimjee, alikua Naibu Meya wa Dsm mwaka 1952 na 1956 na pia Meya wa Dar es Salaam mwaka1954 na 1957.Ila 1959 alichqguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanganyika kuelekea Uhuru(Tanganyika Legislative Council).Na baada ya Uhuru ndo akawa Spika wa kwanza wa Bunge la Tanganyika huru wakati huo vikao wanafanyia Karimjee Hall kabla Bunge halijahamishiwa Dodoma. Wakati huo wabunge walikua wanateuliwa tu na walikua 29 tu. Baadae wakaja wabunge wa kuchaguliwa kwa kura na wakaongezeka kufikia 81.
1961–70, amekua Makamu mkuu wa University College of Dar es Salaam, Mkurugenzi wa National Development Corporation (NDC) na National Bank of Commerce (NBC) pia ndio Muanzilishi wa Tanganyika National Library.
View attachment 1519989
Karimjee Hall, March 19610