Abrianna
JF-Expert Member
- Mar 30, 2021
- 4,696
- 15,390
Very interestingUzee ni uhalisia na hauepukiki , huwa hatma ya kila mtu. Hali hii huwa inakaribia hatua ya mwisho ya maisha ya binadamu, lakini mwanasayansi wa maumbile David Sinclair anakanusha mtazamo huo.
Kwa mujibu wa utafiti ambao umefanywa zaidi ya miongo miwili, anasema kuwa kuna uwezekano wa kuzuia mtu kuzeeka mapema, kwa kuzingatia mambo kadhaa ili kuweza kumfanya mtu kuwa na afya njema kwa muda mrefu.
Sinclair anaamini kuwa muda si mrefu itawezekana kuondoa uzee kwa kutumia dawa pia , ambazo bado ziko kwenye majaribio kwa ajili ya lengo hili na labda tutaweza kuondoa uzee.
Mwanasayansi huyo ambaye ni daktari kutoka chuo kikuu cha Australia, na taasisi ya teknolojia ya Massachusetts ya Marekani anafanya kazi katika maabara ya chuo kikuu cha Harvard ambako anafanya utafiti wa kwanini tunazeeka.
Amepata tuzo kadhaa za kisayansi kutokana na kazi yake. Na hata amekuwa mtu maarufu. Amepigiwa kura kama miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani jarida la Time magazine liliandika .Jarida hilo lina wafuasi wa twitter ambao ni karibu 200,000.,
Mtafiti pia ana wagonjwa 35 na alianzisha kampuni kadhaa za kisayansi, baadhi yazo zimejikita katika kuchelewesha watu kuzeeka au kuzuia uzee.
Sinclair pia ni mwanndishi wa kitabu cha Lifespan kinachoangalia matarajio ya siku za kuishi , kiliibuka kuwa kitabu kinachonunuliwa zaidi.
Aliandika kuhusu imani maarufu ya uzee kutoepukika.
Mwanasayansi huyo anaamini kuwa ni lazima tubadili mitazamo yetu ya jinsi tunavyofikiri kuhusu umri: badala ya kuona kuwa ni mchakato wa kawaida tu na kuwa ni jambo asilia, tunapaswa kuona kuwa huo ni ugonjwa ambao unaweza kutibiwa na ukapona.
Sinclair anasema haya ni mabadililko makubwa katika mtazamo wetu juu ya uzee ambao unaweza kusaidia kuongeza muda wa kuishi.
Na kuachana na imani potofu kuwa lazima kila mtu azeeke.
Vilevile anasema , tiba inaweza kutusaidia kuishi miaka mingine zaidi , inapidi tuzingatie hilo kwa umakini.
Kwanini tunazeeka?
Wanasayansi wameainisha sababu tisa zinazoweza kusababisha uzee, na katika utafiti wake wa miaka 25 iliyopita, tulipata ushahidi kuwa miongoni mwa ushahidi uliopatikana ni kuwa ushahidi mmoja unasababisha tatizo lingine na inajumuisha na kupoteza taarifa.
Tuna taarifa za aina mbili kuhusu miili yetu , moja ni umeirithi kutoka kwa wazazi wetu na pili ni kuathirika na mazingira na muda.
Nadhani hizi ndizo sababu zinazotufanya tuzeeke.
Unasema hatuhitaji kuwa wazee, kwanini?
Hakuna sheria ya kibailojia inayosema lazima tuwe wazee. Hatujui jinsi ya kuachana na dhana hii lakini tunaweza kuwa bora zaidi kama tukipunguza hili.
Na maabara inaweza kufanya mchakato huo.
mCHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Jinsi tunavyoishi kila siku kuna athari kubwa katika maisha yetu ya kila siku na hata kupunguza siku za kuishi.
Kufanya kitu kwa usahihi kunaweza kumfanya mtu asizeeke kwa haraka.
Katika utafiti wetu wa wanyama kama panya na hata papa na tembo ambao wana mifumo tofauti ya maisha na wanaweza kuishi katika miaka tofauti
Zaidi ya hayo, zaidi ya 80% ya afya za siku zetu zijazo zinategemea jinsi tunavyoishi na wala sio vina saba-DNA.
Kuna mambo ambayo wanasayansi wameyagundua kwa watu wanaoishi muda mrefu.
Yakiwa yanajumuisha aina sahihi ya chakula na kiasi ambacho mtu anakula, kutokula chakula chenye mafuta mengi au mtu akila kidogo mara nyingi anaweza kuishi zaidi.
Mazoezi pia yanasaidia.
Na kuna wale ambao wanadhani kubadilisha nyuzi joto la maji ni muhimu pia.
Namna gani mambo haya yanasaidia kupunguza muda wa kuzeeka?
Sababu inayowafanya wanasayansi kuamini kuwa aina fulani ya maisha inaweza kusaidia mwili kupambana dhidi ya ugonjwa wa uzee.
Ni vyema kuanza kula mlo kamili
Kujihisi baridi, kuhisi hasira na kushindwa kupumua pia ni njia nyingine za kupata kinga thabiti.
Utafiti unaamini kuwa kama mtu akifanya mazoezi vizuri na kula chakula sahihi kutasaidia kupunguza kasi ya uzee.
Uzee unasababisha magonjwa mengi sana kama ugonjwa wa moyo, kisukari na magonjwa mengine.
Hivyo wazo la kumfanya mtu kuwa kijana , litaweza kumfanya aweze kuishi muda mrefu zaidi.
Katika utafiti uliochapishwa hivi karibuni katika jarida la Nature limezungumzia suala la watu wa kale kuishi miaka mingi.
Hii ikionesha kuwa kutokana na shughuli tunazozifanya, hatuwezi kuchelewesha uzee au kuzuia watu kuzeeka.
Miaka 200 iliyopita, binadamu alikuwa ana uwezo wa kutembea kwa kasi ya farasi.
Kuna teknolojia ambazo tunaweza kuzitumia na kutatua tatizo hilo na kufanya maisha yawe bora zaidi.
Source: BBC