JF True Life Stories: Unaikubali ipi kati ya hizi?

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Jf ni ulimwengu murua sana, una kila aina ya real life time experiencies, yani ukiwa humu unakuwa ni kama unaiona dunia na yanayoendelea ndani mwake.

Kuna true stories kadhaa zimeletwa na wadau humu jf, ni true stories zenye utamu na msisimuko wa hali ya juu. Ni stori ambazo zitakufurahisha na kukupa fundisho pia.

Baadhi ya simulizi kali ni hizi hapa:

1. Ya kwanza ni ya member anaitwa KigaKoyo, hii ni ya mapenzi, ilianzia kwenye uzi wa kula tunda kimasihara. Baada ya kuvutia wasomaji ikabidi iunganishwe itengenezewe uzi kabisa ambao ameupost JBourne59.

2. Ya pili ni ya member anaitwa jooohs. Hii ni ya mambo ya giza. Jamaa baada ya maisha kuwa magumu ilibidi ajaribu upande wa pili wa shilingi lakini alichokutana nacho......

3. Ya tatu na ambayo bado haijakamilika ni ya member anaitwa jerrybanks ambayo pia inahusu mambo ya nguvu za giza. Hii sasa ndio fungamwaka maana ni mkasa unaosisimua mnoo. Huu mkasa unapatikana kwenye uzi wa "kama ulishawahi kushuhudia nguvu za giza live". Kama bado hujaupitia kaupitie huu mkasa hutojutia muda wako.

4. Ya nne ni ya mtukutu Analyse. Huyu jamaa toka azaliwe ni mtukutu mnoo, toka kuangusha kondomu mbele ya darasa mpaka kufukuzwa seminari kwa kuiba nguruwe[emoji851]. Kaipitie hautojutia.

5. Ya tano ni ya mtu mzima Bossless. Jamaa aliyeshuhudia live vita ya kikabila ya Rwanda iloyosababisha mauaji ya halaiki. Inatisha lkn kuna mengi ya kujifunza


Najua hii mikasa imesomwa na watu wengi sana maana ni nyuzi zenye views 40K+ na comments 2K+. Je ipi kati ya hizo true life stories imetisha zaidi?
 
Jerrybank ni muongo hua anatunga visa, Mtoe kabisa. Kisa nachokipenda ni cha mkuu Analyse kina motivation kubwa.
Kwa mkuu kigakoyo stori yake ndani kama unasoma between lines utaona kuna Fasihi/utunzi pia.
Lakini pia stori ya mzee wa bao 23 Jbourne69 iko poa sana unahisi upo Enzi hizo za 70s.
 
Nimesoma ya joohs mpaka nikawa nahisi nimo kwenye story. Jamaa alisimulia mpaka watu wakawa wanaota usiku daahh.

Ila mkuu kuna story moja ya mzee bossless kuhusu vita vya wanyarwanda na yenyewe ni moto wa kuotea mbali.
 
Story zipo nyingi, fanya collection kwanza iliyokamilika

Kuna story ya Maisha ya Analyse n.k

Kama umeamua kuleta collection umiza kichwa na wewe, angalau uorodheshe hata Uzi/stories 15
Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Ngoja niiongeze hapo juu.
Nimesoma ya joohs mpaka nikawa nahisi nimo kwenye story. Jamaa alisimulia mpaka watu wakawa wanaota usiku daahh.

Ila mkuu kuna story moja ya mzee bossless kuhusu vita vya wanyarwanda na yenyewe ni moto wa kuotea mbali.
 
Pia nyingine ni hizi "ulishawahi kusaidiwa/kumsaidia mtu usiyemfahamu?",hii ina simulizi nzuri sana,pia kuna hii "kwa tuliowahi kufungwa gerezani...."
 
Sijasoma hizo zingine lakin ile simulizi wa mauaji ya Rwanda ilinivutia, maana alisimulia ambayo hatukuwahi kuyasikia. Wacha nizitafte na hzo zingine ambazo zinasifiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…