Jf ni ulimwengu murua sana, una kila aina ya real life time experiencies, yani ukiwa humu unakuwa ni kama unaiona dunia na yanayoendelea ndani mwake.
Kuna true stories kadhaa zimeletwa na wadau humu jf, ni true stories zenye utamu na msisimuko wa hali ya juu. Ni stori ambazo zitakufurahisha na kukupa fundisho pia.
Baadhi ya simulizi kali ni hizi hapa:
1. Ya kwanza ni ya member anaitwa KigaKoyo, hii ni ya mapenzi, ilianzia kwenye uzi wa kula tunda kimasihara. Baada ya kuvutia wasomaji ikabidi iunganishwe itengenezewe uzi kabisa ambao ameupost JBourne59.
2. Ya pili ni ya member anaitwa jooohs. Hii ni ya mambo ya giza. Jamaa baada ya maisha kuwa magumu ilibidi ajaribu upande wa pili wa shilingi lakini alichokutana nacho......
3. Ya tatu na ambayo bado haijakamilika ni ya member anaitwa jerrybanks ambayo pia inahusu mambo ya nguvu za giza. Hii sasa ndio fungamwaka maana ni mkasa unaosisimua mnoo. Huu mkasa unapatikana kwenye uzi wa "kama ulishawahi kushuhudia nguvu za giza live". Kama bado hujaupitia kaupitie huu mkasa hutojutia muda wako.
4. Ya nne ni ya mtukutu Analyse. Huyu jamaa toka azaliwe ni mtukutu mnoo, toka kuangusha kondomu mbele ya darasa mpaka kufukuzwa seminari kwa kuiba nguruwe[emoji851]. Kaipitie hautojutia.
5. Ya tano ni ya mtu mzima Bossless. Jamaa aliyeshuhudia live vita ya kikabila ya Rwanda iloyosababisha mauaji ya halaiki. Inatisha lkn kuna mengi ya kujifunza
Najua hii mikasa imesomwa na watu wengi sana maana ni nyuzi zenye views 40K+ na comments 2K+. Je ipi kati ya hizo true life stories imetisha zaidi?