JF Woman and Man of The Year 2010: Mchakato Wa Kuwapata

JF Woman and Man of The Year 2010: Mchakato Wa Kuwapata

Ni Nani Anafaa Kuwa "JF Man of the Year 2010"?

  • Acid

    Votes: 23 40.4%
  • Kiranga

    Votes: 12 21.1%
  • Nyani Ngabu

    Votes: 22 38.6%

  • Total voters
    57
  • Poll closed .
Watu wote humu JF ni anonymous mtawapaje hizo zawadi?
 
Wanabaraza na Wana Jamii Forums;

Tume ya Uchaguzi ya JamiiForums (JEC) inapendekeza kwanza upitie thread ifuatayo ili kuweza kupata mchakato wa hapa tulipofika:

https://www.jamiiforums.com/celebri...-of-the-year-2010-mchakato-wa-kuwapata-4.html

POLL inayofanyika sasa ni kwa ajili ya kumpata JF WOMAN OF THE YEAR 2010 na pia JF MAN OF THE YEAR 2010.

Zawadi zitatolewa kwa mshindi wa kila Category.

Katika POLL hii inafanyika baada ya Wadau wa JF kupendekeza majina mbalimbali katika kila category, na baada ya kupitia post zote za mapendekezo JEC imechagua wale watatu wa mwanzo waliopata kura nyingi kutoka katika kila category (MAN Category kura zilifungana, kwa hiyo wako 4). Washindi hawa wa kura za maoni sasa tunawapambanisha kupitia upigaji kura yaani JF POLL.

Mwaka huu tofauti na mwakajana itatolewa zawadi yenye hadhi fulani kwa washindi ili kutoa changamoto za umakini katika mabandiko haba jamvini. Tutajulishana zawadi hizi mara tu washindi watakapopatikana baada ya mchakato wa Kupiga kura.

Vigezo vifuatavyo vizingatiwe katika kupiga kura yako:

1. Unayempigia kura awe ni Mwana JF aliyebobea hasa kutokana na Threads alizozianzisha na pia post alizozianzisha. Vyote lazima viwe na impact chanya kwa wasomaji wa JF

2. Awe ni mwenye uwezo wa kusimamia hoja zake na kuzijibu kikamilifu bila jazba na kwa umahiri wa hali ya juu pale ambapo anapata challenge toka kwa wachangiaji.

3. Awe ni mwenye ushawishi wa hali ya juu katika mabandiko anyochangia walau kwa muonekano wa wachangiaji kuunga mkono hoja zake.

4. Asibobee kwenye Jukwaa moja tu. Walau awe mchangiaji mzuri wa majukwaa yasiyopungua matatu

5. Asiwe mtu wa shari katika majibizano kiasi cha kupelekea Mods kumpa "BAN".

6. Aonekane wazi katika mabandiko yake anaweza akahisiwa kuwa Kiongozi Mzuri.

7. Awe Mchangiaji ambaye ni active walau mara moja kwa wiki. Ikiwa zaidi ni vizuri zaidi.

8. Awe ni mtu asiyeogopa kukemea mabandiko yenye lengo la kutukana, kudhalilisha, kubagua, kuleta mfarakano na kutokuelewana baina ya wanachama wa JF.

UPIGAJI KURA:

Mchakato wa Kupiga kura za kumpata JF Man of the Year 2010 and JF Woman of the Year 2010 umeshakamilika. Kura za maoni zimefungwa rasmi Ijumaa 3-12-2010 Saa 6.00 Usiku. Sasa kura zinapigwa kwa wafuatao ambao wamepita katika kura za maoni:

Chagua moja kati ya majina yafuatayo ambayo yamepitishwa na JEC kuingia rasmi kaatika POLL ya kutafuta JF MAN OF THE YEAR 2010:

1. Acid - Kura 2
2. Kiranga - Kura 2
3. Mwanakijiji - Kura 2
4. Nyani Ngabu - Kura 3

Pia katika Thread nyingine tofauti; Chagua moja kati ya majina yafuatayo ambayo yamepitishwa na JEC kuingia rasmi kaatika POLL ya kutafuta JF WOMAN OF THE YEAR 2010:

1. Regia Mtema - Kura 2
2. Gaijin - Kura 2
3. Woman of Substance - Kura 2

Wote mnahimizwa kutumia haki yenu ya kikatiba kwa kumpigia kura mgombea unayedhani amekidhi matarajio yako.

Maoni yanakaribishwa kuelezea sababu la chaguo lako na maoni menine ya kujenga.
Hii post sioni umuhimu wake hapa kwenye thread ya polls kwani ina influence fulani kwa wapiga kura... Kama ni kurahisisha ufuatiliaji nafikiri kama ni member active atakuwa kafuatilia mchakato toka mwanzo au angeweza kuchakata mwenyewe kuona nani anafaa kati yao kwa anaweza kusearch threads na kuona nani anafaa kulingana na vigezo vilivyowekwa. Ila tutavote hivyo hivyo
 
Mkuu Kuberwa, unge-take trouble kidogo kusoma thread hii vema ungegundua kuwa yote unayoyasema yamezingatiwa na watu wameshafanya research tayari. Hebu zingatia hili:

Tume ya Uchaguzi ya JamiiForums (JEC) inapendekeza kwanza upitie thread ifuatayo ili kuweza kupata mchakato wa hapa tulipofika:

https://www.jamiiforums.com/celebriti...uwapata-4.html
 
Kura ni haki yako ya msingi ya JF. Piga kura yako sasa.
 
Kuna habari za kuaminika nimezipata kwenye mtandao kuwa kuna mwana JF amekamatwa na FBI (with conspiracy, bank fraud, wire fraud and Mortgage Fraud Scheme)

Kwa kuwa MaxShimba umerejea hewani naomba umjibu X-PASTER tuhuma hii aliyotoa, stay blessed!
 
Namfagilia sana WOS ambapo napendekeza females wenzake wanaotaka kujua masuala muhimu ya kiuongozi na jamii wamfate awafunde. she is good.
ana KITU huyo mwanamke
 
Namfagilia sana WOS ambapo napendekeza females wenzake wanaotaka kujua masuala muhimu ya kiuongozi na jamii wamfate awafunde. she is good.
ana KITU huyo mwanamke

Mkuu, umeshapiga kura yako?

Na hiyo "KITU" aliyonayo ni nini hasa Mkuu? Kuwa muwazi zaidi.
 
Tueleze zawadi gani watapata??
au nazo tutazipigia kura?
 
Tueleze zawadi gani watapata??
au nazo tutazipigia kura?

Mkuu, bado tunapokea ahadi. Kwa sasa kuna mfadhili moja tu amejitokeza kuwa atatoa laki moja.

Ningependa wafadhili wajitokeze zaidi.
 
Mkuu Kuberwa, unge-take trouble kidogo kusoma thread hii vema ungegundua kuwa yote unayoyasema yamezingatiwa na watu wameshafanya research tayari. Hebu zingatia hili:

Tume ya Uchaguzi ya JamiiForums (JEC) inapendekeza kwanza upitie thread ifuatayo ili kuweza kupata mchakato wa hapa tulipofika:

https://www.jamiiforums.com/celebriti...uwapata-4.html
Nilifuatilia sana mchakato, nlichokuwa worried nacho ni ile kuweka nani kapata kura ngapi hapa kwenye thread hii. Vigezo pekee vngetosha bila idadi ya kura kutoka mchakatoni. Kama mtu angetaka kuona mchakato ulienda vip, angerefer hiyo link ulotoa. Anyway, maji yashamwagika tuendelee na voting. Thanks
4
 
Point taken Mkuu.

Nimeongea na Makamisaa, wana hoja kwako kama unaweza kujiunga na JEC. Please confirm.
 
Point taken Mkuu.

Nimeongea na Makamisaa, wana hoja kwako kama unaweza kujiunga na JEC. Please confirm.
Asante kwa hilo. Kwa sasa nsha vote sijui kama bado naqualify. Nsijeonekama kuwa biased bure. Kama nna qualifikesheni poa tu hamna noma
 
Mods kama kuna uwezekano tungeomba hii mui-Sticky ibaki juu.
 
Mpaka sasa Mchuano ni kati ya Mwanakijiji na Acid
 
Back
Top Bottom