Jiandaeni kisaikolojia kushuhudia haya kwenye mchezo wa Tanzania prisons vs Simba SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
(1) makosa ya kibinadamu kutoka kwa marefa/waamuzi wa mchezo watakaochezesha huo mchezo.

(2)kadi za njano nyingi sana zitatolewa kwa Tanzania prisons mpaka kadi nyekundu kabisa.

(3) Penalty/Tuta ya mchongo ni Jambo la kawaida kutolewa na Simba sc watanufaika nalo.

Mwisho wa dakika 90 Simba sc wataondoka na pointi tatu muhimu haijalishi wamezipata vipi.
 
Mmeshaanza Malalamiko FC
 
GSM akishirikiana na uongozi wa Prisons umetoa motisha katika timu yao ili kuepuka kichapo leo dhidi ya Simba.

Katika kikao kilichofanyia viongozi pamoja na wadau wametoa ahadi ya sh 25milioni kwa wachezaji endapo watapata Ushindi dhidi ya Simba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hii NI Mara ya kwanza kufanya hivi hao Tanzania prisons hata wakicheza na YANGA huwa wanapewa motisha.
 
Umeongea vitu ambavyo vinategemeana:

1:Kadi za njano nyingi - hupelekea kuwepo kwa kadi nyekundu

2:Makosa mengi (rafu). Hupelekea adhabu kama kadi(ya njano/nyekundu)-na faulu/penati.

3:Timu ikayocheza rafu nyingi zaidi hupelekea refa kufanya maamuzi mabovu dhidi yao; hii hupelekea kitu kinaitwa makosa ya kibinadamu.

NB:Other factors remain constant.
 
Aibu
 
Bado unateseka na N. Tegere na Charles Ilamfya au unateswa na unbeaten? Uliwafunga wale wakimbizi wa Sudan ambao hawajala mwezi mzima ukaona dunia yote yako. Sasa kiko wapi?
 
Mwisho wa dakika 90 Simba sc wataondoka na pointi tatu muhimu haijalishi wamezipata vipi.
Mmmeanza kumuelewa mnyama kuwa pointi tatu ni muhimu! Tulishawaambia hayo kuwa kwa sasa tunachoangalia ni ushindi. Mbwembwe nyingine baadaye. Endeleeni tu kumiliki mchezo kwa 98% dhidi ya 2% za Ihefu.
Narejea kauli yako:
"pointi tatu muhimu haijalishi wamezipata vipi."
 
Umekunywa supu lakini?
 
Your browser is not able to display this video.
 
Bado hamjasema
 
4.sisi Utopolo tumeroa bahasha ya sh 25 milioni ili Prisons wakamie.

Jambo Moja ntakubaliana na wewe kadi zitakuwa nyingi kwa Tz Prisons sababu kwa kukamia watajikuta wanacheza rafu nyingi na mbaya, badala ya kucheza mpira watacheza watu. Hivyo kadi njano na hata NYEKUNDU sitashangaa.

Nb: Yanga inajua bila Simba kupoteza hawana ubingwa. Wanatumia njia zozote na njia pendwa yao Ni bahasha.
 
Simba hatunaga konakona. Tanzania prison ni timu ndogo sana kufanyiwa hayo.
 
Naona umeanza kutafuta visingizio mapema ili Simba ikishinda uhalalishe maneno yako ila ikifungwa, "game lilikuwa fair" .
Haki itendeke tu.
 
Hayo yote yanawezekana kutokea kwa sababu Priosons watatumia nguvu nyingi kwa kuwa hawataweza kupishana na Simba muda! Ni lazima watacheza rafu nyingi sana na itawazimu kuadhibiwa na mwamuzi! Jana Ihefu walifanikiwa sana kuuelewa mfumo wa Yanga na ndio maana walifanikiwa ila niliona aibu kuona washabiki wa timu kubwa wanamrushia chupa za maji golikipa wa timu ndogo baada ya kuonyesha uimara wake wa kulinda lango lake! Yule golikipa alikua na siku bora sana kazini kwake jana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…