Jiandikishe kugawa viungo vyako uishi milele

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kule marekani huwa wanaitwa donors, mtu anajiandikisha kwenye orodha maalum ambapo anatoa ridhaa yake mwenyewe kwamba pindi atakapofariki basi immediately viungo vya mwili wake kama ini, moyo, mapafu,figo nk. vivunwe mara moja na kuhifadhiwa kabla havijaharibika ili vitumike kuokoa maisha ya watu wengine ambao watakuwa wanavihitaji.

Kwa upande wa pili kuna kuwa na orodha ya nyingine ya wagonjwa ambao wana-apply kwa ajili ya kupata hizo donors parts pindi zitakapokuwa available. Utaratibu huu umeshaokoa maisha ya malaki ya watu duniani, hasa kwa wale wenye kuhitaji kuwekewa moyo au figo mpya.

Faida zake;

Licha ya kwamba huokoa maisha ya watu, pia hupunguza bajeti ya afya kwa taifa kiujumla, mind you kumng'oa figo mtu aliyehai ili akupe wewe moja na yeye abaki na moja ni suala gumu sana, nilisikiaga kuna mtu alikuwa anauza figo yake kwa 90M,sishangai hata kidogo!

You can imagine jinsi tunavyofukia mabilioni kila siku chini ya ardhi kwenye makaburi! Ila pia moyo wako unapofungwa kwenye kifua cha mtu mwingine ni kwamba wewe bado unaishi ndani yake, na unaweza hata kum-influence huyo recepient akawa na bakshishi kama zako wakati upo hai, hivyo na yeye akija kuugawa tena basi ni kama unaishi milele!

In anycase, spare parts za binadamu ni ghali.., na haziuzwi hovyo madukani, hivyo, ili kulinda figo na ini inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya pombe. Ili kulinda mapafu inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku na bangi, pia ili kulinda moyo jitahidi either kupunguza ulaji wa kitimoto usio na tija au ukishindwa fanya mazoezi asubuhi na jioni, ni muhimu sana.

Cha kushangaza, serikali hutumia pesa nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na pombe na sigara kuliko kodi inayokusanya kutokana na sumu hizo, ni ajabu na kweli, hili liangaliwe upya.

DON FRANCIS


================================
Update: 15/03/2021

=================================
Update: 28/04/2021

==========================
Update: 14/08/2024

 
nataka kujua kwa upande wa dini kama si vibaya basi afadhali kuchangia kuokoa maisha ya watu wengine.
 
Nipo tayari,lakini nianze kupewa advance kabisa kabla mzigo haujachukuliwa,pia nina swali je viungo vya mtu aliyeishi miaka mingi let's say 80-90_au 100 vitafaa kwa mtu mwingine mwenye umri chini ya huo?
 
kumbe ngoja nifikiri kuishi milele au kupata pesa ?nitkuja na jibu nifanye evaluation
 
nanusa harufu ya wagonjwa mahututii kukatishwa maisha ili viungo vivunwe.
Sasa hilo ni suala la ethics.., inabidi tu madaktari wenyewe wawe na ubinadamu na wakumbuke viapo vyao.., other wise thats similar to murder, na sheria zipo!
 
Mimi namuachia urithi mwanangu viungo vyangu....nikifa alipwe 70m inatosha...hiyo ni discount nimetoa kubwa kabusa.
 
kwa mfano we umejitolea moyo, na mi nkaaply kuupata pale utapotangulia... huoni kuwa dua zangu kila siku itakua utangulie mapema na mi nchukue huo moyo!!!
 
kwa mfano we umejitolea moyo, na mi nkaaply kuupata pale utapotangulia... huoni kuwa dua zangu kila siku itakua utangulie mapema na mi nchukue huo moyo!!!

Fresh tu....ndo maana waswahili wanasema kufa kufaana.
 

Cha kushangaza, serikali hutumia pesa nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na pombe na sigara kuliko kodi inayokusanya kutokana na sumu hizo, ni ajabu na kweli, hili liangaliwe upya.

DON FRANCIS

Serikali ipi? Kama unamaanisha ya hapa kwetu nakushauri ukafanye upya research. Ukiumwa magonjwa hayo unayoyataja MAKE PEACE WITH YOUR MAKER labda wao wenye nchi ndio utasikia wamepelekwa India
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…