Jiandikishe kugawa viungo vyako uishi milele

Jiandikishe kugawa viungo vyako uishi milele

Na sisi tuanzishe zoezi hilo kwa kadri tuwezavyo.....!
 
Hiyo teknolojia inahitaji uwekezaji wa hali ya juu..Kwa nchi yetu itakuwa baadae sana!
 
Kule marekani huwa wanaitwa donors, mtu anajiandikisha kwenye orodha maalum ambapo anatoa ridhaa yake mwenyewe kwamba pindi atakapofariki basi immediately viungo vya mwili wake kama ini, moyo, mapafu,figo nk. vivunwe mara moja na kuhifadhiwa kabla havijaharibika ili vitumike kuokoa maisha ya watu wengine ambao watakuwa wanavihitaji.

Kwa upande wa pili kuna kuwa na orodha ya nyingine ya wagonjwa ambao wana-apply kwa ajili ya kupata hizo donors parts pindi zitakapokuwa available. Utaratibu huu umeshaokoa maisha ya malaki ya watu duniani, hasa kwa wale wenye kuhitaji kuwekewa moyo au figo mpya.

Faida zake;

Licha ya kwamba huokoa maisha ya watu, pia hupunguza bajeti ya afya kwa taifa kiujumla, mind you kumng'oa figo mtu aliyehai ili akupe wewe moja na yeye abaki na moja ni suala gumu sana, nilisikiaga kuna mtu alikuwa anauza figo yake kwa 90M,sishangai hata kidogo!

You can imagine jinsi tunavyofukia mabilioni kila siku chini ya ardhi kwenye makaburi! Ila pia moyo wako unapofungwa kwenye kifua cha mtu mwingine ni kwamba wewe bado unaishi ndani yake, na unaweza hata kum-influence huyo recepient akawa na bakshishi kama zako wakati upo hai, hivyo na yeye akija kuugawa tena basi ni kama unaishi milele!

In anycase, spare parts za binadamu ni ghali.., na haziuzwi hovyo madukani, hivyo, ili kulinda figo na ini inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya pombe. Ili kulinda mapafu inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku na bangi, pia ili kulinda moyo jitahidi either kupunguza ulaji wa kitimoto usio na tija au ukishindwa fanya mazoezi asubuhi na jioni, ni muhimu sana.

Cha kushangaza, serikali hutumia pesa nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na pombe na sigara kuliko kodi inayokusanya kutokana na sumu hizo, ni ajabu na kweli, hili liangaliwe upya.

DON FRANCIS


================================
Update: 15/03/2021

=================================
Update: 28/04/2021

Aliyomba/nunua /recipient akifa kabla ya donor hapo vipi?
 
Nipo tayari,lakini nianze kupewa advance kabisa kabla mzigo haujachukuliwa,pia nina swali je viungo vya mtu aliyeishi miaka mingi let's say 80-90_au 100 vitafaa kwa mtu mwingine mwenye umri chini ya huo?
Advance Muhimu
 
Aliyomba/nunua /recipient akifa kabla ya donor hapo vipi?
Orodha ya donors inakuwa ni kubwa, na orodha ya waombaji ni kubwa pia, sio one on one, na hujui ni nani au lini utampa/ au utapokea, ni kama bahati nasibu
 
mmh acha ntangulie na viungo vyangu... kuishi milele sio hivi

Mimi huu utaratibu hua nauona ni mzuri sana tu. Aftaroo hata ukizikwa na hayo maviungo yanaenda kuliwa na mafinyofinyo tu huko ardhini, bora hata usaidie kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzio.
 
Back
Top Bottom