Junior. Cux
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 5,319
- 3,786
Fresh tu....ndo maana waswahili wanasema kufa kufaana.
Moyo wa plastic tu huwa unafanya kazi.., itakuwa wa binadamu mwenzio? pata elimu hapa https://www.jamiiforums.com/habari-...vyofungwa-ndani-ya-kifua-na-kufanya-kazi.html
Inawezekana kabisa.., sema kuna hatari akawa kama wanaume wa Dar..
Fresh tu....ndo maana waswahili wanasema kufa kufaana.
Inawezekana kabisa.., sema kuna hatari akawa kama wanaume wa Dar..
NdioIvi inawezekana kuwekewa moyo kutoka kwa marehemu na moyo ukapiga kazi.nielimishwe hapo
Na sisi tuanzishe zoezi hilo kwa kadri tuwezavyo.....!
Mh Tanzania tunaweza kweli??
Hiyo teknolojia inahitaji uwekezaji wa hali ya juu..Kwa nchi yetu itakuwa baadae sana!
Ukifa wewe kwanza?kwa mfano we umejitolea moyo, na mi nkaaply kuupata pale utapotangulia... huoni kuwa dua zangu kila siku itakua utangulie mapema na mi nchukue huo moyo!!!
Aliyomba/nunua /recipient akifa kabla ya donor hapo vipi?Kule marekani huwa wanaitwa donors, mtu anajiandikisha kwenye orodha maalum ambapo anatoa ridhaa yake mwenyewe kwamba pindi atakapofariki basi immediately viungo vya mwili wake kama ini, moyo, mapafu,figo nk. vivunwe mara moja na kuhifadhiwa kabla havijaharibika ili vitumike kuokoa maisha ya watu wengine ambao watakuwa wanavihitaji.
Kwa upande wa pili kuna kuwa na orodha ya nyingine ya wagonjwa ambao wana-apply kwa ajili ya kupata hizo donors parts pindi zitakapokuwa available. Utaratibu huu umeshaokoa maisha ya malaki ya watu duniani, hasa kwa wale wenye kuhitaji kuwekewa moyo au figo mpya.
Faida zake;
Licha ya kwamba huokoa maisha ya watu, pia hupunguza bajeti ya afya kwa taifa kiujumla, mind you kumng'oa figo mtu aliyehai ili akupe wewe moja na yeye abaki na moja ni suala gumu sana, nilisikiaga kuna mtu alikuwa anauza figo yake kwa 90M,sishangai hata kidogo!
You can imagine jinsi tunavyofukia mabilioni kila siku chini ya ardhi kwenye makaburi! Ila pia moyo wako unapofungwa kwenye kifua cha mtu mwingine ni kwamba wewe bado unaishi ndani yake, na unaweza hata kum-influence huyo recepient akawa na bakshishi kama zako wakati upo hai, hivyo na yeye akija kuugawa tena basi ni kama unaishi milele!
In anycase, spare parts za binadamu ni ghali.., na haziuzwi hovyo madukani, hivyo, ili kulinda figo na ini inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya pombe. Ili kulinda mapafu inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku na bangi, pia ili kulinda moyo jitahidi either kupunguza ulaji wa kitimoto usio na tija au ukishindwa fanya mazoezi asubuhi na jioni, ni muhimu sana.
Cha kushangaza, serikali hutumia pesa nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na pombe na sigara kuliko kodi inayokusanya kutokana na sumu hizo, ni ajabu na kweli, hili liangaliwe upya.
DON FRANCIS
================================
Update: 15/03/2021
Wizara ya Afya yaandaa muswada wa kuvuna viungo vya watu, kama maini, figo, mapafu nk
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto imeanza kuandaa muswada wa sheria itakayosimamia uvunaji viungo vya binadamu zikiwemo figo, maini, moyo na mapafu ili vipandikizwe kwa wanaovihitaji. Ofisa katika kitengo cha magonjwa yasiyoambikiza katika Idara ya Tiba kwenye wizara...www.jamiiforums.com
=================================
Update: 28/04/2021
Serikali yaandaa Mswada wa taratibu za uvunaji na upandikizaji viungo vya binadamu
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema kutokana na kuongezea kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo. Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji...www.jamiiforums.com
Advance MuhimuNipo tayari,lakini nianze kupewa advance kabisa kabla mzigo haujachukuliwa,pia nina swali je viungo vya mtu aliyeishi miaka mingi let's say 80-90_au 100 vitafaa kwa mtu mwingine mwenye umri chini ya huo?
Orodha ya donors inakuwa ni kubwa, na orodha ya waombaji ni kubwa pia, sio one on one, na hujui ni nani au lini utampa/ au utapokea, ni kama bahati nasibuAliyomba/nunua /recipient akifa kabla ya donor hapo vipi?
Unajua maana ya ‘Donor/ Donation’?Naulizia Malipo,Kiasi Gan nalipwa Kama Fidia kabla Sijafa
mmh acha ntangulie na viungo vyangu... kuishi milele sio hivi