Da!!!!! kwa hali hii,hii ikipita, sintolewa tena na kutembea barabarani,,,unaweza kugongwa na gari makusudi ili wakakuvune figo!!Kule marekani huwa wanaitwa donors, mtu anajiandikisha kwenye orodha maalum ambapo anatoa ridhaa yake mwenyewe kwamba pindi atakapofariki basi immediately viungo vya mwili wake kama ini, moyo, mapafu,figo nk. vivunwe mara moja na kuhifadhiwa kabla havijaharibika ili vitumike kuokoa maisha ya watu wengine ambao watakuwa wanavihitaji.
Kwa upande wa pili kuna kuwa na orodha ya nyingine ya wagonjwa ambao wana-apply kwa ajili ya kupata hizo donors parts pindi zitakapokuwa available. Utaratibu huu umeshaokoa maisha ya malaki ya watu duniani, hasa kwa wale wenye kuhitaji kuwekewa moyo au figo mpya.
Faida zake;
Licha ya kwamba huokoa maisha ya watu, pia hupunguza bajeti ya afya kwa taifa kiujumla, mind you kumng'oa figo mtu aliyehai ili akupe wewe moja na yeye abaki na moja ni suala gumu sana, nilisikiaga kuna mtu alikuwa anauza figo yake kwa 90M,sishangai hata kidogo!
You can imagine jinsi tunavyofukia mabilioni kila siku chini ya ardhi kwenye makaburi! Ila pia moyo wako unapofungwa kwenye kifua cha mtu mwingine ni kwamba wewe bado unaishi ndani yake, na unaweza hata kum-influence huyo recepient akawa na bakshishi kama zako wakati upo hai, hivyo na yeye akija kuugawa tena basi ni kama unaishi milele!
In anycase, spare parts za binadamu ni ghali.., na haziuzwi hovyo madukani, hivyo, ili kulinda figo na ini inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya pombe. Ili kulinda mapafu inabidi upunguze au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku na bangi, pia ili kulinda moyo jitahidi either kupunguza ulaji wa kitimoto usio na tija au ukishindwa fanya mazoezi asubuhi na jioni, ni muhimu sana.
Cha kushangaza, serikali hutumia pesa nyingi kutibu magonjwa yatokanayo na pombe na sigara kuliko kodi inayokusanya kutokana na sumu hizo, ni ajabu na kweli, hili liangaliwe upya.
DON FRANCIS
================================
Update: 15/03/2021
Wizara ya Afya yaandaa muswada wa kuvuna viungo vya watu, kama maini, figo, mapafu nk
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto imeanza kuandaa muswada wa sheria itakayosimamia uvunaji viungo vya binadamu zikiwemo figo, maini, moyo na mapafu ili vipandikizwe kwa wanaovihitaji. Ofisa katika kitengo cha magonjwa yasiyoambikiza katika Idara ya Tiba kwenye wizara...www.jamiiforums.com
=================================
Update: 28/04/2021
==========================Serikali yaandaa Mswada wa taratibu za uvunaji na upandikizaji viungo vya binadamu
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema kutokana na kuongezea kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo. Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji...www.jamiiforums.com
Update: 14/08/2024
Prof. Janabi: Chama cha Figo Tanzania kitawasilisha pendekezo la kuvuna Figo za Marehemu
Chama cha Figo nchini kimejiandaa kupeleka mapendekezo Serikalini kuanzisha uchukuaji wa Figo kwa marehemu, ili kuongeza idadi ya wapandikiziwaji kwani wengi wanashindwa kumudu kutokana na uchache wa watoaji figo hizo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili...www.jamiiforums.com