Jibu langu kwa Liverpool VPN na wenye shaka sa ndoa

Jibu langu kwa Liverpool VPN na wenye shaka sa ndoa

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Liverpool VPN ameanzisha uzi huu
Sasa mnaoa ili iwaje? Hebu angalia hii familia kimsingi ameonyesha kwamba kwa kuwatazama wenza aliowaelezea hakuna haja ya ndoa.

Anashare msimamo na watu wanaojitambulisha kama MGTOW (Men Going Their Own Way) kabla sijafika mbali nauliza hili swali "Mapenzi ni hisia au uchaguzi?"

Kuna nadharia moja inasema kwamba "Kinachosababisha umpende mtu ndicho hicho hicho kitasababisha muachane" yaani ni kwamba ule uzuri, utanashati unaomuona nao mwenza wako kuna siku utaona haukupi mshtuko kama wa zamani, shape yake utaona inakudistract na ucheshi wake utakua usumbufu.

Humu JF niliwahi andika kuhusu 'Sex rut' katika ndoa na hii nadharia inaashiria kwamba 'Sex rut' haikwepeki. Na mimi nakubaliana nayo kwamba 'sex rut' haikwepeki. Hivyo kila muunganiko wa wenza ni lazima upitie hapo.

Na kama kila muunganiko lazima upitie hapo narudia tena swali langu "Mapenzi ni hisia au uchaguzi?"

Wengi wetu Wazazi wetu wamekaa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 20 na kama tunakubaliana kwamba sex rut haikwepeki inamaanisha hata wao wameipitia. Kilichowafanya wabaki mpaka leo ni hisia au uchaguzi?

Liverpool VPN ndoa ambayo umeishuhudia ni ndoa ambayo hao wawili wanatarajia hisia zije kutatua migogoro iliyopo lakini kiukweli kinachohitajika ni wao kuchagua kama waendelee ama la. Nikiwa field Mbeya Bibi wa miaka 72 alileta kesi ofisini ili asuluhishwe na mumewe. Bibi wa miaka 72 anataka suluhu na mumewe, she chose kuendelea na mumewe.

So msimamo wako kwamba hakuna haja ya ndoa kwa kuutumia mfano wa rafiki yako ni sahihi? Hapana, hata kidogo. Kutumia ndoa za wachache ambao hawajaamua kustick na wenza wao na kupuuzia ndoa ambazo zina wenza ambao wamechagua kuendelea hata baada ya hizo roughs siyo fair.

Juzi juzi kuna member aliweka uzi kuuliza jinsi gani watu wanamove on kwa urahisi. Katika hii scenario ni kwamba a guy made a choice na chaguo likawa kuachana na mleta uzi, on the other hand mleta uzi bado ametawaliwa na hisia kiasi kwamba haoni kua mwenza wake tayari ameshachagua kumove on.

Kwa urahisi tunasema kwamba hisia zinatuingiza katika mahusiano ila kubaki na kuyaimarisha mahusiano ni uchaguzi. Rafiki yako na mkewe hawajachagua, wangechagua hata nafasi ya kuandika uzi ungekosa.

NB: Sex rut ni hali ya kutovutiwa kushiriki ngono na mwenza wako, spark mliyowahi kua nayo inakata na mnakua mnashiriki ngono kukamilisha ratiba. Hutokea kuanzia miaka 2 mpaka 5 ya kuishi pamoja.

Natumaini nimeeleweka kiasi chake.
 
Liverpool VPN ni mcheshi tu kama FUTUHI, rejea nyuzi zake…. nyingi ni kukandia ndoa wakati huo yeye mwenyewe ameoa.

It’s just a comedy genre of his choice.
 
Basi sawa.
Maoni yako juu ya anal sex yanaashiria you are open na unaweza jadiliana na mwenzi wako jambo lolote and kinky. Hiyo attitude nenda nayo kwenye ndoa mtapita katika phase ya sex rut easily.
 
In short,

Mapenzi ni feelings na emotions na ndoa ni commitments, ukiwa kwenye ndoa itafika muda hisia mapenzi zitakata, yani Mme au mke wako utamuona kama ndugu yako tu, ikifika hali iyo basi una baki na commitment ya ndoa

tatizo linakujaga wengi wana picture ndoa kwenye upande mmoja tu wa mahisia na mahaba niue, wanasahau kuwa committed na ndoa zao

samahan wadau, hivi kiswahil cha neno commitment ni nini? 😂😂😂
 
Dangote
Bill Gates
Jeff Bezos..
Ni sahihi? Kuwaweka hawa watu?

Dangote ameoa na kuacha mara mbili. Nafikiri yupo ndoa yake ya tatu.

Gates katoka kutalikiana na Bezos katoka kutalikiana.
 
Hayo ni mawazo yako ila nawajua watu Wana Mali, pesa na umri na wamegoma kuoa.

Role model wao ni DANGOTE..!!!

#YNWA
Mali kuwepo au kutokuwepo hakuhalalishi wala kubatilisha ndoa.

Dangote ameoa na kuachana mara mbili. Yupo ndoa ya tatu.
 
In short,

Mapenzi ni feelings na emotions na ndoa ni commitments, ukiwa kwenye ndoa itafika muda hisia mapenzi zitakata, yani Mme au mke wako utamuona kama ndugu yako tu, ikifika hali iyo basi una baki na commitment ya ndoa

tatizo linakujaga wengi wana picture ndoa kwenye upande mmoja tu wa mahisia na mahaba niue, wanasahau kuwa committed na ndoa zao

samahan wadau, hivi kiswahil cha neno commitment ni nini? 😂😂😂
Ndani ya ndoa muda unafika hata mwenza akisafiri unasema afadhali nipumzike hizi kero za kujilazimisha unatamani hata amalize mwezi ndo arudi labda utakuwa umepata hisia....ila wazo la kuachana halipo na hapo unawaza Mungu awajalie mtoto mwingine 😂😂😂😂😂
 
Hayo ni mawazo yako ila nawajua watu Wana Mali, pesa na umri na wamegoma kuoa.

Role model wao ni DANGOTE..!!!

#YNWA
Dangote hajawai kuoa? Ni ndoa zinamsumbua ila anaoa yule...kina bill gate mwenyewe alioa, Bezos alioa, trump mwenyewe alioa
 
Ndani ya ndoa muda unafika hata mwenza akisafiri unasema afadhali nipumzike hizi kero za kujilazimisha unatamani hata amalize mwezi ndo arudi labda utakuwa umepata hisia....ila wazo la kuachana halipo na hapo unawaza Mungu awajalie mtoto mwingine 😂😂😂😂😂
Enhe. Endelea na dondoo
 
Back
Top Bottom