Jicho la kisheria kuhusu uhalali wa barua ya Spika Ndugai kujiuzulu

Nashauri serikali isije kukosea ikamlipa mafao ya u-spika.
Huyu mtu ameondoka kwa kashfa na hajamaliza muda wake!
Tusitumie vby fedha za walipa kodi jamani, ale vihela vya ubunge vinamtosha!
Siyo kwa ccm ndugu. CCM ni kama ukoo wa panya. Lowasa alijuzulu lkn bado analipwa marupurupu yote Kama mstaafu ikiwemo pension ambayo ukubwa wake ni 80% ya mshahara wa Majaliwa (pm wa Sasa). Why not Ndugai?
 
Wananchi wepi hao? Labda mazuzu kama wewe.

Spika pekee aliyejijengea heshima kwa wananchi ni Samuel Sitta peke yake na akaja kujivunjia heshima mwenyewe kwenye bunge la katiba kwa tamaa ya Urais.
 
Kuna siku tutaskia Mnyika kapokea Barua ya kujiuzulu Uenyekiti wa Taifa Bw. FREEMAN
Sawa,ila hiyo haiondoi ukweli kwamba kajiuzuru pamoja na hizo proceedings,labda aikane barua yake mwenyewe,kwamba si yeye aliyeiandika
 
Yawezekana kuwa barua Ile hakuiandika yeye na Wala haikuchapwa kwenye ofisi yake na secretary wake Kwa jinsi ilivyopangiliwa pamoja na kutumia herufi kubwa kwenye barua yote!
Yawezekana mwandishi siyo secretary wake na au imechapwa na tiss Kisha yeye kulazimishwa kuweka sahihi yake!
Aje hadharani aikatae au kuikubali barua Ile na aseme kwanini hakuizingatia katiba na kanuni za bunge ambazo kashiriki kuzitunga na kuwapa kuzisimamia!
Kwa mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndiye mshauri wa rais kwenye masuala ya sheria anatakiwa amweleweshe rais kasoro zilizopo kwenye barua hiyo na ilibidi rais aikatae ili ikaandikwe upya na ama sheria na kanuni za bunge zizingatiwe ili kuepusha mgogoro wa kikatiba ambao upo wazi Kwa Sasa!
Haya ni mashaka na mtazamo wangu japo wasio na uelewa wa makosa hayo watanichana kimhemko!
 
Kutokana na Barua ya kujiuzulu kwa Spika kuelekezwa kwa katibu mkuu wa chama ambapo ni kinyume cha katiba iliyompa mamlaka, ambapo angepaswa kuiwasilisha bungeni ni wazi kwamba hizo ni dharau!
Ndungai ni kama alikuwa amekwiamini pengine yeye bunge ni la kwake na kwamba pengine lisingeweza kutokea lolote la kumwajibisha!
Ndungai kwa maneno yake mengine bungeni ambayo alikuwa akiyatamka kibabe, na wakati mwingine kutumia ubabe kufanya yale aliyokuwa akifanya, alidhani boss wake ni mmoja tu na kikatiba hakuna popote anabowajibika!
Haiwezekani kwa spika ambaye alianza kuwa naibu spika kisha spika kamili ambapo amesimamia mengi bungeni kwa kuzingatia kanuni za bunge na katiba halafu akafanya alichofanya!
Hiki alichofanya si kwa bahati mbaya bali ni dharau kwa katibu mkuu ambaye ni mwanamama!
Kwa hili alilolifanya ahojiwe na achukuliwe hatua stahiki kwa dharau zake!
 
Wananchi wepi hao? Labda mazuzu kama wewe.

Spika pekee aliyejijengea heshima kwa wananchi ni Samuel Sitta peke yake na akaja kujivunjia heshima mwenyewe kwenye bunge la katiba kwa tamaa ya Urais.
Hata huyo six hovyo tu. Na hata kama angekuwa mzur bado uzur wake hauwez kuonekana ndani ya katiba iliyopo sababu katiba hii inalifanya bunge kama nyumba ndogo ya executive. Ndugai yeye alienda mbali zaid, hakuna nyumba ndogo tu bali alijigeuza kabisa house boy wa banda la ng'ombe huko chatrou
 
Mm binafsi naona tatizo co ktb au sheria tatizo ni utashi wa viongozi mf ktb iliyopo ni mara ngapi tunaona viongozi wakiivunja?hatua8 zipi zimechukuliwa au nani kakemee bussines as usual wt wanaapa kuilinda na kuitetea ktb lakini hao hao ndio wanaivunja na sheria zo wazi ukivunja ktb unatakiwa ufukuzwe kazi lakini nani kafukuzwa sbb hakuna anayejali hivyo ata tukiwa na ktb mpya nani atailinda na kuitetea jama viongoz ni walewale wasiokuwa na utashi wananchi tunatakiwa tuwe watetezi tukiona kuingoz anavunja jtb tuseme no
 
Nchi ya hovyo sana hii... halafu Chongolo kwa umbumbumbu wake akaaja front kusema kapokea barua ambayo haikufuata utaratibu. Huenda hii barua imeandikwa na maccm yenyewe ili kumfurahisha mwenyekiti.
Yote heri....
 
Ndugu zangu watanzania mnafahamu fika nchi yetu si yenye kufuata misingi ya sheria na utaratibu, hata issue ya Job kuhoji, katiba inamruhusu ila kwa sababu nchi yenyewe haina mwenye kauli ya mwisho ndiyo basi tena.

Angalau Mkapa au late faza of nation angekuwepo tungepata last say now kila mtu anapiga ngoma anavyoweza na mwenye ngoma iko na sauti kubwa huyo ndiye wachezaji wanakata viuono kwa juhudi.
 
Tuna mkuu wa nchi ambaye ndiye mkuu wa mihimili yote. Ndungai kwa bahati mbaya au kwa kukusudia alimkwaza sana mkuu wa nchi kwa kumbeza kukopakopa. Mkuu wa nchi kakasirika sana na hata baada ya kuombwa msamaha na huyo Ndungai, mkuu wa nchi alikataa kumsamehe.

Kwa hali kama hiyo the best logical option ilikuwa ni Ndungai kumwaandikia (direct) barua ya siri mkuu huyo wa nchi aliyemkwaza kumjulisha uamuzi wake huo wa kukaa pembeni (kujiuzuru) ili kazi iendelee bila vikwazo na kumuahidi atakuwa raia mwema na mtiifu kwa nchi yake. Mkuu wa nchi baada ya kupokea barua hiyo na kuridhia, ndiye angalizielekeza mamlaka husika kufanya mchakato wa kupata spika mwingine.

Haya mambo ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kutoa TAARIFA KWA UMMA hayafai. Hata huo msamaha aliomuomba mkuu wa nchi kwa kupitia vyombo vya habari, ni utaratibu mbaya. Kwa nini hakumuandikia mkuu wa nchi moja kwa moja na/ au kuonana naye moja kwa moja? Siku ya kutathimini matumizi ya huo mkopo wa 1.3 trillion ilikuwa mhimu kwake ku lobby kuhudhuria kikao hicho na kupewa fursa ya kuweka mambo sawa na kuomba msamaha kwa kutoeleweka vizuri.

Kama ulivyosema katiba na kanuni za bunge hazitoi maelekezo ya namna spika anavyoweza kujiuzuru katika mazingira ya aina hii yaliyomkuta Job Ndungai. Katiba na kanuni za bunge zinaelekeza tu namna ya kupata spika mwingine mara kiti hicho kinapokuwa wazi.
 
Ni kweli kabisa Katiba inaelekeza kama Spika atajiuzulu,ataandika barua kwenda Bunge ( Katibu wa bunge) kitendo cha Katibu kupewa Nakala siyo Sahihi, hivyo Ndugai anapaswa kuandika barua kwenda kwa Katibu wa Bunge kama Mtendaji.
 
Nchi ya hovyo sana hii... halafu Chongolo kwa umbumbumbu wake akaaja front kusema kapokea barua ambayo haikufuata utaratibu. Huenda hii barua imeandikwa na maccm yenyewe ili kumfurahisha mwenyekiti.
Chongolo ni punguani flani hivi. Ndio maana hata Badjita alikuwa anayaburuza
 

Majivuno ndio yamemuangusha. Huwezi kusema " mama yenu juzi hapa kaenda kukopa" wakati huo mkopo ulipitia kwenye kamati ya bunge. Ndugai anatafuta maslahi ya kisiasa Kama angekuwa mkweli asingekubali pesa za walipa Kodi ziwalipe wabunge wasiokuwa na sifa.
 

Pole Sana Tanzania hakuna utawala wa sheria. ndio maana leo tunatoza wananchi na kukopa nje ili tuwalipe wabunge 19 wasiokuwa na sifa kikatiba.
 
Watanzania na dunia mzima inajua kwamba Ndugai kajiuzulu uspika. Hiyo ndo fact. We ukatae ni shauri yako na hakuna kitacho badilika. Huo ndo ukweli. Lakini kama ni school/academic discussion haya!
Ok uko vizuri.lakni kumbuka katika sakata la matibabu ya Lissu .ndugai alisema ofs yake haijui kuwa Lissu Yuko wapi na anafanya Nini wakati dunia mzima
inajua yalo mpata Lissu
 
Kwa mtazamo wangu mimi, nadhani kuna scenario kadhaa za kuzingatia;

1. Kwanza lazima tuelewe pia kuwa, jambo hili pamoja na kuwa ni la kisheria na kikatiba, lakini pia ni la KISIASA, kwamba, ndani yake kunachezwa gemu ya kisiasa kupumbaza umma...

2. Spika Ndugai na administration ya Bunge kwa ujumla si wajinga wa taratibu za kisheria na kikatiba kiasi hicho hata hata washindwe kuona njia sahihi ya kujiuzulu Spika..

3. Kuna possibility kubwa barua iliyokwenda kwa KM wa CCM ni nyingine (ndiyo tunayopumbazwa nayo) na wakati huohuo Katibu wa Binge naye akiwa amepata barua iliyofuata utaratibu halali wa kisheria na kikatiba kujiuzulu kwake...

4. Kumbeni kuwa, CCM ni watu wajanja na wanajua sana kucheza michezo ya kisiasa. Yote hii ni katika ku - minimize political damage ya chama chao...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…