Shakira M. Selemani
Member
- Nov 7, 2019
- 38
- 77
JICHO LA TATU _ KILA KITU UNACHO PASWA KUJUA.
👉Kwa karne nyingi watu wamekuwa wakizungumza kuhusu Jicho la Tatu. Baadhi ya watu hulitafuta jicho la tatu kama nyenzo au njia ya kuwasiliana na viumbe wa ulimwengu mwingine wasioonekana, wengine huliona jicho hilo kama chombo cha kuwasaidia kutabiri mambo yajayo, na wengine hulichukulia kama "nguvu maalumu" inayo weza kufunua mambo yajayo..
👉Hatahivyo, habari nyingi zinazo sambaa hivi leo kuhusu jicho la tatu , nyingi kati ya hizo ni mchanganyiko wa nusu-ukweli, imani na mifumo ya zamani ambayo badala ya kusaidia kufungua jicho la tatu inaweza kulifunga zaidi.
JICHO LA TATU NI NINI HASA?.
👉Jicho la Tatu sio mpira wa kichawi ulio wekwa kichwani kwako kwamba unaweza "kuuwasha" tu kimchezo mchezo. Sio uganga wa jdi wala sio ushirikina.
👉Katika mafundisho ya siri ya kiroho, Jicho la tatu ni uwezo wa asili wa utambuzi unao unganisha Mwili wa kifizikia na viwango vya ndani zaidi vya uhalisia visivyo onekana kwa urahisi.
Katika zile hisia tano au milango mitano yafahamu kama vile Kunusa, kusikia, kuhisi, kuona na kuonja...basi Jicho la Tatu ni sehemu ya hisia nyingine ya Sita ...six sense..ni hisia isiyo hisi mwili bali yale yasiyoonekana ni hisia iliyopo ndani yetu na si uchawi.
👉Kimaumbile ama kibaiolojia, Mara nyingi Jicho la Tatu linahusishwa na Tezi ya Penueli (Pineal Gland) iliyopo ndani yetu kwenye ubongo ni tezi halisi kama vile Kongosho, Pituitary n.k Tezi hii ya Penueli ipo eneo la katikati ya nyusi zako na linahusishwa na Kituo cha sita cha Ufahamu yaani AJNA CHAKRA.
👉Hata hivyo, Jicho la Tatu si Tezi penueli pekeake. Ni uwanja mzima wa Ufahamu unao mwezesha mtu kutambua mambo yanayopita hisia tano/milamgo mitano ya fahamu za kawaida --- kama vile Nguvu, mifumo, mahusiano, bishara, nia za kweli, kumbukumbu za yaliyo pita, maono,na zaidi ya yote kutambua kwa ushahidi kupitia wewe mwenyewe uwepo wa Chanzo (Source).
👉Jicho la Tatu linapokuwa Safi na Hai, mtu hudaiwa kuwa na Uwezo wa:
•Kuona na kuhisi ukweli ulio nyuma ya maneno:
•Kutambua hali au nguvu za watu na maeneo;
•Kupata picha na maarifa ya ndani bila kulazimika kuyatafuta yaani bila kusoma popote.
•Kuwasiliana na vipengele vya juu zaidi vya nafsi yako na pia utaweza kuwasiliana na viumbe wengine bila upotoshaji...hakuna kiumbe wa uongo atae weza kukudanganya bila kutambua kuwa anafanya uhuni au anakuingiza mtegoni ...utakuwa makini AWARE bila kutumia nguvu.
YANAYO SEMWA KUHUSU JICHO LA TATU ___ NA YASIYO YA KWELI.
IMANI YA KWANZA ILIYO SAMBAA INASEMA "Jicho La Tatu likisha funguka Halifungiki tena"
UKWELI: Kwa mujibu wa mtazamo huu wa kiroho, inaelezwa kwamba; Jicho la tatu linaweza kufunguka na kufunga kulingana na hali ya kiroho na kisaikolojia ambayo mtu anaishi ndani yake..
Linaweza kuanza kufunguka kidogo, na kisha kuongezeka kuwa hai kwa kiwango kikubwa zaidi, au kudhoofika tena ama kufunga tena pale mtu anapo rudi tena katika hali na mifumo ya hofu, hatia au udhibiti.
👉IMANI YA PILI: "Meditate tu kwa kuweka mkazo kwenye jicho la tatu - paji la uso na kila kitu kitafunguka"
UKWELI: Kwa kuzingatia pekeake eneo lililopo katikati ya nyusi wakati wa meditation mara nyingi kunaweza kuchochea picha za akilini na mawazo ya kubuni. Bila kutuliza nafsi na kuunganisha utambuzi huo na moyo, mtu anaweza kuchanganya mawazo na fikra zake na kile anacho dhani ni Jicho la kweli...kwamba utakuwa ukipata tu mawazo ya kubuni yakufikilika badala ya utambuzi wa kweli wa Jicho la Tatu.
👉IMANI YA TATU: "Jicho lako la Tatu likifunguka utaiona mizimu, na viumbe wa nje ya Dunia (ETs) pamoja na kuona mambo yajayo ya baadaye"
UKWELI: Kwa mujibu wa mafundisho ya kiroho inaelezwa kwamba; Jicho la tatu kwanza humwelekeza mtu kwenye ukweli kuhusu nafsi yake mwenyewe na maisha anayo ishi ama uhalisia anao ishi. Mtu huanza kutambua udanganyifu, ushawishi na mifumo yake ya ndani isiyoonekana.
Na vipengele vingine huja ama hutokea baadaye..kwanza ni nafsi yako.
ZINGATIA: Ikiwa mtu ataanza kuona mara moja mambo ya ajabu ajabu bila kujitambua yeye mwenyewe (haoni chochote kuhusu yeye mwenyewe), Hayo ni mawazo ya kubuni au tafsiri zisizo sahihi (potofu) badala ya utambuzi wa kweli wa ndani.
👉IMANI YA NNE: "Jicho La Tatu ni Hatari na linaweza kukuangamiza"
UKWELI: Jicho la Tatu halionekani kuwa ni hatari ikiwa utazingatia mtazamo wa kiroho:
Kinacho weza kuwa tatizo ni mtu kujaribu kufungua uwezo huo wa kiroho bila utulivu wa ndani na wa kisaikolojia, bila kujikita katika uhalisia wa maisha na bila msingi thabiti wa kiroho ...uwezo wa kutofautisha Hisia, mawazo na ukweli.
KWANINI WATU WENGI HAWAWEZI KULITUMIA?
ZIFUATAZO NI SABABU ZINAZO FANYA WENGI WASHINDWE KULITUMIA JICHO LA TATU NI;
➖Uzito wa Hali Ya Ndani: Hofu, hatia, kujikosoa kupita kiasi, kujilaumu na mawazo yanayo jirudia vinaweza kuzuia utulivu wa akili..vinaweza kuathiri uwezo wa mtu wa kutulia na kutambua mambo kwa uwazi.
➖Kutengana na Moyo au Kutenganisha Akili na moyo: Jicho la Tatu likitumiwa bila uwiano wa hisia na huruma kwamba utambuzi wa akili bila huruma na hekima unaweza kuwa wa baridi, na uchambuzi kupita kiasi au kutawaliwa na nafsi ya chini yaani Ego.
➖Imani potofu ya kuamini kwamba "Hupaswi kuona ..huruhusiwi kuona" : Baadhi ya watu hubeba imani za zamani zinazowafanya wajizuie kuchunguza kikamilifu ulimwengu wao wa ndani...imani zinazo wafanya waamini kwamba hawapaswi kutambua au kuelewa mambo fulani kikamilifu. Imani hizo zinaweza kuachwa.
➖Msongamano wa Taarifa - Taarifa nyingi kupita kiasi: Utambuzi wa ndani unapoongezeka bila mtu kuwa na utulivu wa kutosha, anaweza kupata hofu au kuchanganyikiwa.
➖Kutafuta Uzoefu wa Nje badala ya Ukweli wa ndani: Watu wengi wanapo fungua jicho la tatu hutaka kuona "Nuru au viumbe wa nje" lakini hawako tayari kujitazama na kujichunguza wao wenyewe kwa uaminifu.
JINSI YA KULIFUNGUA JICHO LA TATU KWA MUJIBU WA MAFUNDISHO YA KIROHO.
Si kwa kutumia nguvu si kwa kulazimisha. Wala si kwa kutumia mbinu au njia zinazo lazimisha kufunguka...njia zinazo lazimisha uzoefu fulani kutokea.
1. ANZA NA MOYO:
👉Kila siku pumua kwa utulivu huku ukielekeza umakini kwenye eneo la moyo. Fikiria nuru ya dhahabu ikienea taratibu kupitia mwili mzima.
Kwa mujibu wa mafundisho ya kiroho, Jicho la Tatu hufunguka kwa uwazi zaidi pale moyo unapokuwa na utulivu..umetulia na kuna uwiano.
2.USAFI WA MAISHA YA NDANI - SAFISHA HALI YAKO YA NDANI.
👉Acha kuulisha moyo wako na akili yako kwa hofu, umbea, malalamiko yasiyo isha na mawazo yanayo jirudia bila sababu bila kukoma.
Katika lugha ya alama, mambo hayo ni kama "Moshi mzito unao funika Jicho la Tatu"
Epuka hizo hofu, umbea, kulalamika na Stress
3. TAMBUA BILA KULAZIMISHA.
Badala ya kusema "Nataka kuona"
wewe sema "Niko tayari kutambua Ukweli"
Kisha tulia na tazama kwa utulivu kile kinacho jitokeza...hisia, picha za akilini au maarifa ya ndani...bila kulazimisha tafsiri zake.
4. TUMIA PUMZI NA TASWIRA YA NURU (PUMZI NA NURU)
👉Pumua kwa upole taratibu huku ukielekeza umakini wako kwenye eneo lililopo katikati ya nyusi na kwa wakati huohuo kwenye moyo. Fikiria vuta picha maeneo hayo mawili yakiunganishwa kwa daraja la dhahabu.
Usilazimishe, ruhusu hali hiyo itokee kwa utulivu.
5. ISHI KWA ULINGANIFU NA UKWELI WAKO.
👉Jicho la Tatu lenye nguvu zaidi, linahusishwa na mtu anaye ishi kwa kufuata kile anacho kiona kuwa ni kweli.
Kujifanya (kuishi kwa maigizo), uongo na kujidanganya mwenyewe kuna weza kuzuia utambuzi huo wa ndani.
UTAJUAJE KUWA UMEUNGANISHWA?.
👉Kwa mujibu wa mafundisho ya kiroho, kama umesha unganishwa Unaweza kuanza:
•Kuhisi hali au nguvu ya mtu kabla hajazungumza.
•Kutambua mtu kama anasema ukweli au la bila kufanya uchambuzi mrefu...utaanza kutambua tofauti kati ya ukweli na uongo bila kuchambua kila kitu kupita kiasi.
•Utaanza kupata picha au maarifa ya ndani ambayo baadaye yanaonekana kuwa sahihi
•Utaanza kuwa na dira imara ya ndani inayo kusaidia kujua mahali pa kwenda na mahali pa kuepuka.
•Utaanza kutambua unapokuwa katika hali nzuri ya ndani na unapokuwa umevurugika.
•Utaanza kutohitaji uthibitisho wa nje kila wakati.
•Utaanza kupata hali ya amani hata pale ambapo hujui kitakacho tokea baadaye.
👉Hata hivyo, dalili kama vile maumivu makali ya kichwa, shinikizo kwenye paji la uso, wasiwasi au mkanganyiko wa mawazo si ushahidi wa kweli kwamba Jicho la tatu linafunguka. Dalili kama hizo zinaweza kuwa na sababu nyingine za kimwili au kisaikolojia na zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito.
NI NINI AMBACHO SI JICHO LA TATU?
👉Jicho la Tatu sio chombo cha kuwadhibiti wengine.
👉Jicho la Tatu sio njia ya kuikimbia dunia au kuyakimbia maisha (Halikuletei pesa wala nini ...pesa fanya kazi utapata Jicho la tatu halitajirishi ni upotofu)
👉Jicho la Tatu sio Udhibitisho kwamba wewe ni "Wa juu" umetaalamika kuliko watu wengine.
Kwa mujibu wa mafundisho ya kiroho..Jicho La Tatu ni "Uwezo wa asili wa fahamu unao mrudisha mwanadamu kwenye utambuzi mpana zaidi wa nafsi yake na maisha"
Ni uwezo unao mrudisha kiumbe kutoka kwenye chanzo kurudi katika hali ya utambuzi kamili.
HITIMISHO
👉Jicho la Tatu halifunguki ili uone miujiza.
Linafunguka ili uweze kuona Ukweli.
👉Na unapo anza kuona Ukweli....kuhusu wewe mwenyewe, kuhusu Ulimwengu, kuhusu Nafsi yako, Kuhusu kile kilicho halisi na kile ambacho ni mfumo wa mawazo ulio pandikizwa tangu unazaliwa (programu)....mambo mengine yoote huanza kujitokeza yenyewe na kujipanga yenyewe.
Jicho la Tatu si Lengo. Ni kurudi kwenye Nafsi yako...ni kurudi kwenye hali yako ya Asili.
⚠️Kwahiyo wale wanao sema "Nguvu ya Jicho la Tatu na Pesa" ni waongo wakubwa, wanatumia dhana ambazo watu hawazijui vizuri hawazielewi kulaghai wengine ...wao wamefanya mikataba ya kichawi ili kupiga pesa kupitia ujinga wenu na Maapizo ya kichawi kujitajirisha binafsi..... MIAKA YA MBELENI WATAUMBUKA NA MTAUKUMBUKA UJUMBE HUU
KWA UPENDO NAKUWASILISHIENI UKWELI HUU.