Uchaguzi 2020 Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...


Mbona mnapata tabu sana, mchakato wa kupata mgombea ni jukumu lao Chadema wenyewe na kinachofanyika ni mipango mkakati ya Chama sasa hizi kelele za nini? Kama wasingeweka mgombea mngesema wanatia mpira kwapani, hivi mnajua nani atapitishwa kugombea? Ya ngoswe muachieni ngoswe mwenyewe? Mbona wao hawawasemi nyie kuminya Demokrasia kwa kotoa form moja tu ya mgombea Urais?
 
Mbowe hachafuliwi bila kujichafua mwenyewe. Muwache kuvaa miwani za jua usiku, na muache kutembea mchana huku mumefumba macho.

Chadema kina viongozi wengi wazuri, chadema sio mbowe pekee, wacheni kujiambukiza maradhi ya upendeleo, alafu mnawasingizia watu, kuwa wanamifitini.

Hebu fuatili historia ya siasa zaa Mbowe ndani ya chadema , kuanzia enzi za Chacha wangwe, Zitto, Slaa, Lowassa, Sumaye, na sasa Lissu.
 
usalama wa taifa anavunjwa mguu na akina musukuma na lijua likali????hebu fikiria tena uje!!!!
 
Ishu ya Chacha Wangwe mnavoiimba kama ni kweli Mbowe huyu angeshafungwa kifungo cha maisha au kunyongwa kabisa.

CCM kupitia 'manyigu' ndiyo walimchochea Chacha na yeye bila kujua kuwa anatumika akajaa na ugomvi ulipofikia kwenye kilele wakafanya yao wakijua jumba bovu litaiangukia Chadema.

Kama kawaida yenu haraka haraka mkaandaa statement na kuwapa wapambe waisambaze kumhusisha Mbowe na Chadema juu ya kifo cha Chacha, lakini Watanzania siyo wajinga na kilichotokea kule Tarime kila mtu anajua mlivuna aibu na Kaka yako Makamba Snr akaondoka Tarime usi usiku. Wacheni siasa za kishamba za maji taka na kutegemea dola kuwafanyia siasa.
 
Mayalla unaenda kuaibika kuhusu issue ya Lissu. Wagombea Wabash in danishes ndani ya chama tena kwa namna ya kipekee kupata kutokea Tanzania. Kuna mdahalo wa ndani utafanyika na Presidential material ataonekana dunia nzima sio kwa wanachadema pekee, atapita.

Je, akionekana baada ya mdahalo anayefaa mfano ni Msigwa na akapitishwa na Mbowe akajitokeza kuwa anaheshimu maamuzi nani mwingine kati ya watai nia anaweza kulalamika? Hakuna.

Na unadhani baada ya mdahalo huo Watanzania wangapi wanaweza kuona na kutambua ubora wa mgombea wa Chadema? Maana mdahalo sio kupiga pushups au kuruka mapanga shaa!
 
Nimekuelewa kwenye para ya kwanza tu, jamaa ana mabandiko mengi humu mpaka yameanza kuboa, anakosa muda wa kutulia aandike kitu kinachoeleweka, ni kama vile analipwa kwa kupandisha uzi humu every hour, who knows!. Alishaonesha hampendi Mbowe toka wakati ule wa uchaguzi ndani ya chama, akapandisha uzi wake wa kipuuzi kutaka wapiga kura wasimchague Mbowe, akashindwa.

The rest kuhusu Chadema na Mbowe umeandika pumba, kama unaamini Chadema inaenda kupoteza nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani ungesema sababu sio kuimba tu, na wewe unajua, Chadema inalazimishwa kupotezwa but miongoni mwa watanzania bado ni favourite political party, hivyo hizi ndoto zenu mnajifurahisha tu.

Kuhusu Mbowe pia umeandika pumba, huwa anachaguliwa kwenye vikao halali kwa kupigiwa kura na walio wengi, hizi kelele zenu za dikteta sasa zinaonekana ni utoto tu.
 
Ugonjwa wako ni mdogo sana.

Unataka Mbowe asijitokeze kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi wa chama chake, wacha ushamba, hao unaowaita wagombea wazuri wajitokeze kushindana nae, usilete mawazo ya kitoto hapa.

Mbowe ana haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama chake na kama wapiga kura wanamkubali wataendelea kumchagua, una akili finyu sana, unataka asigombee ili hao uliowataja wapite bila ushindani ili wajinga nyie mfurahi!.

Una hoja za kitoto sana.
 
Siku hizi ong'wise unanipa raha sana unavyoweka kinga! Unajua tu raia lazima wakupopoe ndiyo maana unatanguliza ngao ya mawe kama ukuta wa Berlin! Jichunguze na ujirekebishe tu mkuu!
 
Kwani Dr slaa wakati anagombea 2010 alikua ni tajiri? Chadema ni watu wa tafiti katika kuwapata wagombea na ndo maana kila wakati kimekua kikiongezea madiwani na wabunge
 
Aisee kweli chadema Ni CHADOMO yaani chama Cha DOMOCRASIA yaani Raisi Bora anapatikana kwa namna anavyochonga mdomo kwenye mdahalo.

Mchonga mdomo Sana ndio anapewa ugombea uraisi chadema .Aiseee very sad.Kuna vigezo vizito vya kumpima mgombea uraisi hicho Cha domokaya hakimo kwa Chadema mfano Ni uwezo dhibitika binafsi wa kifedha au wa wafadhili wenye track record pia uwezo wa eneo la ubunge ulilokuwa nalo ulilifanyia nini? hapo watu Kama Mbowe Hai kaitendea haki kupeleleka maendeleo,Msigwa pia Jimbo la Iringa kafanya vizuri mno , Nyalandu pia kafanya vizuri alipkuwa Mbunge.

Lisu kwenye hiki kipengele anatolewa knock out hata na Msigwa.Kama akishindwa kuhudumia eneo bunge lake tu kuliletea maendeleo uraisi wa kuhudumia nchi nzima hawezi .Hao watatu Mbowe, Nyalandu na Msigwa waweza graduate kwenda next level sababu kwenye eneo bunge lao wamefanya vizuri

Lisu Ni mpiga Domo tu ndio maana anataka mdahalo sababu he has nothing to show kwenye jimbo lake!!! Anataka tu kuongea Kama kameza album

Raisi anayetafutwa ni mjenga Jimbo lake na mjenga nchi sio mjenga hoja .Wajenga majimbo ndio wagombee.

Hakuna haja ya mdahalo wa kubishana maneno ya kingereza kuonyesha Nani anajua kingereza kuliko mwingine maisha sio mdahalo ni vitu real !!! jimboni umefanya nini Hadi utake uraisi?

Chadema msiendekeze vitu vya kitoto kama midahalo kwenye uteuzi wa mgombea uraisi.Uraisi Ni serious issue is more than a secondary school debate
 
Lumumba magufuri inaonekana atachukua fomu tena ndani ya ccm, swali ni je, Kuna ruhusa na mwingine kuchukua fomu ya urais ili kumshindanisha na magufuri? ccm hiyo kwenu mko tayari??
 
Mtani rudi darasani kidooogo hapo kwenye mgombea mwenza wa Mbowe kuwa Mayrose umechapia, mgombea mwenza lazima atoke upande wa pili wa Muungano.
 
Kwani Dr slaa wakati anagombea 2010 alikua ni tajiri? Chadema ni watu wa tafiti katika kuwapata wagombea na ndo maana kila wakati kimekua kikiongezea madiwani na wabunge
Wafadhili wa nje wa chadema Dr slaa ndie alikuwa mtafutaji mkubwa .Na alikuwa ndie contact person wa wafadhili wa chadema was nje ya Nchi.Ndio maana uliona akizinguka ulaya na Marekani akipokelewa Kama Raisi kwenye Kila eneo aliloenda kutembelea ulaya marekani kwa donors. Wafadhili wa nje ndio kuliwafanya chadema wampe ugombea uraisi kwani wafadhili wake walikisaidia Sana Chadema kifedha ,semina,nk .Kipindi chake viongozi Chadema walikuwa kutwa ulaya na Marekani kwa gharama za wafadhili wa Slaa ambao wengi alifahamiana nao akiwa katibu was Baraza la maaskofu Tanzania

Slaa kuwekwa ugombea uraisi ilikuwa Asante kwake kwa mchango mkubwa wa pesa za kigeni kwa Chadema toka kwa wafadhili wake..Tundu lisu je? Anategemea tu kuchonga mdomo!!! Kampeni zinahitaji pesa sio kupepeta mdomo!!!

Yes utafiti ulifanyika kuwa Nani apewe ugombea uraisi mwenye pesa zenye ushahidi kuwa zipo Dr Slaa akapewa na wafadhili hawakumwangusha walimpa pesa za kampeni sema tatizo tu kura haziikuenea .Lakini hakuwa na shida ya pesa zilikuwa pesa za wafadhili zinatiririka Kuingia akaunti za Chadema kabla ya kugombea na ziliendelea kutiririka alipogombea

Swali wafadhili wa Tundu Lisu wanatiririsha pesa akaunti za Chadema jibi Ni la .Hana hata alizotoa tangazo kuwa achangiwe anataka ziende kwenye namba za simu za mtu binafsi.Ni mtangaza Nia pekee ambaye pesa Hana keshaanza kusumbua watu wamchangie yeye binafsi badala ya chama hata kabla uteuzi haujafanyika!!!

Wenzie pesa wanazo Nyalandu kurusha helikopta angani nchi nzimai kwenye kampeni kwake Ni kitu kidogo Sana ,Mbowe ndio usiseme

Hao malofa wawili Msigwa na Lisu Ni mizigo ya gunia la misumari kwa Chadema na wanachadema kwenye kampeni .Ulofa mwingi na chadema pesa hakina anatakiwa mgombea anayejibeba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…