Jicho langu Kuu la 'Kiuchambuzi' na 'Kimtazamo: juu ya 'Mabadiliko' ya Saa 24 tu zilizopita

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
1. Ni mabadiliko ya kuonyesha kumbe kulikuwa hakuna kabisa Maelewano kati ya aliyelala mazima na aliye Hai akiendelea na Kazi, bali ni Unafiki mtupu ndiyo ulikuwa Umeshamiri japo kuna Mtu kila katika Hafla alikuwa akionekana Kutabasamu na hata Kutuhutubia Watu kwa Kuunga mkono harakati zote za Kiutendaji za kuanzia 2015 mpakae tarehe 17 Machi, 2021.

2. Ni mabadiliko ya Kufyagia mazalia yote ya aliyelala mazima ili aliye Hai aweke anaowaamini na watakaomsujudia pia.

3. Ni mabadiliko ya Kimkakati hasa kwa Kumteua tena Mtu ambaye aliondoshwa mahala fulani mpaka Kutishiwa Bastola kwa Tukio baya la 'Gaidi na Fisadi Matege' mahala fulani Mikocheni hivyo amerudishwa hapo ili Kesi ya Tukio hilo sasa irejewe upya na hatimaye Mhusika akamatwe ili Chanzo cha Mashitaka mengine makubwa yanayomkabili kipatikane na hatimaye nae mwaka huu 2022 akione cha Moto ( Mtema Kuni ) kama alichokiona Mwenzake wa Hai Mkoani Kilimanjaro.

4. Ni mabadiliko ya Kuwafyagia waliokuwa Wanafiki wa Kipindi cha aliyelala mazima na Kuwakaribisha wapenda Uhalisia ila wasiopenda Kukosolewa wa aliyeko.

5. Ni mabadiliko ya Kuwathibitishia Watu kuwa kuishi Magogoni au Chamwino au Zanzibar hakuangalii sana Jinsia ya Mtu bali ni Kujiamini, Uwezo na kuwa Mwanadiplomasia mwenye Ubabe Moyoni kama si Rohoni.

6. Ni mabadiliko ya muendelezo wa Utamaduni wa Kiafrika kuwa Kipaumbele Kikuu ni Kuunda Safu yako ( Genge lako ) ili ule vyema na kwa Kujiamini kabisa Rasilimali Keki zilizopo kwa 95% na matatizo ( mahitaji ) ya Watu uyakabili kwa 5% tu ukiamini kuwa wanaokuja nao watayatatua.

7. Ni mabadiliko hasa ya Kutuonyesha wenye Akili Kubwa kuliko Wao kuwa si kweli kuwa kuna Watu wanakitaka Kiti cha Ufalme kama tulivyodanganywa kama si Kuaminishwa hapa Juzi kati Mkutanoni bali Lengo Kuu ni Kuua Makundi ( Magenge ) hasa Kuelekea Chaguzi ndani ya Nyumba Kuu ya Kitawala ( Kisiasa ) mwaka huu na kwamba japo Zanzibar inatuongoza Machoni mwetu ila uhalisia ni kwamba Pwani ( Bagamoyo na Chalinze ) ndiyo Usukani Kamili wa Tanzania kuanzia Machi 2021 mpaka 2025 na huenda hata 2025 hadi 2030.

Hongereni na Poleni kwa Mabadiliko.
 
Mimi nathibitisha kwamba jk hakuwaga na mpango wa kuondoka ikulu. Kama mtakubuka kwanza kuliwa na minong'ono ya kuahirishwa kwa uchaguzi. Baada ya watu kupiga kelele kwa kuwa walikuwa wamechafukwa ndani na nje ya green, ikawa kama imefukiwa hiyo agenda. Lakini hadi siku chache kabla ya kuapishwa kiongozi mpya, aliendelea kufanya teuzi hali isiyo ya kawaida.

Naomba nisiongelee mawazo yangu kipindi kilichofuata hadi jana.
Kuanzia hapa tulipo, naona sasa Mulugo anarudi kwenye baraza soon.
 
Sisi wasukuma tunapata shida sana maana tutikosoa tu utasikia huyu ni sukuma gang ...sasa tuwaache wagawane mbao ila wasisahau matokeo ya urais ama kula nyingi ziko kanda ya ziwa.Acha walete usela mavi tutakutana 2025
Nani kakwambia CCM inahitaji kura ya mtu kushinda? Hata msipopiga kura sisi tutashinda tu, ni kiasi cha kupakia mabegi kwenye fuso tu.
 
Samia mjanja sana!

1. Dotto Biteko Geita
2. Angela Mabula Mwanza
3. Mashimba Ndaki Simiyu
4. Patrobas Katambi Shinyanga!

Kanda ya Ziwa kagusa! Karibu sehemu kubwa! Na tangu awe Rais, kaenda Mwanza zaidi ya mara 3!

CCM hata wakiweka jiwe watashinda, kile Ni chama dola sio chama Cha siasa. Ndio maana hata speaker alipotoa maoni yake Ni CCM walimuondoa haraka.
 
Watanzania zumbukuku kaeni mkao wa kushangilia wapigaji wanapokula hata kama hutapata hata senti yao moja toka pesa zenu za kodi mtakazotozwa kwa kushangilia kwenu.

ID fake za EFD za revenue collection kwa wadau wasio na maslahi kwa umma zimeingia tena vuup bila hodi ! Wataiona pesa inaingia kwao mapema asubuhi kabla hawajapiga mswaki bila wajibu wao kazini. Tumekwisha! Tulidhani Zanzibar kulikuwa na ufalme pekee kumbe hata Tanzania bara umerudi. Karume kisha mwanae sasa.

Mwinyi kisha mwanae na Hulu bara hali kadhalika habari ndiyo hiyo!
 
Samia mjanja sana!

1. Dotto Biteko Geita
2. Angela Mabula Mwanza
3. Mashimba Ndaki Simiyu
4. Patrobas Katambi Shinyanga!

Kanda ya Ziwa kagusa! Karibu sehemu kubwa! Na tangu awe Rais, kaenda Mwanza zaidi ya mara 3!
Wakat huku Lindi na Mtwara hajawahi kukanyaga ..ht moja
 
Sisi wasukuma tunapata shida sana maana tutikosoa tu utasikia huyu ni sukuma gang ...sasa tuwaache wagawane mbao ila wasisahau matokeo ya urais ama kula nyingi ziko kanda ya ziwa.Acha walete usela mavi tutakutana 2025
Ngosha,

Fanya kazi. Wasukuma ni watu wa kazi, tunajua mlikuwa victims waMagu kiasi kwamba mpaka sasa mna hang over isiyoeleweka.

Hicho kikura chako hakitabadili chochote kile.

Anyway, Magu hakuwa msukuma.

Mimi pia kwetu LAKE ZONE.
 
1. Ni mabadiliko ya kuonyesha kumbe kulikuwa hakuna kabisa Maelewano kati ya aliyelala mazima na aliye Hai akiendelea na Kazi, bali ni Unafiki mtupu ndiyo ulikuwa Umeshamiri japo kuna Mtu kila katika Hafla alikuwa akionekana Kutabasamu na hata Kutuhutubia Watu kwa Kuunga mkono harakati zote za Kiutendaji za kuanzia 2015 mpakae tarehe 17 Machi, 2021.

2. Ni mabadiliko ya Kufyagia mazalia yote ya aliyelala mazima ili aliye Hai aweke anaowaamini na watakaomsujudia pia.

3. Ni mabadiliko ya Kimkakati hasa kwa Kumteua tena Mtu ambaye aliondoshwa mahala fulani mpaka Kutishiwa Bastola kwa Tukio baya la 'Gaidi na Fisadi Matege' mahala fulani Mikocheni hivyo amerudishwa hapo ili Kesi ya Tukio hilo sasa irejewe upya na hatimaye Mhusika akamatwe ili Chanzo cha Mashitaka mengine makubwa yanayomkabili kipatikane na hatimaye nae mwaka huu 2022 akione cha Moto ( Mtema Kuni ) kama alichokiona Mwenzake wa Hai Mkoani Kilimanjaro.

4. Ni mabadiliko ya Kuwafyagia waliokuwa Wanafiki wa Kipindi cha aliyelala mazima na Kuwakaribisha wapenda Uhalisia ila wasiopenda Kukosolewa wa aliyeko.

5. Ni mabadiliko ya Kuwathibitishia Watu kuwa kuishi Magogoni au Chamwino au Zanzibar hakuangalii sana Jinsia ya Mtu bali ni Kujiamini, Uwezo na kuwa Mwanadiplomasia mwenye Ubabe Moyoni kama si Rohoni.

6. Ni mabadiliko ya muendelezo wa Utamaduni wa Kiafrika kuwa Kipaumbele Kikuu ni Kuunda Safu yako ( Genge lako ) ili ule vyema na kwa Kujiamini kabisa Rasilimali Keki zilizopo kwa 95% na matatizo ( mahitaji ) ya Watu uyakabili kwa 5% tu ukiamini kuwa wanaokuja nao watayatatua.

7. Ni mabadiliko hasa ya Kutuonyesha wenye Akili Kubwa kuliko Wao kuwa si kweli kuwa kuna Watu wanakitaka Kiti cha Ufalme kama tulivyodanganywa kama si Kuaminishwa hapa Juzi kati Mkutanoni bali Lengo Kuu ni Kuua Makundi ( Magenge ) hasa Kuelekea Chaguzi ndani ya Nyumba Kuu ya Kitawala ( Kisiasa ) mwaka huu na kwamba japo Zanzibar inatuongoza Machoni mwetu ila uhalisia ni kwamba Pwani ( Bagamoyo na Chalinze ) ndiyo Usukani Kamili wa Tanzania kuanzia Machi 2021 mpaka 2025 na huenda hata 2025 hadi 2030.

Hongereni na Poleni kwa Mabadiliko.
Siasa na mpira wapi na wapi? We baki na simba yenu, siasa waachie wenyewe
 
Mkuu una jicho zuri Sana. Nimelipenda jicho lako
 
Samia mjanja sana!

1. Dotto Biteko Geita
2. Angela Mabula Mwanza
3. Mashimba Ndaki Simiyu
4. Patrobas Katambi Shinyanga!

Kanda ya Ziwa kagusa! Karibu sehemu kubwa! Na tangu awe Rais, kaenda Mwanza zaidi ya mara 3!
Umesahau na yule Waziri wa ulinzi.
 
Back
Top Bottom