Jicho langu la Kiufundi na Tahadhari kwa Simba SC kuelekea katika ' Desicive Game ' yake na AS Vita Club tarehe 2 April, 2021

Jicho langu la Kiufundi na Tahadhari kwa Simba SC kuelekea katika ' Desicive Game ' yake na AS Vita Club tarehe 2 April, 2021

Umenena ukweli mtupu

Kuna kipindi nilibishana na mpuuzi moja kibanda-umiza,ila game ya merreikh kutoka nao sare, Kutokuwafunga wale vibonde kule kwao, bado kunatuweka wakat mgumu...
Kibonde kwenye group akifungwa na wenzio woote kisha ww usimfunge ana kudhurumu mahesabu

Ile mechi ilikuwa muhimu saana, kwanza ingeamua sisi kufuzu kwa kushika usukani, jambo ambalo ni zuri zaidi, hatua inayofata tungekutana na maji yetu, ila tukifuzu watu wa pili, robo fainali tutaangukia kwa mamelodi, esperence ama wydad casablanca aisee.. Hawa sio watu wazuri kabisa..

Pili mpaka sasa hatujafuzu, tutegemee mechi ngumu mnoo kutoka kwa as vita, vita watakuja kichwa, miguu, mikono, kila kitu yaani wazima wazima, hawana cha kupoteza na mpira hauna adabu unaweza ukapigwa kimoja, ikawa chomoa, chomoa na ww.

Yote kwa yote kila la kheri chama langu
Na simba atapigwa kimoja na hatachomoa mimba ya albino hiyo ukichomoa unaondoka nayo.​
 
Tatizo la defense kupoteza umakini hasa dakika za lala salama ilitokea hata dhidi ya Al Ahly Manula akatuokoa kama jana. Tusipokuwa makini dhidi ya Vita kuna uwezekano mkubwa tukafungwa.

Namuomba Didier atumie muda mwingi zaidi mazoezini kufanya ukarabati mkubwa safu ya ulinzi.
Kuna kipindi mabeki walijisahau wakafikiri jukumu.lao kubwa ni kufunga
 
Wachezaji wamecheza vizuri sana kama timu. Tatizo kubwa lipo kwa mugalu na chama kwenye umaliziaji, chama anatakiwa kuwa na mentality ya kufunga sio anawaza tu kutoa pasi na pia anatakiwa kuwa sharp kufanya maamuzi kwa zile beki za vita watampa ulemavu.
Mugalu tutafute mbadala kwa mechi zijazo
Kahata alibadili mpira na kuwa wenye ladha ndani ya muda mfupi, kocha amtafutie nafasi ili miq na Morri wasogee mbele kusukumia wavuni
Mugalu mi namwona ni mchezaji mzuri hasa kwa mfumo. Sometime pressure inamsumbua. Abaki
 
Mugalu mi namwona ni mchezaji mzuri hasa kwa mfumo. Sometime pressure inamsumbua. Abaki
Huyu jamaa match na Vita acheze first half tu..
Simba ikienda misri acheze vipindi vyote!
Mungu amsaidie Onyango apone, maana huyu Muduva sijui bado mfumo hajauelewa!
Mzamiru angekua makini angesaidia match na Vita ila
Coach ajaribu friendly match lwanga na Mkude kwa ajili ya maandalizi game na VITA,
Bwalya pia asinze ikiwezekana
 
Bado beki zinafanya makosa ya kipuuzi credit kubwa zimwendee Onyango anavyojitoa, tatizo la kukaa nq mpira halipo kwa Chama peke yake hata Shabalala anakaa sana na mpira kwa mpira wa sasa ambao timu inashambulia na kulinda kwa haraka unapokaa sana na mpira unampq advantage timu pinzani.
Mugalu anakosa magoli menginya wazi aongeze umakini na Mzamiru anarudia makosa yaleyale kila siku mipira yake ya mwisho mingi haona faida.
Pamoja nq hayo tuwapongeze benchi la ufundi pia warekebishe mapungufu yanayoendelea ili timu yetu iimarike zaidi.
Kwa kweli chama anakaa sana na mpira lakini mugalu umuhimu wake upo sana yule jamaa tofauti na kagere yule jamaa anakaa kwenye position yake ...hivo inakua ngumu kwa mabeki kupanda mbele tofauti na kagere ambaye anamove saaana

My opinion mugalu atafutiwe mbadala ni mtu mwenye stamina lakini kasi hana ambayo ni muhimu pale timu inapozidiwa na mnabidi mtumie counter kwa mipira ya kutanguliziwa
 
Hivi nyie utopolo mtaendelea kututisha Simba kwa riwaya katika media?

Kama club bingwa Afrika amefungwa,unaanzaje kututisha na wengine ambao ni size yetu tu?

Hivi hamjui nao wanatuogopa?
Umenena ukweli mtupu

Kuna kipindi nilibishana na mpuuzi moja kibanda-umiza,ila game ya merreikh kutoka nao sare, Kutokuwafunga wale vibonde kule kwao, bado kunatuweka wakat mgumu...
Kibonde kwenye group akifungwa na wenzio woote kisha ww usimfunge ana kudhurumu mahesabu

Ile mechi ilikuwa muhimu saana, kwanza ingeamua sisi kufuzu kwa kushika usukani, jambo ambalo ni zuri zaidi, hatua inayofata tungekutana na maji yetu, ila tukifuzu watu wa pili, robo fainali tutaangukia kwa mamelodi, esperence ama wydad casablanca aisee.. Hawa sio watu wazuri kabisa..

Pili mpaka sasa hatujafuzu, tutegemee mechi ngumu mnoo kutoka kwa as vita, vita watakuja kichwa, miguu, mikono, kila kitu yaani wazima wazima, hawana cha kupoteza na mpira hauna adabu unaweza ukapigwa kimoja, ikawa chomoa, chomoa na ww.

Yote kwa yote kila la kheri chama langu
 
Chama anakosa kujiamini mara nyingi akiwa eneo la adui, anakaa na mpira anachelewa kuchukua maamuzi matokeo yake anawapa nafasi wapinzani wajipange na kuokoa hatari langoni mwao.

Hili tatizo lake aambiwe alifanyie kazi, akitaka kuremba awe anaremba katikatika ya uwanja, lakini sio wakati timu ime break kwa counter attack unakita wako three against two halafu tunaupoteza mpira kizembe coz of him delaying the move.

Hao Vita ni kuwakazia tu, naamini hata wachezaji wa Simba SC wanajua umuhimu wa hiyo mechi, hawatakiwi kuremba kabisa, hiyo ndio tiketi yao kwenda robo fainali, kama walikufa kwao sioni sababu kwanini wasife kwa Mkapa.

Mwisho kabisa napata ukakasi na bonasi wanazopewa wachezaji kama timu ikishinda, huwa najiuliza hivi ikitokea wasiahidiwe bonasi hawatacheza kwa kujituma? kwanini watu wanaolipwa mishahara mizuri bado mpaka waahidiwe bonasi ndio washinde? hapa kwangu nawaona wachezaji wamekosa professionalism, ni kama wanadekezwa ndio mana mitimu kama Prison huwa zinatusumbua.
 
ANGALIZO

Nitakayoyaandika (Kuyaeleza) hapa ni Maoni na Mtizamo wangu Mimi All - Rounder na sikulazimishi uukubali bali uheshimu tu tafadhali.

PONGEZI
Nisiwe mchoyo wa Pongezi kwa Mafanikio haya makubwa ambayo kwa sasa Klabu ya Simba imeyafikia ikiwemo Ushindi wake wa jana wa Magoli 3 kwa 0 na pia kuwa na Clean Sheet ya Kutokuruhusu hata Goli 1 katika Michezo yake Minne ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CL)

Pia nitoe pongezi zangu nyingi sana kwa Serikali ya Tanzania (kupitia Wizara husika ), Uongozi mzima wa Klabu ya Simba kuanzia Mwekezaji Mohammed Dewji, CEO Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangungu, Msemaji wa Simba Haji Manara na Wanachama, Wapenzi pamoja na Mashabiki wote wa Simba SC na Wachezaji wote wa Simba SC kwa Ushirikiano wao mkubwa ambao umezalisha Mafanikio haya ambayo hayaipaishi tu Tanzania pekee bali hata Afrika ya Mashariki nzima imewakilishwa vyema na Simba SC.

MAPUNGUFU YA KIMSINGI YA KIKOSI
Pamoja na kwamba Simba SC imepata (imefikia) Mafanikio haya ila nisiwe Mnafiki na wala tusifichane kuambiana Ukweli kuwa bado Klabu ( Kiuchezaji na Kiufundi ) ina matatizo ya Kimsingi ambayo kama yasipofanyiwa Kazi haraka kuna Uwezekano Mechi yetu dhidi ya AS Vita Club ambayo Kwangu Mimi itakuwa a Decisive Game basi tukafungwa na Ndoto yetu ya Kutinga Nusu Fainali ikaishia kwa kutokufuzu hata Robo Fainali yenyewe.

Bado Mabeki wa Simba SC wameendelea na tatizo lao lile lile la kupoteza Umakini katika Kukaba, Kujisahau, Kutegeana huku Mabeki wa Kati Wakijichanganya na wa pembeni kupenda kupanda Kushambulia na Kuchelewa kurejea kwa haraka.

Sina shida sana katika eneo la Kiungo kwani wanajitahidi kutekeleza vyema Majukumu yao na huenda hata Mafanikio haya ya Timu Kutokufungwa hadi sasa yamechagizwa na Idara hii Muhimu kwakuwa Mipango yote ya Wapinzani huwa inaharibiwa Kiustadi na Ushirikiano mkubwa wa Viungo wa Kimkakati akina Thadeo Lwanga na Muzamiru Yasin huku akina Miquissone na Chama au Larry Bwalya na Bernard Morrison wakichagiza katika Kuwachanganya Maadui hadi Kuwadhoofisha.

Washambuliaji wa Simba SC hasa Kinara wao wa sasa Chris ' Kopa ' Mugalu, Meddie Kagere na John Boko wanajitahidi mno na tunawapongeza kwa hili ila wana Makosa ya Kiufundi sana ambayo kuna muda yanasababisha hata wawe wanakosa Kizembe zaidi Magoli au kusababisha Timu ishinde kwa taabu au kwa Magoli machache.

CLATOUS CHAMA NI KIKWAZO AONYWE
Wiki kadhaa hapa hapa JamiiForums na katika Jukwaa hili hili niliwahi Kuandika Mada ya Kumsema na Kumkosoa Clatous Chota Chama kuwa anatuchelewesha mno Ushindi kwa Kuremba sana Mipira nikaeleweka namchukia ila nashukuru sasa kuwa Observation yangu kumuhusu imeanza Kueleweka na sasa Sote tunaimba nyimbo moja ya Kukereka ( Kukerwa ) nae.

Naendelea Kusisitiza kuwa Clatous Chota Chama ni Mchezaji very Talented, Intelligent ( Football Genius ) na Playmaker hasa ila ana tatizo moja Kubwa la kutokujua wapi arembe ili kuwapotezea muda Wapinzani ( Timu ikiwa inaongoza ) au wapi anatakiwa achangamke kwa kutoa ( kuachia ) Pasi kwa haraka kwa Wenzake wakiwa katika Striking Momentum ili Timu ishinde.

Kwa aina ya Uchezaji wa Clatous Chota Chama Mimi All - Rounder ningekuwa ni Kocha ningekuwa namchezesha pale tu Timu ikiwa imeshashinda ili kuwapotezea muda Wapinzani au katika zile Mechi nyepesi ambazo najua Simba SC itashinda tu hata kama Ushindi utachelewa ila katika zile Tough Games kamwe sitoweza Kumuanzisha au hata Kumpanga kwani ameshaonyesha kuwa akikutana na Timu inayocheza Mpira wa Nguvu ( Kazi Kazi ) huku Wachezaji wake wakiwa wanafika ( wanagongana ) huwa hafui dafu na Mpira unamshinda.

Benchi la Ufundi ama limuonye au limrekebishe abadilike japo nimeanza kuona ni kama vile Clatous Chota Chama ama anaogopwa au Ufalme wake ndani ya Kikosi unamfanya kuwa ni Untouchable na above the whole Team hivyo na Yeye pia kujawa na Kiburi, Jeuri na hata Dharau kwakuwa anajua hakuna wa kumwambia Kitu kwani ameshaziteka Akili za wanasimba wote.

UKWELI MCHUNGU KUHUSU AS VITA CLUB
Hapa wala tusidanganyane kwa tunaojua Mpira au hata tu Kucheza na kuwa Wafuatiliaji wazuri wa Mipira tutakubaliana kuwa hakuna Mechi ambayo Simba SC itapata Usumbufu, Shida na Taabu kama hii itakayocheza na AS Vita Club tarehe 2 April, 2021.

Kwa Mtu aliyewatizama walipocheza Mechi zao na Al Ahly na hata ile ya dhidi ya Simba SC kwao Congo DR atakubaliana nami kuwa hawa Jamaa wapo vizuri tena katika kila Idara na wanaupiga mwingi mno huku Silaha yao Kubwa ni Kucheza Kitimu zaidi tofauti na Simba SC ambayo muda mwingi wanacheza Kibinafsi zaidi.

Kwa Mapungufu ya Kimsingi ya Simba SC ambayo nimeyaelezea vyema tu hapo juu kama hawa AS Vita Club wakija Dar es Salaam ( kwa Mkapa ) na Kucheza Mpira wao ninaoubatiza ' Pira Nguvu, Pira Mbio, Pira Ufundi na Pira Pumzi nyingi ' kuna Uwezekano Simba SC ikafungwa ( japo siombei ) goli zaidi hata ya Moja. Tuwe Makini nao sana tafadhali.

NINI KIFANYIKE?
Kuanzia sasa (leo) Simba SC hasa Benchi la Ufundi liweke Mkakati mzito wa namna ya Kukabiliana na AS Vita Club ambao Mimi All - Rounder nawaogopa hata kuliko Al Ahly.

Mapungufu yote niliyoyaainisha hapa katika huu Uzi wangu yafanyiwe Kazi na Wachezaji wa Simba SC ikiwezekana katika hiyo ( hii ) Mechi wajitoe Maradufu kwa Kupambana Uwanjani ( wakiweza hata Kufia Uwanjani ) ili tushinde au ikishindikana basi tutoke nao Sare (Suluhu ) tu ambayo itatuvusha kwenda Robo Fainali.

SAIKOLOJIA
Nashauri kuelekea Mechi hii Muhimu na ya Kimaamuzi kwa Simba SC basi apatikane haraka Mtu wa Saikolojia ili aweze Kuwajenga vyema Kiakili Wachezaji wetu kuelekea Mechi yao na AS Vita Club.

Kiufundi Saikolojia nayo ina nafasi kubwa sana katika Mafanikio ya Timu hivyo hili lisipuuzwe na lizingatiwe kwa Umakini mkubwa sana. Wachezaji wa Kiafrika ( hasa ) wa Kitanzania tunawajua wenyewe katika nyakati kama hizi hivyo Saikolojia ni Muhimu Kwao.

HITIMISHO
Mpaka hapa ilipofika sina Shaka na Simba SC na najua itafanya vyema tu ila kupeana Ushauri na Tahadhari si Jambo baya kama sehemu ya Uanamichezo na Upendo kwa Timu husika.

Uongozi endeleeni kutoa Motisha zenu ( Pesa ) kwani hii nayo nina uhakika imechangia Mafanikio haya ya Simba SC kwani Wachezaji wana uhakika mkubwa wa Ustawi wao wa Kiuchumi.

Mwenyezi Mungu aipiganie Simba SC, aibariki zaidi na ifanikiwe kushinda Mechi yake hii Muhimu dhidi ya As Vita Club ili itinge Robo Fainali na tujipange zaidi kuelekea katika Lengo Mama letu la kufika Nusu Fainali kwa Msimu huu.

OMBI
Naomba Uzi huu kwa aliye karibu na Uongozi wa Simba SC au Benchi la Ufundi au Bodi ya Simba SC au Haji Manara awafowadie ili na Wao wauone na wausome nikiamini kuna mema na mazuri tu ya Kiushauri watayapata hapa.

Na wale ambao huwa mnapenda Kuchukua Mada hapa JF na Kuzichapisha ( Kuziweka ) katika Magazeti yenu au Mitandao yenu mbalimbali ( siyo JamiiForums ) tafadhali mkipenda Kutumia hili Bandiko langu kuweni Waungwana kwa kunipa Credit ( Acknowledging ) na pia Kuutaja huu Mtandao wa JamiiForums kuwa ndipo umetoa Uchambuzi huu.

Inakatisha tamaa pale Mtu anapotumia muda wake mwingi, Akili zake za Kiuchambuzi na Kimtizamo pamoja na Maarifa kisha unaikuta Taarifa ( Habari ) yako imechapishwa ( inatumika ) Kwingineko na wakisema ni yao. Ni matumaini yangu makubwa hili litazingatiwa kama ambavyo All - Rounder nimeshauri na kulitahadharisha pia. Sikatai Kutumika ila Credit from the Source ifanyike tafadhali.

Kila Ia Kheri

Wenu All - Rounder ( alias ) Brainiac
mkuu gentamicin waga unatoa wapi haya madini mzee

nimekubali 🤝🤝
 
frengwaaa ila kwa Chama umekosea, huyo jamaa ndio decesive midfielder wa goals nyingi za Simba , either zitaanzia wake au kusabababisha. Yeye anaslow game na kui nyanyua game. Anaujua, another factor ya muhimu Simba game ya Vita warelax na Managua wanachokitafuta, uzoefu wa mashindano haya so far utawapiga chapuo. Simba knows what they want na Managua sisi Mashabiki na Nchi nini kinahitaji
 
Wachezaji wamecheza vizuri sana kama timu. Tatizo kubwa lipo kwa mugalu na chama kwenye umaliziaji, chama anatakiwa kuwa na mentality ya kufunga sio anawaza tu kutoa pasi na pia anatakiwa kuwa sharp kufanya maamuzi kwa zile beki za vita watampa ulemavu.
Mugalu tutafute mbadala kwa mechi zijazo
Kahata alibadili mpira na kuwa wenye ladha ndani ya muda mfupi, kocha amtafutie nafasi ili miq na Morri wasogee mbele kusukumia wavuni
kwa sasa mugalu mbadala wake ni kagere tu haina namna wakizungushana na bocco. Pia Miraji wanamchukulia poa sana ni fundi huyo adunje kama vipi apewe tisa tu hapo
 
Kuna kipindi mabeki walijisahau wakafikiri jukumu.lao kubwa ni kufunga
Defense ilikuwa tight muda wote. Kawaida kama forward zinafanya upuuzi basi mido huwa zinaingilia jukumu la kufunga na baadae defenders wanaingilia Kati kama alivyofanya tshaba na kupata goli lililowapa aibu forward. Mwisho tungeanza kuona morison na miq wanalazimisha wafunge kwasababu vinginevyo mechi ingeisha draw na hata kupoteza. Hii mechi kipindi cha kwanza tu tungeenda na goli 5 achilia mbali kipindi cha pili.
Kazi kubwa iliyopo kwa kocha ni finishing, huwezi kupata nafasi za wazi namna ile dhidi ya vita na ahly
 
Chama anakosa kujiamini mara nyingi akiwa eneo la adui, anakaa na mpira anachelewa kuchukua maamuzi matokeo yake anawapa nafasi wapinzani wajipange na kuokoa hatari langoni mwao.

Hili tatizo lake aambiwe alifanyie kazi, akitaka kuremba awe anaremba katikatika ya uwanja, lakini sio wakati timu ime break kwa counter attack unakita wako three against two halafu tunaupoteza mpira kizembe coz of him delaying the move.

Hao Vita ni kuwakazia tu, naamini hata wachezaji wa Simba SC wanajua umuhimu wa hiyo mechi, hawatakiwi kuremba kabisa, hiyo ndio tiketi yao kwenda robo fainali, kama walikufa kwao sioni sababu kwanini wasife kwa Mkapa.

Mwisho kabisa napata ukakasi na bonasi wanazopewa wachezaji kama timu ikishinda, huwa najiuliza hivi ikitokea wasiahidiwe bonasi hawatacheza kwa kujituma? kwanini watu wanaolipwa mishahara mizuri bado mpaka waahidiwe bonasi ndio washinde? hapa kwangu nawaona wachezaji wamekosa professionalism, ni kama wanadekezwa ndio mana mitimu kama Prison huwa zinatusumbua.
Mimi huwa nawaza simba tukisitisha kutoa bonasi 2 za milioni 200 jumla 400 na tuzielekeze kununua basi lenye hadhi ya simba. Haiingii akilini unatoa bonus mil 200 kwa mechi moja halafu timu inatumia basi la milioni 40 miaka nenda rudi
 
Tatizo la defense kupoteza umakini hasa dakika za lala salama ilitokea hata dhidi ya Al Ahly Manula akatuokoa kama jana. Tusipokuwa makini dhidi ya Vita kuna uwezekano mkubwa tukafungwa.

Namuomba Didier atumie muda mwingi zaidi mazoezini kufanya ukarabati mkubwa safu ya ulinzi.
halafu pia manuraaa anachelewa sana kujishauri akirudishiwa pasi na beki zake
 
kwa sasa mugalu mbadala wake ni kagere tu haina namna wakizungushana na bocco. Pia Miraji wanamchukulia poa sana ni fundi huyo adunje kama vipi apewe tisa tu hapo
Kuna umuhimu wa kuwa na combination mbadala pale mbele. Sipati picha kwa zile nafasi zingemkuta okwi na kagere wa wakati ule
 
Mimi huwa nawaza simba tukisitisha kutoa bonasi 2 za milioni 200 jumla 400 na tuzielekeze kununua basi lenye hadhi ya simba. Haiingii akilini unatoa bonus mil 200 kwa mechi moja halafu timu inatumia basi la milioni 40 miaka nenda rudi
Hili nalo ni Neno Kuntu kabisa Ndugu.
 
halafu pia manuraaa anachelewa sana kujishauri akirudishiwa pasi na beki zake
Ila kwa sasa Kipa Aishi Salum Manula amebadilika sana Kiakili na Kiuchezaji. Pongezi nyingi kwa Kocha wa Makipa Mbrazil kwani amembadilisha Vitu vingi ila Kubwa ameweza Kumjengea zaidi Confidence na hata Footwork yake Manula ya sasa iko juu mno. Akifungwa ni bahati mbaya tu na nu hali ya Kimchezo.
 
Mimi huwa nawaza simba tukisitisha kutoa bonasi 2 za milioni 200 jumla 400 na tuzielekeze kununua basi lenye hadhi ya simba. Haiingii akilini unatoa bonus mil 200 kwa mechi moja halafu timu inatumia basi la milioni 40 miaka nenda rudi
Mkubwa huko ni kuingilia mfumo wao wachezaji mpira ndio ajira na pia uongozi matokeo ndio kipimo Chao cha timu kilele cha mafanikio yao km kipimo ss waache wanunue basi sioni kbs wanaweza pata kwa namna nyingine

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Ila kwa sasa Kipa Aishi Salum Manula amebadilika sana Kiakili na Kiuchezaji. Pongezi nyingi kwa Kocha wa Makipa Mbrazil kwani amembadilisha Vitu vingi ila Kubwa ameweza Kumjengea zaidi Confidence na hata Footwork yake Manula ya sasa iko juu mno. Akifungwa ni bahati mbaya tu na nu hali ya Kimchezo.
Nimeliona hilo kwa manula amebadilika sana kuanzia decision making, positioning, body movements, confidence hata mipira ya nje ya 18 si threat tena kwake na mashabiki
 
Back
Top Bottom