Mapensho star
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 3,052
- 4,104
Somo letu la Leo tutazungumzia Jinsi ya kuandika matangazo yenye mvuto. Kwa hivyo kama unafanya biashara, unauza bidhaa au unatoa huduma, labda umeshawahi kujaribu kuandika matangazo lakini hujapata matokeo mazuri basi naomba ufuatilie kwa umakini sana makala hii kwani nataka nikupe fomula ambayo unaweza kuitumia mara moja katika kuandika matangazo na ikakuletea matokeo mazuri sana.
Kabla ya kuangalia fomula hiyo kwanza ningependa niongelee aina za matangazo. Kuna aina mbili kubwa za matangazo
Aina ya kwanza inaitwa Institutional Advertising: Aina hii ya matangazo ni matangazo yanayozungumzia kampuni/biashara yako, yanazungumzia bidhaa au huduma unayotoa. Pia tunaweza kuiita branded advertising yaani tangazo lako linakuwa linaisifia kampuni au bidhaa unayouza. Na tunaweza kuona matangazo hayo kama vile mataangazo ya Tigo, CocaCola, matangazo mengi tunayoona kwenye Tv yanakuwa ni Institutional advertising.
Hakuna ubaya katika aina hii ya matangazo ispokuwa matangazo haya yanahitaji uwe na subira katika kupata matunda. Yaani unatakiwa uwekeze kwa kiasi kikubwa mpaka watu waone matangazo yako sana mpaka wazoee brand yako ndio waanze kukuamini na kuanza kununua bidhaa na huduma unayotoa.
Kama biashara yako ni ndogo na sio kubwa kama Tigo, Airtel au vodacom basi institutaional advertising inaweza ikakutia hasara. Na ukiwa unajaribu wewe kama mfanyabiashara mdogo kufanya institutional advertising katika biashara yako ndogo basi unaelekea kuiua biashara yako. Kwa hiyo kama unafanya biashara ndogo nakushauri njia nzuri unayoweza kutumia kutangaza biashara yako ni kufanya Direct Response Advertising. Hii ni aina ya tangazo ambao baada ya kujizungumzia wewe unamzungumzia mteja.
Angalia mfano ufuatao ili uweze kuelewa kwa undani tofauti iliy opo kati ya institutional advertisng na direct response advertising. Mimi ninamiliki hospitaali. Kama nitaamua kutangaza hospital yangu kupitia intitutional advertising, tangazo langu litakuwa Temeke Hospital ni hospital bora kuliko Hospitali zote za dar vifaa vizuri na madaktari wazuri, Karibu sana Temeke hospital Upate huduma bora zaafya]” Katika tangazo hili mtu anayesikiliza hautegemei akuamini kwa 100% kwa sababu hakujui, hakufahamu na wala hakuamini kwa hiyo kwa kuweka tangazo hilo sio rahisi kumshawishi kuja kupata hudumaa katika hospitali yako japokuwa baadhi ya watu wanaweza kufika kutokana na tangazo hili. Na kama nitaamua kutengeneza tangazo la Direct Response Advertising tangazo litakuwa kama hivi “[Habari muhimu kwa wagonjwa wote wa sukari, Kisha nitaandika, Kama wewe ni mgonjwa wa sukari ambaye umekuwa unahangaika kwa muda mrefu, basi nifuatilie kwa makini kabisa kwani katika makala hii naenda kukuonyesha hatua 5 unazoweza kuzifuata ili kuondoa tatizo lako la sukari.]” Kwa hiyo hapo sijaizungumzia hospitali, sijajizungumzia mimi na wala sijazungumzia product au huduma ninazotoa bali nimezungumzia tatizo la mteja na suluhisho lake. Kwa hiyo ndani ya makala hiyo nitazungumzia tatizo la mteja na suluhisho lake. Na mwisho kabisa nitaweka Kwamba katika siku ya jumamosi kutakuwa na consultation ambayo watu 20 wa mwanzo watapatiwa consultation bure. Na ukikosa kuwa kati ya hao watu 20 wa mwanzo, basi itakugharimu kiasi cha pesa si chini ya laki moja. Kwa hiyo fanya booking haraka ili kupata nafasi hii, Kwa hiyo hapo mgonjwa yeyote wa sukari akishasoma hiyo makala kuna uwezekano mkubwa wa kupiga simu na kuweka booking. Kwa hiyo hapo focus inakuwa kwa mteja na sio kwako, kwa hiyo mwisho ninaweza nikaandika jina la hospitali yangu lakini mwanzoni nimeanza kumzungumzia mteja, tatizo lake na suluhisho lake.
Kwa hiyo tofauti kubwa iliyopo kati ya Institutional advertising na Direct Response Advertising ni kwamba institutional advertising inafocus kwenye kampuni au huduma unazotoa wakati Direct Response Advertising inafocus kwa wateja. Njia nzuri zaidi ni ya kufocus kwa wateja na sio kujifocus wewe mwenyewe.
Jinsi ya kuandika tangazo la Biashara yako
AIDA formula.
A=Attetion grabing headline, Ni kuwa na kichwa cha habari cha tangazo lako chenye mvuto. Kwa hiyo kama una bidhaa inayosaidia watu kupunguza uzito, unaweza ukaandika Jinsi ya kupunguza uzito bila ya kufanya mazoezi wala kumeza dawa. Kichwa cha habari kizuri ni kile kinachoelezea jinsi ya kusolve tatizo.
I=Interest, Unatakiwa kumfanya mtu aendelee kusoma tangazo, lengo la Kichwa cha habari ni kumfanya mtu asome mstari wa kwanza wa Tangazo na lengo la mstari wa kwanza ni kumfanya mtu aendelee kusomaa mstaari wa pili vivo hivyo hadi mwisho wa tangazo.
D=Desire, Unataka kumfanya awe na hamu ya kuja kwako kupata suluhisho la tatizo yake, na hapa ndio unasema “Kama umependa makala hii, au audio hii au somo hili basi tunatoa ushaauri wa bure juu ya jambo hili (Ulilolizungumzia ) au maneno mengine ambayo yatamfanya mteja aje kwako kupata suluhisho”.
A=Action, Hapa unamwambia afanye nini?, Kwa mfano katika tangaazo unamwambia Kufanya booking Piga simu. Na hapa hautangazi bidhaa, Kosa kubwa linalofanywa na watu wengi ni kutangaza bidhaa au huduma katika matangazo yao. Usifanye hivyo, bali toa kitu bure kabla ya kuanza kuuza bidhaa au huduma.
Nakuhakikishia kama utaanza kutumia fomula hii katika matangazo yako, utaanza kuona matunda yaake hivi punde.