Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Awali yote niwashukuru sana mlioanzisha na kuchangia katika uzi huu kwani mmenielimisha hadi nikafanikiwa kufanya manunuzi online na kuweza kuutuma mzigo kupitia carrier DHL.

Naomba kuuliza hivi mzigo unachukua siku ngapi unapofika Dar ndipo usafirishwe kuja mkoani ? Cz nimekuwa niki utrack tokea huko sasa nashangaa ulipoingia dar umeshakaa zaidi ya siku tatu.
 
Kuna matapeli mtandaoni ukiwapa credit card details wanahamisha account yote!
 

Huenda ikachukua hadi siku 14 - 21 kukufikia mzigo. Huu ni uzembe mkubwa sana, tena sana, Kwa mzigo uliotoka nje ya nchi kwa siku 3-5.

Mfano iwapo mimi wa Dar kwa mzigo uliofika tangu 04 March 2016 mpaka sasa bado haijafahamika ni lini hasa watautoa.

Sababu kubwa wanayotoe eti TRA bado hawajaukagua, na wanamizigo mingi inayoingia na yote inasubiri kukaguliwa na TRA.

Angalia hii picha

 
------------------------------------------------------
Mrejesho:
Mzigo niliupata baada ya siku 9 tokea ulipofika Dar kuja Mwanza. Mbaya zaidi kodi niliyokuta nadaiwa na TRA ilikuwa Mara mbili ya bei ya mzigo niliyonunulia. Sikuwaelewa kabisa,ikabidi wanipe simu niongee na mtu wa custom ambaye alisema kuwa baada ya wao kuukagua mzigo wamebaini bei yake ilio ambatanishwa katika documents haiendani na thamani halisi yake na bla bla nyingine kibao tu.
Kuja na kuwauliza WHY inatake muda mwingi hivyo kwa mzigo tukifika Dar wakasema eti tena hapo wala mzigo haujachelewa kabisa, ni kawaida kwa mzigo kukaa Dar ukifika even for 15 days.

Kiukweli Mkuu hawa jamaa wa custom sijui TRA wana waaribia kazi sana hawa jamaa wa DHL. Inakuwa haina maana tena ya neno "Express".
 
Siku nyingine tumia hawa jamaa wanaitwa Armax wao mizigo yao inaingilia Nairobi kutoka pale inakuja kwa post kawaida ni faster na ushuru hamna dhl tulishawaacha siku nyingi ukiwatumia lazima uumie fikiri computer and computer accessories hazina ushuru wowote kwa sera ya serikali lkn kwa hawa jamaa lazima ulipe kiasi chochote
 

Mkuu nashukuru kwa advice. Vipi hao jamaa wapo hadi mikoani??
 
Kwa wale wanaotaka kujiunga na paypal. Kuna hawa UBA bank, wana card zao ambbazo unaweza kufanyia miamala online. Unapata kadi instant ndani ya masaa matatu kadi inakuwa hewani. Unakuwa na uwezo wa kumanage funds online. Kadi ni 11000, hakuna makato ya mwezi. Ila kila ukifanya transaction kununua kitu utakatwa sh 3000. Haina longolongo.
 
BANC ABCni 15000 na unakatwa kiasi unacholipia tu hakuna makato ya transaction wala nini,mfano,unanunua bidhaa yenye thamani ya Usd 120 utakatwa Usd 120 tu

w
 
ahsante mkuu kwa taarifa nitafanya hilo kupitia hawa maana ndiyo bank yangu, na vipi kuhusu ofisi za Fedex zipo kila mkoa mfano kwa dodoma watakuwepo? Belo
Hizo huduma bei yake ni kubwa pia mkuu. Fedex, UPS, DHL ni huduma za ghali kidogo ndio maana kama huna haraka na mzigo bora tu kutumia Standard Internatinal Shiping Yaaani njia ya Posta. Hata EMS pia ni ghali sana kwakweli kuna siku nilitaka kutuma pasipoti nje ya nchi kwa njia ya EMS nikaambiwa ni alfu 65 nilitoka nduki bila kugeuka nyuma. Nikatuma kwa njia ya register kwa sh.7000 na tracking number nikapewa.
 
hello wadau...........samahani napo sign up na ebay pande wa POST CODE SIJAPAELEWA
 
Naomba msaaada mkuu, katika kufanya malipo ni njia ipi ni salaam zaidi kati ya pay pal na kulipa kwa visa card mojamoja (as long as card ina uwezo wa kufanya online transaction)?
 
Naomba msaaada mkuu, katika kufanya malipo ni njia ipi ni salaam zaidi kati ya pay pal na kulipa kwa visa card mojamoja (as long as card ina uwezo wa kufanya online transaction)?
- Pendelea kutumia option ya paypal ni salama zaidi.
- Usipende kutumia card direct ( ila zipo site salama kama amazo .com hapo lazima kadi itumike direct)
Soma ABC za paypal kwa paul s.s hapa: Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni
 
Natumia exim bank vp naweza jiunga na pay pal huko na makato yao yapoje anaejua tafadhali
 
Samahan mi nataka kujua mzigo ukitumwa kwa dhl ni lazima utatozwa gharama za ushuru hata kama ni laptop na ilikuwa labeled as a gift? Mana niliwai sikia viyu vya kujifunzia kama laptop huwa havitozwi ushuru? Afu bado naskia ushuru lazma sasa napata mkanganyiko kidogo
 
Samahan mi nataka kujua mzigo ukitumwa kwa dhl ni lazima utatozwa gharama za ushuru hata kama ni laptop na ilikuwa labeled as a gift? Mana niliwai sikia viyu vya kujifunzia kama laptop huwa havitozwi ushuru? Afu bado naskia ushuru lazma sasa napata mkanganyiko kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…