Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Nina mpango wa, kufungua duka la nguo kuna uwezekano wa kuwa na nunua nguo kwa njia hii
 
naomben mnijuze kuhusu paypal coz wengne n wagen wa mambo hayo
eCommerce- kwa ufupi, kuuza na kununua mtandaoni. Notable multinational ni kama Amazon, Ebay, Alibaba, Best Buy etc.

eBay- multinational eCommerce, unaweza kuuza au kununua, pia kufanya minada.

PayPal- mfumo wa malipo mtandaoni, kulipa na kutuma hela mtandaoni mbadala wa checks na money order or wire order, awali Paypal ilimilikiwa na ebay kama primave payment method baadae paypal ilijitgemea.
Kujisajili PayPal na ebay ni bure, na ukitumia huduma ya PayPal anayelipwa ndo analipia huduma, mfano, nimenunua kitu nkalipa kwa paypal muuzaji ndo atalipia fees, wewe mnunuji hutakatwa chochote.
Natumia sana hii huduma na wateja wangu wanapenda kutumia kwasababu akituma $500 mfano, yeye hakatwi mm ndo ntalipia kama 3% ya total amount. Na pia unaweza kulipia huduma ya kwa paypal hata kama huna account ya paypal.

PayPal Tanzania- Kwa Tanzania watumiaji wa PayPal wanaruhusiwa tu kulipia malipo na sio kupokea malipo, means huwezi ukatoa hela kwa account yako ukahamishia bank, ila unaweza kuweka hela from bank to PayPal ukanunua vitu.

PayPal Kenya- Bank ya Equity upande wa Kenya wameungana na PayPal kutoa huduma ya money withdraw. Maisha wamekuwa murua na sio TZ, BOT hawataki. So napokea malipo through PayPal natuma kwa account yangu then after 3 days hela hiyooo kwa account.

Ushauri- eCommerce ni huduma poa sana Post Office Box inatosha ww kupokea mzigo, lakini umakin unahitajika pia, kama walivyostate hapo juu. PayPal nayo ni huduma poa sana nalipa, nalipwa kwa PayPal app on my phone. email to password nalipwa madola. Hakikisha password hajui mtu au tumia 2-Step Verification kwa account nyeti kama hizo. Pia ukitaka kutoa hela PayPal tafuta someone you can trust Kenya umtumia hela akutolee kwa Equity. Kama una ndugu maisha yanakuwa poa.

No PM please, just ask here.
 







Nokia 6 nimeipata kwa 650000/=, Smart watch kwa 40000/=
Bei ya bongo ilinishinda simple like that...
 
mkuu vipi mimi ambaye hata akaunti ya bank sina?na vip kuhusu kufungua akaunti
 
nimekuelew mkuu lakin sina account ya back nataka nifungue vipi gharama za kufungua
Nenda equity bank na 10000/= pamoja na kitambulisho cha kura siku hiyo hiyo upewe kadi iliyo tayari kufanya manunuzi mtandaoni.
 
Ebay siyo matapeli. Ipo organized sana. Yaani kila utakacho utakipata.

Ila wengi wa wauzaji wanataka uwe na paypal ambayo wengi wa wabongo hatuna au hatujajisaijili na mtandao huo.


Ndugu nimejifunza kitu..

1. Fundi wa vifaa vya teknology wanapata faida ya kifaa, 7bu nimeona vitu ni bei nafuu
2. Tufundishane namna ya kupata bidhaa wakati wa kuagiza
 
Hata ALI EXPRESS wapo vizuri na wanabei nzuri kama ebay
 
 
Habari ya Leo wanandugu, Naomba mnisaidie ushauri, Nilinunua calculator (CASIO FX-9750GII GRAPHING CALCULATOR) tarehe 3/1/2018 katika ebay, Ilikuwa inatoka Lithuania,Europe kuja Tanzania. Kutokana na tracking app ninayotumia (17track) Mzigo uliondoka tarehe 6/1/2018 kutoka ulaya. Tarehe 24/1/2018 mzigo ulifika Johanesburg International Mail Center, SouthAfrica (JIMC, ZAJNBA). Tangu siku hiyo mzigo haujatembea tena hadi leo (16/2/2018). Ila tarehe 6/2/2018 niliwasiliana na seller akaniambia kwamba nisubirie utafika tu. Nimesubiri wee nikaona hapana. Nikatuma email kwa JIMC hakuna majibu mpaka leo, Jana tar 15/2/2018 nikanunua kifurushi cha kimataifa niwapigie, nimepiga weee mpaka salio limeisha lakini hawakupokea. Inavyoonekana mzigo umetumwa kwa ems na Anwani ipo sahihi na destination inaonekana ni Tanzania. Naombeni ushauri nifanyaje?
 
Fungua kesi ebay, uwe refunded.
Niliagiza unyunyu kutoka marekani, baada ya mwezi kwenye tracking naona uko dubai haufiki bongo. Nikimcheki seller hajibu, nikafungua kesi ebay wakarefund baada kuona kweli seller kazingua
 







Nokia 6 nimeipata kwa 650000/=, Smart watch kwa 40000/=
Bei ya bongo ilinishinda simple like that...
mkuu vipi kodi baada ya mzigo kufika bongo walikutoza kiasi gani? na mzigo uliupokea kwa njia gani ?
 
Nenda equity bank na 10000/= pamoja na kitambulisho cha kura siku hiyo hiyo upewe kadi iliyo tayari kufanya manunuzi mtandaoni.
vipi equity bank hawaitaji barua za serikali ya mtaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…