Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Naona bora kutumia M-PESA mastercard kwa ajili ya malipo ya mtandaoni maana hata kama kuna refund unaipata moja kwa moja kwenye kadi yako na unaweza kuhamishia hiyo hela kwenda M-PESA moja kwa moja.
Equity card yao ni Visa Debit, kupokea refund moja kwa moja inakuwa ni ngumu sana kwa usalama wa ac yako wanavyodai. Kama card ya bank ni bora utafute hizi pre-paid card kama za Exim au BancABC hizo refund zinaingia moja kwa moja. Ila hata m-pesa virtual card ipo vizuri.
 
Hizo

Hizo update nimezipata na siyo kwamba nilikosea kujaza anuani yangu ila nilijaza vizuri kabisa. Nisaidieni mapema mzigo usije ukarudishwa ulikotika Kwa maana niliusubiria sana.
Ondoa shaka! Ni mara nyingi tracking system uonyesha hivo, wewe jiandae kwenda kuchukua mzigo wako tu.
 
msaada nimejaribu kufanya manunuzi ebay kwa mpesa mastercard vitu vya bei ndogo kwanza na nimefikia hapa je hiyo tracking number nitaipataje au ni baada ya mzigo kutumwa
 

Attachments

  • Screenshot_2019-05-23-12-18-22.png
    82.1 KB · Views: 58
Nimepokea mzigo wangu baada ya kwenda posta. Ila hawa watu Wa posta wana kauzembe fulani.
Hawako makini kwa maana kuna jamaa nimemkuta nikamwambia aniangalizie mzigo huo, akaangalia-angalia akasema kati ya mizigo iliyopo hakuna mzigo wa international. Nikamwonyesha tracking informations akasema nimsubiri Post master, yeye akaniuliza kama nimeshapigiwa Simu nikamwambia bado akaangalia angalia akasema mbona sioni kitu kama hicho nikakata tamaa ghafla akaniomba kitambulisho moyoni nikasema yap! Basi akanipa fomu kupokea mzigo nikajaza akanikabidhi mzigo. Nawashukuru walionishauri kwenda posta.

Sasa swali ni kwamba Kwa nini hawa jamaa wapokee mzigokisha wanakaa nao kimya?
 
Unge wauliza apo apo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…