Nimepokea mzigo wangu baada ya kwenda posta. Ila hawa watu Wa posta wana kauzembe fulani.
Hawako makini kwa maana kuna jamaa nimemkuta nikamwambia aniangalizie mzigo huo, akaangalia-angalia akasema kati ya mizigo iliyopo hakuna mzigo wa international. Nikamwonyesha tracking informations akasema nimsubiri Post master, yeye akaniuliza kama nimeshapigiwa Simu nikamwambia bado akaangalia angalia akasema mbona sioni kitu kama hicho nikakata tamaa ghafla akaniomba kitambulisho moyoni nikasema yap! Basi akanipa fomu kupokea mzigo nikajaza akanikabidhi mzigo. Nawashukuru walionishauri kwenda posta.
Sasa swali ni kwamba Kwa nini hawa jamaa wapokee mzigokisha wanakaa nao kimya?
View attachment 1106391