Jifunze kilimo cha nyanya

Nashukuru sana kiongozi, na je hii busterView attachment 698436 kipimo chake ni ml ngapi kwa solo la lt 20 msaada tafadhali
Huwaga wanaandika kwenye label yake... Na hapo ilipoandikwa sioni ila katika hili nadhan the horticulturist atatupa mwongozo, pia atuambie kama hii booster inafaa kuweka wakati mmea ukiwa mdogo au inafaa kutumika kama finisher!!
 
Hii unapiga mmea ukiwa shambani kabla haujaanza kutoa maua hivyo ni wa kukuzia tu,ikianza maua usipige hii yatadondoka yote
 
nyanya zinachukua miezi mitatu baada ya kupanda unaanza kuvuna

changamoto ya magonjwa sio kubwa sana ni kuwa makini tu shambani na kupiga dawa mapema kila unavyoona dalili za ugonjwa na zipo dawa za kuzuia wadudu kabla hawajaanza kushambulia mazao
embu nikuulize kwa nini dumila mnalima nyanya lakini hamziwekei nguzo ili mnyanya usimame na na hii itasaidia matunda ya nyanya kuwa hewani .kwa kufanya hivi sidhani kama kuna nyanya hata moja inaweza kuharibika

pili nahitaji kulima vitunguu mwaka huu muda gani ni muafaka? mbegu gani ni bora kati ya nyekundu au nyeupe na ipi bei yake huwa juu kuzidi nyingine?
 
embu nikuulize kwa nini dumila mnalima nyanya lakini hamziwekei nguzo ili mnyanya usimame na na hii itasaidia matunda ya nyanya kuwa hewani .kwa kufanya hivi sidhani kama kuna nyanya hata moja inaweza kuharibika
Sijui huko dumila wanalima nyanya gani ila kwa nnavyojua kuna nyanya fupi, za wastani na ndefu! sasa nyanya ndefu kama anna f1 hizi lazima uweke kamba au nguzo, na nyanya za wastani kama assila f1 pia lazima uweke nguzo maana zinarefuka sana, ila hizi nyanya fupi sio lazima uweke nguzo...
 
Piga hiyo label upande wa instructions nisome nikujuze au label haina instructions zozote???

hiyo sehem ya vegetables imeandikwa 1.0 - 1.5 L/Ha use approx 600 - 800 | water/ ha. Nimeshindwa kuelewa kabisa hapo japokua nimeenda kuulizia niliponunua wamenambia nipime mls 35 kwa solo moja
 
View attachment 700975View attachment 700976 hiyo sehem ya vegetables imeandikwa 1.0 - 1.5 L/Ha use approx 600 - 800 | water/ ha. Nimeshindwa kuelewa kabisa hapo japokua nimeenda kuulizia niliponunua wamenambia nipime mls 35 kwa solo moja

Hiyo ya hekta moja 1.0 liter igawanye kwa 2.5 upate kwa ekari moja,ni mls 400 kwa ekari. Sasa maji ni 600 kwa hekta hivyo ni 600/2.5=240
Hivyo kama maji ni 240 means ni solo za lita 20 zipatazo (240/20) 12
Dawa kwa ekari ni 400 gawanya kwa solo 12 ni (400/12)= 33 kwa solo la lita 20 so hata 35 sio mbaya sababu kuna ratio kubwa na ndogo hapo
 
Nashukuru sana kiongozi
 
Nataka kuwekeza katika secta ya Kilimo,wadau wa mwanza nijulisheni maeneo nayoweza kufungua Duka la pembejeo nikauza hizo inputs...... Asante
 
Wakuu ninasumbuliwa na ugonjwa wa mnyauko kwenye shamba langu la nyanya.
Msaada tafadhali. Nyanya ziko stage ya matunda

Wakuu ninasumbuliwa na ugonjwa wa mnyauko kwenye shamba langu la nyanya.
Msaada tafadhali. Nyanya ziko stage ya matunda

Kwa hapo itakua mnyauko bacteria au fungus,vipi kuna mtaalam wa kiliko karibu na wewe aje akutazamie ni upi haswa ili upate uhakika kwanza
 
Wakuu ninasumbuliwa na ugonjwa wa mnyauko kwenye shamba langu la nyanya.
Msaada tafadhali
Nyanya ziko stage ya matunda

Mkuu jaribu kupuliza copper oxychloride au copper hydroxide.

Baada ya mavuno usirudishe tena nyanya hapo, choma masalia yoote na panda vitunguu au zao jingine.
 
Mkuu jaribu kupuliza copper oxychloride au copper hydroxide.

Baada ya mavuno usirudishe tena nyanya hapo, choma masalia yoote na panda vitunguu au zao jingine.
Asante mkuu. Ngoja nitafute hiyo dawa madukani.
 
Wakuu ninasumbuliwa na ugonjwa wa mnyauko kwenye shamba langu la nyanya.
Msaada tafadhali
Nyanya ziko stage ya matunda

Huu ugonjwa huwaga unaambukiza mkuu, na ukizubaa utasambaa shamba zima!!

Sizan kama kuna dawa ila kama ukikosa dawa, ng'oa mimea yote iliharibika tupa mbali na shamba ikiwezekana choma moto!!
 
Hakuna mtaalamu wa kilimo hapa mkuu

Chukua glass nyeupe au kopo la kilimanjaro likate uchukue cha chini.
Weka maji nusu. Chukua eneo la shina la mche ulianza kukauka,kata na uweke kwenye maji ukiwa umening'ia usifike mpaka chini,kisha tazama kama utaona kuna ute ute mweupe unatoka chini ya hilo shina,ukitoka jua ni bacterial wilt usipotoa ni fusarium. Tazama leta majibu hapa nitakuelekeza cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…