Jifunze kilimo cha nyanya

Jifunze kilimo cha nyanya

NYANYA ni zao linalopendwa kutumiwa....kunogesha chakula, chakula kilichowekwa NYANYA huwa na radha nzuri inayomvutia mlaji
8abd5c2d5a678ccee53030d33702d3d4.jpg

Wakulima wengi hutamani kulima zao hili wengi huandika FAIDA na kusahau kujadili kuhusu HASARA zisababishwazo na kilimo cha zao hili.

6d8b4994ba24a2b378205b4e964f6e35.jpg

Kiukweli NYANYA inaweza ikakutoa ukafanikiwa ki maisha ila inaweza vile vile ikakupa hasara kubwa ukajuta kufanya kilimo cha zao hili.
50e4ae8e855e61b91d1907f5af0ca828.jpg

Andaa matuta vizuri lakini naomba nikwaMbie ndugu msomaji kila aina ya Tuta ina mahala pake na ardhi yake maalum hivyo ni bora kuichunguza ardhi yako vizuri maana kwa udongo wa kichanga ukiweka matuta ni dhahiri udongo utapelekwa na maji...kipindi cha kumwagilia.

e9f17163709b78b1b026c292755412aa.jpg

Zingatia nafasi katika upandaji wa zao hili la nyanya nafasi inayopendekezwa ni cm50 kutoka mche hadi mche mwingine .... usipande zao hili pasipo kufuata kanuni ya nafasi ya cm50 maana zao hili lina majani na ukipanda kwa kubananisha sana utasababisha joto kuzidi, vile vile matawi yakigusana kutoka mche mmoja kwenda mche mwingine unaweza kusababisha miche iambukizane magonjwa.
b4a1e3cc16e8ad7ea456c06797837e7b.jpg

Kwa kawaida zao hili huchukua siku 72 hadi 120 kupanda hadi kuanza kuvuna...
Zao la nyanya ni zao linalofyonza sana rutuba hivyo hakikisha ardhi unaiboresha kwa kuiweka mbole mara kwa mara...kwa mbolea za dukani Urea, dap, N.p.k, can na nyinginezo hakikisha unafuata maelekezo ya mtaalaam kabla ya kutumia hizo mbolea...mbolea ya Samadi au za mifugo hakikisha mbolea hizo ziwe zimekauka kabisa ziwe kama unga au kavu maana mbolea za mifugo zikiwa mbichi zitasababisha miche kuungua...na inaweza kudumaa pia.
7150f6744a80dee402843bbefbcd671b.jpg

Nyanya inashambuliwa sana na wadudu ambao hupelekea zao hili kupata magonjwa hivyo kabla hujapanda zao hili hakikisha unaanda shamba na kupiga dawa za wadudu pamoja na dawa za magonjwa za ukungu. Ni vigumu sana kutibu nyanya pindi utakapoanza kuona dalili kwenye mche ulioathiriwa na magonjwa. Hivyo kipindi chote cha uhai wa nyanya ni lazima kuzingatia matumizi ya dawa.
ca2f57debc94abbba252f182e284aa24.jpg

Endapo utagundua baadhi ya miche imepata maambukizi muone mtaalam wa madawa akushauri ukishindwa kuutibu ni bora ukaung'oa uo mche maana nayo huambukizana magonjwa kama tunavyoambukizana binaadam.
9837d975b574e846df9ae1c390193abe.jpg

Uhai wa nyanya unategemea Maji, Mbolea na Dawa japo baadhi ya wataalam hushauri kuongeza na busta...ila ndani ya baadhi ya hizi booster kuna kemikali inayozuru afya zetu...kama utaamua kutumia booster yoyote weka akilini kuwa ndani ya booster kuna kemikali...
Hivyo kwa ushauri wangu...ni bora mkulima ukatumia mbolea asilia, na maji....dawa usitumie mara kwa mara...
Tumia dawa wakati wa kuandaa shamba...
Tumia dawa kukinga magonjwa ya ukungu...
Tumia dawa kuangamiza wadudu waharibifu...
Tumia dawa kutibu miche iliyoathirika...
Ila dawa isitimike kwa kiwango kikubwa...na hakikisha unafata maelekezo ya dawa yaliyopo kwenye kibandiko.
eceb415d9ec4f6b0eb4786894ab9f747.jpg

Kama utaihudumia miche ya nyanya vizuri kwa kuweka mbole pindi inapohitajika, kumwagia maji japo kwa wiki mara tatu...na hakikisha siku za kumwagia unamwagia asubuhi na jioni...Nyanya inaweza kuanza kutoa Vitumba (maua) ndani ya wiki ya 5 hadi ya 6 tuu tokea ulipoipanda.
d3f406d0fa02d3a8d74bbf6109f8c683.jpg

Unapopuliza madawa kuwa makini sana maana kipindi ambacho nyanya imeanza kutoa maua ni kipindi ambacho nyanya inahitaji uangalizi wa hali ya juu wanaita (INTENSIVE CARE)...kuna baadhi ya dawa ni marufuku kabisa kugusa maua hayo kwani hukausha kabisa hayo maua....
2cd57fd8c143a8a84a1aebb70a29f26f.jpg

Zao hili lina faida sana ukinunua mbegu kutoka kwa wauzaji makini unaweza kupata zaidi ya kilo 5 kwa kila mche japo zipo mbegu zinazo zaa hadi kilo 12 na kuendelea...na zipo pia mbegu ambazo ukianza kuvuna na ukiihidumia vizuri unaweza kuvuna zaidi ya miezi 6 hadi mwaka.
2681922792c78397862e020d87762e35.jpg

Hasara kwenye kilimo cha nyanya mara nyingi husababishwa na uzembe....nasema ni uzembe kwasabu wengi tumejikuta tunakimbilia kilimo kwakuwa jirani amenunua pikipiki kwaajiri ya kilimo...na watu wengi husifia faida waliyopata pasipo kueleza na hasara walizopata....hivyo ukipiga dawa isiyosahihi upo uwezekano wa kuikosa miche yote....
Ukiweka mbolea vibaya upo uwezekano wa kuiunguza miche yote...
Usipo mwagia maji unaweza kuipoteza miche yote...
Usipo weka dawa kwa wakati unaweza kupoteza miche yote...hivyo ni jukumu letu wakulima kuzingatia uwekaji sahihi wa mbolea...kuzingatia uwekaji wa maji si lazima umwagie maji mengi eti ili kesho usimwagie mwagia majo kiasi cha kutosha ila usimwagie maji hadi matope yatapakae huku na huko...nyanya haihitaji maji kwa muda mrefu...itaoza....
Weka dawa kwa wakati...hapo utashinda na utapata faida ya uhakika....
Nimeona nichangie mawazo yangu juu ya kilimo hiki cha nyanya .....nakaribisha maoni
MuNgU akubariki sana.
vzr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu...tatizo huwa tunajisahau kwenye upuriziaji wa dawa...unatakiwa upige dawa kwa kubadilisha badilisha baadhi ya wadudu huwa wanajibadilisha kupambana na dawa...wakizoea dawa moja ni vigumu kuwamaliza....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hivi majani ya nyanya kuungua msimu wa mvua husababishwa na nini?
maji Yale ya mvua au kuna wadudu wanaoshambulia kipindi mvua ikianza?

Na dawa nzuri ya kuzuia kuungua ni ipi?
 
JIFUNZE KILIMO BORA CHA NYANYA

Utangulizi
Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalolimwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake.

Maeneo yanayolima nyanya
Inadhaniwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru au Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania mikoa inayolima nyanya kwa wingi hasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Iringa (Ilula), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.

tomatoes.jpg

Nyanya tayari kwa kuvuna


Mazingira yanayofaa kwa kilimo cha nyanya
Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa)

Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0.

Mwinuko: Nyanya hustawi vizuri kutoka sehemu za mwambao hadi kwenye mwinuko wa mita 400-1500 kutoka usawa wa bahari; yaani nyanda za chini kati hadi za juu kutoka usawa wa bahari. Nyanya zinazopandwa nyanda za juu sana hukumbwa na mvua za mara kwa mara ambazo huambatana na magonjwa ya jamii ya ukungu; kama Bakajani chelewa (Late Blight).

Aina za nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
  1. Aina ndefu (intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tengeru 97, Marglobe (M2009). Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
  2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)

Kulingana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawaili:
  1. OPV (Open Pollinated Variety) – Hizi ni aina za kawaida
  2. Hybrid – Chotara: Hizi ni nyanya zilizoboreshwa, aina hii zina mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
  3. Soma hapa mbegu bora mpya za mazao

Hata hivyo katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema. Nyanya zinazoonyesha kuwa na sifa ya kuhifadhika bila kuharibika mapema ni kama:

a) Tengeru’97 ambayo ina sifa vifuatazo:
  • Huzaa sana kutokana na wingi wa matunda na muda mrefu wa kuvuna, ambao hufikia michumo mikubwa kati ya 6-7 kuanzia kuvuna hadi mwisho wa mavuno.
  • Aina hii ina sifa ya kuwa na ganda gumu, hivyo haziharibiki haraka wakati wa kusafirisha au kuhifadhi (wastani wa siku 20)
  • Zina sifa ya kuvumilia baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa kunyauka
  • Tengeru’97 hustahimili mashambulizi ya minyoo fundo (Root knot nematodes)

b) Tanya
  • Sifa kubwa ya Tanya ni kwamba nayo huzaa sana
  • Huwa na ganda/ngozi ngumu ambayo inazuia kuoza au kuharibika kwa urahisi wakati wa kusafirisha au wakati wa kuhifadhi kwa muda mrefu.
  • Tanya nayo ina ladha nzuri inayopendelewa na walaji wengi

Zingatia: Tatizo la Tanya na T97 ni kwamba si kubwa sana kama marglobe 2009. Lakini ukubwa ni karibu unge karibiana, haujapishana sana. Kwa ujumla, ukubwa na wingi wa mazao hutegemea sana matunzo, udongo, hali ya hewa na mazingira kwa ujumla. Soma hapa mbegu bora mpya za mazao

Maandalizi ya Shamba la Nyanya
Shamba la nyanya liandaliwe mwezi mmoja au miwili kabla ya kupanda miche. Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya. Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya. Andaa mashimo ya nyanya kutegemeana na idadi ya miche uliyonayo, nafasi na aina ya nyanya. Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au zao litakalo changanywa na nyanya.

Jinsi ya kupanda miche ya nyanya
  • Weka samadi viganja viwili au gram 5 za mbolea ya kupandia kwenye shimo kabla ya kupanda mche.
  • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
  • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
  • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa kitaluni.
  • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kisha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Miche iliyopandikizwa shambani

Utunzaji wa zao la nyanya shambani
Umwagiliaji wa nyanya
Nyanya, kama ilivyo kwa mazao mengine, zinahitaji maji mengi ili kuzaa matunda yenye afya. Kutegemeana na aina ya udongo, unaweza kumwagilia nyanya mara mbili kwa wiki. Hakikisha unapanga ratiba maalum ya kumwagilia na unaifuata ili kuepuka kumwagilia kiholela holela kwani umwagiliaji usio na mpangilio huathiri afya ya matunda ya nyanya na kupelekea nyanya kuoza kitako (tomato blossom end rot). Unapotumia vifaa kama water can au mpira jitahidi sana usimwagilie kwenye majani ya mmea au matunda kwa sababu kulowesha mmea kunavutia wadudu na magonjwa ya ukungu unaoharibu nyanya.

Zingatia: usituamishe maji kwenye bustani au shamba la nyanya,

Palizi: Kudhibiti magugu
Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini. Palilia shamba lako wiki ya pili au ya tatu baada ya kupandikiza miche, lakini unaweza kupalilia kila unapoona magugu kwani shamba linatakiwa kuwa safi muda wote. Unaweza kuondoa magugu kwa kutumia dawa za kuua magugu au jembe la mkono. Magugu ni hatari kwa sababu tatu:

Kwanza: magugu yanashindana na mimea katika kuchukua nafasi na hivyo mimea kushindwa kujitanua. Pili: magugu huzuia mimea ya nyanya kupata mwanga wa jua wakutosha hivyo kuifanya mimea kushindwa kujitengenea chakula cha kutosha. Na tatu: magugu hushindana na mimea ya nyanya kufyonza virutubisho/chakula ardhini kitu ambacho kinapelekea mimea kuwa dhaifu. Pia magugu yanahifadhi wadudu na magonjwa na hivyo kuhatarisha zaidi usalama wa nyanya.

Mahitaji ya mbolea kwenye nyanya
  • Mbolea ya kupandia: weka mbolea ya DAP au Minjingu wakati wa kupandikiza miche shambani. Kiasi cha gram 5 ambayo ni sawa sawa na kifuniko kimoja cha soda kinatosha kwa kila shimo lenye mche mmoja. Tanguliza mbolea kwanza kwenye shimo kisha funika na udongo kiasi ili mbolea isigusane moja kwa moja na mizizi ya nyanya.
  • Mbolea ya kukuzia: unatakiwa kuongeza mbolea ya kukuzia kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche shambani. Mbolea hii ya iwekwe kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 kutoka kwenye shina. Kwa ajili ya kukuzia mimea ya nyanya tumia mbolea kama vile CAN, NPK, au SA. Tumia kifuniko kimoja cha soda kwa shina. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza.
Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, na pilipili hoho) inapaswa kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka.

Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya shambani (hasa usafi wa shamba na kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.

Kuweka matandazo
Matandazo ni nylon, majani au takataka za mimea zinazowekwa shambani au bustanini kwa lengo la kutunza unyevu na kuzuia au kupunguza kasi ya uotaji wa magugu, pia yakioza huongeza rutuba kwenye udongo. Mfano wa matandazo yanayoweza kutumika katika shamba la nyanya ni: nylon/turubai (plastic mulch), majani makavu, majani ya migomba, pumba za mazao, takataka za mbao. Plastic mulch inawekwa kabla ya kupandikiza miche shambani lakini matandazo mengine yawekwe baada ya kupandikiza miche. Na inafaa yawekwe kuzunguka eneo la shimo la mmea au katika shamba zima. Hivyo ni vizuri matandazo ya aina hii yawekwe mara tu baada ya kupandikiza (kama shamba halina magugu) au baada ya palizi ya kwanza.


Matandazo kwenye shamba la nyanya

Kupogolea matawi
Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.

Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji uegemezi, unashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.

Kupogolea majani
Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna.

Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche. Ondoa majani yote ambayo yana dalili za magonjwa, yaliyozeeka, yaliyobadilika rangi na kuwa njano au kuanza kukauka. Wakati wa utoaji majani kuwa makini kutojeruhi shina kwani maambukizi yanaweza kuanzia hapo.
  • Kumbuka: Matawi/majani ya chini ya mmea wowote huwa hayana msaada sana katika uzaaji wa matunda na zaidi ni kwamba kwa kiasi kikubwa yamepoteza uwezo wake wa kutengeneza chakula. Hivyo kuendelea kubaki kwake kutapunguza chakula ambacho kingeenda kuongeza wingi na kukuza ukubwa wa matunda.

Kusimikia miti (staking)
Nyanya ziwekewe miti/mambo ili kuzuia zisianguke au kutambaa kwenye udongo, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara mengi ya nyanya. Nyanya zinazotambaa zinahitaji kusaidiwa kuonyeshwa njia ili zisiguse chini. Nyanya zinapotambaa ardhini au kugusa chini zinaweza kuambukizwa wadudu na magonjwa ya ardhini kwa urahisi sana na pia wakati wa jua kali nyanya huchomwa na joto kali la ardhini. Hivyo basi shindilia mti mmoja (pigilia chini mambo) kando ya kila mmea wa nyanya na tumia kamba kufunga shina la mmea kwenye mti huo. Simika miti wiki mbili baada ya kupandikiza miche. Miti iwe imara na isiyooza haraka. Iwe na urefu wa mita moja hadi mbili na unene usiopungua sm 2.


Shamba la nyanya lililosimikwa mambo

Wadudu na Magonjwa hatari ya nyanya
Uvunaji wa nyanya
Vuna wakati nyanya zimekomaa lakini bado zina rangi ya kijani. Wakati wa kuvuna nyanya tenganisha tunda na kikonyo chake na sio kikonyo na shina ili kuepuka kuujeruhi mmea kitu ambacho kinaweza hurahisisha maambikizi ya magonjwa kwa mimea. Wakati mzuri wa kuvuna ni asubuhi na jioni. Inatakiwa nyanya ziwekwe kwenye vyombo vinavyopitisha hewa, na vyombo maarufu ni matenga. Matenga ya nyanya yanaweza kuwa yametengenezwa kwa mbao au mianzi.

Mara tu baada ya kuvuna/kuchuma nyanya inashauriwa zikusanywe chini ya kivuli kwa muda ili ziweze kutoa joto la shambani kabla ya kuzifungasha kwenye matenga.



Nyanya zinawekwa kwenye matenga

Namna ya kuhifadhi nyanya
Nyanya ni miongoni mwa mazao mepesi sana kuharibika hivyo ni muhimu sana nyanya zihifadhiwe mahali ambapo hapataharakisha kuoza kwake. Mahali pazuri ni pale penye ubaridi kiasi. Nyanya zenye ukijani zinaweza kuhifadhiwa mahali penye joto la 8o C hadi 10o C na zinaweza kukaa kwa muda wa hadi wiki tano bila kuharibika. Nyanya zilizoiva zinaweza kuhifadhiwa mahali penye kiasi cha joto cha 7o C na ni vizuri zaidi kama zitauzwa au kutumika mapema, yaani isizidi wiki moja. Katika mahali pakuhifadhia nyanya hali ya unyevu anga inatakiwa iwe ni kati ya 85% hadi 90%.

SOURCE: Kilimo Bora cha Nyanya | Mogriculture Tz

Ahsante sana mkuu nimepata kitu
 
Fupi inakaa miezi mitatu inakua imeisha inatoa nyanya juu kwenye kichwa cha mche,mavuno unavuna mengi kwa wakati mfupi sababu kila shina linaachwa hivyo ikiwa na mashine manne inamaana ni zaidi ya kg 2 utavuna kwa wiki kwa kila mmea,mmea mfupi mpaka kuisha chotara nyingi ni kg 10 kwa mche mmoja ila za kienyeji fupi ni kg 2 mpaka 3 kwa mche mmoja.


Ndefu hazina mwisho wa kukua hivyo uvunwa sita mpaka nane na hata zaidi kutegemea na huduma yako,ndefu hukupa wastani wa chini kg 20 kwa shina moja ila uvunaji wake kila wiki ni kichane kimoja ambacho mara nyingi huwa kg 1
Mzee msaada number zako nataka nilime nyanya mwezi huu
 
Huo mchanganyiko unapoteza mbolea nyingi sana dap ina nitrate,can ina nitrate na kwenye npk kuna nitrate. Madhara ya nitrate ikizidi ni mmea unakua haraka sana but unazalia juu sana na matunda hafifu. Pia dap inapaswa iwekwe kabla ya kupanda ukichelewa ni siku unapanda sababu phosphate ni madini yanayotolewa taratibu na yanasafiri taratibu pia yanahitaji mapema sana ili ikuze mizizi,ukiweka dap mapema hata mimea mingi kufa itapungua sababu inahitaji chakula pale inapohamishwa.

Kuepuka huo mchanganyiko bora utumie otesha inamadini yote hayo maana ina npk
Msaada number yako tukikwama tukutafte
 
Mm ni mkulima wa nyanya na mpunga kijiji cha mbigili,dumila mkoani morogoro
wakulima wenzangu wa nyanya tubadilishe uzoefu kilimo cha nyanya kuhusu mbegu,mbolea,magonjwa,madawa na masoko
karibuni sn
56cf2ca6970ba3ac157c53c37b1085ec.jpg
0ab7cb4ef777665dcd561f3fd8542a25.jpg
d5bdacda633cb03c38ae62bd31849565.jpg
f049f2f4fc7fda2d32ffc798a38732dc.jpg
66bdd58d14c0705288cea0e4e9f8c4f7.jpg
Huu uzi nimeusomaa kwa siku 4 aiseeeee....Nyanya Ninyanyue tu uwezi ninyanyasa.......january naingiaaaa shambani rasmi tukutane sokoni march
 
Mm ni mkulima wa nyanya na mpunga kijiji cha mbigili,dumila mkoani morogoro
wakulima wenzangu wa nyanya tubadilishe uzoefu kilimo cha nyanya kuhusu mbegu,mbolea,magonjwa,madawa na masoko
karibuni sn
56cf2ca6970ba3ac157c53c37b1085ec.jpg
0ab7cb4ef777665dcd561f3fd8542a25.jpg
d5bdacda633cb03c38ae62bd31849565.jpg
f049f2f4fc7fda2d32ffc798a38732dc.jpg
66bdd58d14c0705288cea0e4e9f8c4f7.jpg
naomba kama inawezekana unitumie hilo kopo la mbegu za assila na namna nzur ya kusiha.
 
Back
Top Bottom