Jifunze kilimo cha nyanya

ndomana uwa nawashauri watu ni bora usilime kabisa kuliko kulima mbegu za kawaida maana tofauti yake ni bei ya mbegu tu Huduma zote ni sawa

tukija kwenye mavuno utajilaumu kwanini ulipanda mbegu za kawaida.
 

Samahani mkuu, hizo 2-3m unaweza kunipa mchanganuo wake?
Kwa mfano, mimi nina shamba na liko safi tayari. Maji nimeshachimba kisima na kiko tayari, ni suala la kupandisha maji kwenye tank tuu na kumwagilia. Je, kuanzia kulima shamba, kuandaa matuta na kuendelea mpaka kuvuna itafika hiyon 2m?
 
Habari Wadau.

Bajeti ya millioni moja haiwezi ikatosha mdau kulima ekari moja? Eneo unapolima wewe ekari moja unakodi kwa bei gani?
Na mbegu za muda mfupi unavuna baada ya mda gani? Unaweza ukapanda nyanya mara mbili au tatu kwa mwaka? Yaani ukivuna ulime tena? Yeyote anayejua naomba anisaidie mawazo. Shukrani.
 
Sio milioni moja hata laki 5 unaweza kulima nyanya ukanunua mbegu za kawaida, mbolea unaweza ukuweka au usiweke madawa utapiga kidogo kwa kulipua. kwakifupi hakuna utakachopata zaidi ya kupoteza muda

Ukitaka kulima vzr kwa uhakika wa mbegu bora, mbegu peke yake anafika laki 5 bado mbolea na madawa na hao vibarua watakaopanda itabidi uwalipe, wachimba mashimo nao walipwe, wapiga dawa nao walipwe

Bora ujipange ufanye kazi ya uhakika.
 
hakuna mbegu ya muda mfupi wala ya muda mrefu, mbegu zote ni miezi mitatu unaanza kuvuna

mbegu ya kawaida na ya kisasa tofauti ni bei tu mambo mengine yote ni sawa
 
mkuu inahitaji muda sn kuandaa huo mchanganuo wake wa kulima nyanya bado kuna gharama zengine huwezi kuzipanga, hatujui nyanya zitashambuliwa na ugonjwa gani na utapiga dawa gani

sawa una shamba je linafaa kupanda nyanya? udongo wake upoje? alafu shamba wala halina gharama hata upewe shamba la bure bado mbegu utanunua, bado utalima kwa trekta, utapiga shimo, utapanda, utaweka mbolea, utarudishia, utapiga madawa kwakifupi huwezi kuzikimbia gharama
 
Kwenye swala la kumwagilia vp changamoto zake?
 
Kwenye swala la kumwagilia vp changamoto zake?
bila kuona shamba na bila kujua unapanda nyanya wakati gani siwezi kujua changamoto zake

ipo hivi ukipanda nyanya wakati wa mvua huna haja ya kumwagilia, na nyanya inahitaji maji wakati wa kupanda ikishashika haina haja ya maji labda shamba liwe kavu sn

kwenye kilimo ukifika shamba ndio unajua kila kitu lakini bila kuona shamba inakua ngumu kujua changamoto zake
 
Mkuu kwa mara yakwanza nimeshuhudia nyanya ya asila aise nibonge la nyanya
Je siwezi kuchukua nyanya zake kisha niakaotesha vip matokeo yake
Gram 10 ya asila inaweza toa miche mingapi?
Mahahaha mkuu mbegu zote za kisasa hazikamuliwi kuhusu miche ngumu kujua idadi Ila ni michache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…