petro matei
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 803
- 937
Naombe msaada kujua ubora wa mbegu ya nyanya Rio grand
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si zaid ya laki 5Mkuu hivi nikilima kipindi gani nitavuna kipindi nyanya sio nyingi sokoni, na nikitumia drip irigation kulima enea la bustani la nyumbani la mita 30 kwa 30,itanigharimu shilingi ngapi kuweka mfumo wa umwagiliaji wa drip.
ubora wa mbegu unategemea na shamba na Huduma, Ila ni ya kawaida tu tofauti na mbegu za kisasaNaombe msaada kujua ubora wa mbegu ya nyanya Rio grand
Mkuu mavuno ya nyanya yapo hivi,
sisi tunauza kwa box, na tunavuna kila wiki.
Sasa ule mchumo wa kwanza tunaita fundisha, sasa mfano mchumo wa kwanza ukichuma box 20 utaangalia na bei itakavyokuwa sokoni mfano ikiwa 10000 utapata 200,000/=
Utakuja mchumo wa pili box zinaongeza unaweza kupata box 60 pia utazidisha kwa bei iliyopo sokoni au tufanye ile ile 10000 utapata 600,000/=
mchumo wa tatu unaweza kupata box 120 pia utazidisha kwa bei
mchumo wa 4 utaweza kupata box 180 pia utazidisha kwa bei
mchumo wa 5 unaweza kupata box 240 utazidisha kwa bei,
baada ya hapo nyanya nitaanza kupungua mchumo unaofata zitarudi 180 alafu 120 alafu 60 mwisho 20 biashara imeisha
utajumlisha kila mchumo umepata bei gani utatoa na gharama ulizotumia
hizo bei ni mfano zinaweza kuzidi au kupungua
mkuu mavuno ya nyanya yapo hivi,
sisi tunauza kwa box, na tunavuna kila wiki.
sasa ule mchumo wa kwanza tunaita fundisha, sasa mfano mchumo wa kwanza ukichuma box 20 utaangalia na bei itakavyokuwa sokoni mfano ikiwa 10000 utapata 200,000/=
utakuja mchumo wa pili box zinaongeza unaweza kupata box 60 pia utazidisha kwa bei iliyopo sokoni au tufanye ile ile 10000 utapata 600,000/=
mchumo wa tatu unaweza kupata box 120 pia utazidisha kwa bei
mchumo wa 4 utaweza kupata box 180 pia utazidisha kwa bei
mchumo wa 5 unaweza kupata box 240 utazidisha kwa bei,
baada ya hapo nyanya nitaanza kupungua mchumo unaofata zitarudi 180 alafu 120 alafu 60 mwisho 20 biashara imeisha
utajumlisha kila mchumo umepata bei gani utatoa na gharama ulizotumia
hizo bei ni mfano zinaweza kuzidi au kupungua
Mbolea ni lazima, kuna mbolea za chini za kupandia na kukuzia ukishapanda miche shambaniTUNASHUKURU SANA KWA ELIMU KUBWA, NAOMBA KUFANHAMU KAMA UNATUMIA PIA SAMADI KATIKA KUPANDA HIYO MICHE YA NYANYA.
Hayo ni makadirio, itategemea ubora wa shamba,huduma na mbegu utakayotumia kupata hizo boksiTUKISHUSHA HESABU MAMBO YATAKUWA HIVI
20 10,000 200,000
60 10,000 600,000
120 10,000 1,200,000
180 10,000 1,800,000
240 10,000 2,400,000
180 10,000 1,800,000
120 10,000 1,200,000
60 10,000 600,000
20 10,000 200,000
10,000,000 hii ni jumla ya mauzo ya michumo yote
lakini kazi hii inatakiwa kujitoa sana, mda wa kutosha, pesa na weledi.
Ni mbegu ya kawaida tuHabari wanajamvi, nimelima nyanya msimu huu na nimepanda mbegu inaitwa Mwanga, naomba kujuzwa ubora wake kwa anaye ifahamu.
Ni mbegu ya kawaida tu
Ubora itategemea na shamba lako, mbegu na huduma
Ubora wa shamba ni udongo, kila zao na udongo wake kuna udongo mzuri wa nyanya. Ukiwa na shamba lenye udongo mzuri kinachofata umelilimaje? Yani ulisafishe vzr alafu ulime kwa trekta baada ya hapo upige shimo vzrShamba bora la nyanya linatakiwa liweje mkuu? Au pale unaposema ubora itategemea na shamba langu unakuwa na maana gani?
Kwa sasa 140 asila 10gMbeya assila gramu 10 ni 130k
Ubora wa shamba ni udongo, kila zao na udongo wake kuna udongo mzuri wa nyanya
Ukiwa na shamba lenye udongo mzuri kinachofata umelilimaje? Yani ulisafishe vzr alafu ulime kwa trekta baada ya hapo upige shimo vzr
Kwakifupi huo ndio ubora wa shamba
Kwa sasa 140 asila 10g
Shukrani kwa Jibu zuri, na pia usinichoke kwa kuwa nina lengo la kujua na kufanikiwa zaidi katika kilimo cha nyanya, Hapo kwenye udongo ni udongo gani ndio unafaa zaidi kwa kilimo cha nyanya?
Nyanya inafanya vzr kulimwa kwenye udongo wa mfinyanzi na tifutifu, nyanya haifanyi vzr kwenye udongo wenye kichangaShukrani kwa Jibu zuri, na pia usinichoke kwa kuwa nina lengo la kujua na kufanikiwa zaidi katika kilimo cha nyanya, Hapo kwenye udongo ni udongo gani ndio unafaa zaidi kwa kilimo cha nyanya?
Kwa kiswahili tuna kichanga,mfinyanzi na tifutifu ambapo ni sawa na kusema sand,clay and silt kwa lugha ya kigeni sasa kuna udongo unaitwa loamy soil huo ndio unafaa zaidi kwa kilimo lakini sasa kiswahili chake sikifahamu vyema ila kwa ufupi unakua na mchanganyiko mchanga, tifutifu na mfinyanzi haujapishana sana na udongo wa msituni ukinyesha maji yanakaa ila si kama mfinyanzi na hayapotei kama kichanga kilivyo,kwa kua unasifa ya mfinyanzi basi pia unauwezo wa kuzuia madini mengi hivyo unakua na madini pia na hata ukiweka mbolea unaona kweli imefanya kazi, pia sio mgumu umejiachia kama tifutifu ila haupotezwi kwa upepo.
Pendelea sana kumwaga samadi shambani kwako na hata mazao ukivuna yalimie humo huko na trekta inafaida sana ya kutunza ardhi yako na kuiboresha kua loamy soil
Nyanya inafanya vzr kulimwa kwenye udongo wa mfinyanzi na tifutifu, nyanya haifanyi vzr kwenye udongo wenye kichanga
Na ikiwa shamba lako lina kichanga basi unatakiwa upige shimo lefu kwenda chini hadi uupate udongo mweusi
Madhara ya kulima nyanya kwenye kichanga nyanya hazizai sn na zinawahi kuisha yani unaweza kuchuma mara tatu ukakuta nyanya zimeisha shambani