Hongereni wakulima wa nyanya, nimeona first page mambo ya mbegu naomba nichangie,
Ukulima nyanya hybrid/chotara au unalima za kawaida/opv tambua huduma zake ni sawa yaani kiasi cha dawa, mbolea,maji,muda wa palizi,vibarua,shamba kama la kukodi bei ni ile ile tofauti iliyopo kati ya kutumia mbegu chotara na mbegu ya kawaida ni mosi bei mbegu chotara ghali kuliko za kawaida na pili mavuno mbegu chotara ina mavuno mengi sana kuliko za kawaida na other advantage chotara inauvumilivu wa magonjwa kuliko za kawaida.
Huwa iko hivi kulima nyanya ya faida kwa asilimia Mia moja za mavuno basi asilimia 10 inatoka kwenye mbegu na asilimia 90 inatoka kwenye huduma. Hivyo unapoona mbegu chotara ghali ukanunua za kawaida tambua umeshajiandaa kupata hasara sababu huduma ni the same.
Tuondoke kwenye kulinganishiana maeneo yaani alielima pakubwa ndio mkulima lah tuje kwenye kulima eneo ambalo unaweza kuhudumia vyema na unapata mavuno bora basi utafanikiwa.
Kama unalima let's say jarrah rz unapata crate 1000 kwa ekari (ndio uzao wake) na mwingine analima rio grand akapata crate 200 kwa ekari na muda Huo Huo uduma sawa sawa kote basi alielima jarrah atapata faida hata kama nyanya itauzwa elf 10 kwa crate na alielima rio grand atapata hasara hata crate likiuzwa elf 40