Jifunze kilimo cha nyanya

Jifunze kilimo cha nyanya

Hongereni wakulima wa nyanya, nimeona first page mambo ya mbegu naomba nichangie;

Ukulima nyanya hybrid/chotara au unalima za kawaida/opv tambua huduma zake ni sawa yaani kiasi cha dawa, mbolea,maji,muda wa palizi,vibarua,shamba kama la kukodi bei ni ile ile tofauti iliyopo kati ya kutumia mbegu chotara na mbegu ya kawaida ni mosi bei mbegu chotara ghali kuliko za kawaida na pili mavuno mbegu chotara ina mavuno mengi sana kuliko za kawaida na other advantage chotara inauvumilivu wa magonjwa kuliko za kawaida.

Huwa iko hivi kulima nyanya ya faida kwa asilimia Mia moja za mavuno basi asilimia 10 inatoka kwenye mbegu na asilimia 90 inatoka kwenye huduma. Hivyo unapoona mbegu chotara ghali ukanunua za kawaida tambua umeshajiandaa kupata hasara sababu huduma ni the same.

Tuondoke kwenye kulinganishiana maeneo yaani alielima pakubwa ndio mkulima lah tuje kwenye kulima eneo ambalo unaweza kuhudumia vyema na unapata mavuno bora basi utafanikiwa.

Kama unalima let's say jarrah rz unapata crate 1000 kwa ekari (ndio uzao wake) na mwingine analima rio grand akapata crate 200 kwa ekari na muda Huo Huo uduma sawa sawa kote basi alielima jarrah atapata faida hata kama nyanya itauzwa elf 10 kwa crate na alielima rio grand atapata hasara hata crate likiuzwa elf 40
ndomana uwa nawashauri watu ni bora usilime kabisa kuliko kulima mbegu za kawaida maana tofauti yake ni bei ya mbegu tu Huduma zote ni sawa

tukija kwenye mavuno utajilaumu kwanini ulipanda mbegu za kawaida.
 
41e8d86778c6eaf81b0dec12b426b4a2.jpg

nilitumia hii
Bei?asante
 
tunauza kwa box sio kwa kilo, unapata box nyingi kama utalima kwenye shamba zuri na utahudumia vzr

Heka moja inaweza kugharimu mil 2-3 itategemea na changamoto za magonjwa na madawa kadri inavyojitokeza

faida itategemea na bei Ila ikianzia 10000 tu unapata faida, sababu inatoa box nyingi na unavuna sn
ukianza kuchuma unachuma kila wiki sasa hizi nyanya zina michumi mingi inafika hadi michumo 9

Samahani mkuu, hizo 2-3m unaweza kunipa mchanganuo wake?
Kwa mfano, mimi nina shamba na liko safi tayari. Maji nimeshachimba kisima na kiko tayari, ni suala la kupandisha maji kwenye tank tuu na kumwagilia. Je, kuanzia kulima shamba, kuandaa matuta na kuendelea mpaka kuvuna itafika hiyon 2m?
 
Habari Wadau.

Bajeti ya millioni moja haiwezi ikatosha mdau kulima ekari moja? Eneo unapolima wewe ekari moja unakodi kwa bei gani?
Na mbegu za muda mfupi unavuna baada ya mda gani? Unaweza ukapanda nyanya mara mbili au tatu kwa mwaka? Yaani ukivuna ulime tena? Yeyote anayejua naomba anisaidie mawazo. Shukrani.
 
Habari Wadau.
Bajeti ya millioni moja haiwezi ikatosha mdau kulima ekari moja? Eneo unapolima wewe ekari moja unakodi kwa bei gani?
Na mbegu za muda mfupi unavuna baada ya mda gani? Unaweza ukapanda nyanya mara mbili au tatu kwa mwaka? Yaani ukivuna ulime tena? Yeyote anayejua naomba anisaidie mawazo.

Shukrani.
Sio milioni moja hata laki 5 unaweza kulima nyanya ukanunua mbegu za kawaida, mbolea unaweza ukuweka au usiweke madawa utapiga kidogo kwa kulipua. kwakifupi hakuna utakachopata zaidi ya kupoteza muda

Ukitaka kulima vzr kwa uhakika wa mbegu bora, mbegu peke yake anafika laki 5 bado mbolea na madawa na hao vibarua watakaopanda itabidi uwalipe, wachimba mashimo nao walipwe, wapiga dawa nao walipwe

Bora ujipange ufanye kazi ya uhakika.
 
Habari Wadau.

Bajeti ya millioni moja haiwezi ikatosha mdau kulima ekari moja? Eneo unapolima wewe ekari moja unakodi kwa bei gani?
Na mbegu za muda mfupi unavuna baada ya mda gani? Unaweza ukapanda nyanya mara mbili au tatu kwa mwaka? Yaani ukivuna ulime tena? Yeyote anayejua naomba anisaidie mawazo. Shukrani.
hakuna mbegu ya muda mfupi wala ya muda mrefu, mbegu zote ni miezi mitatu unaanza kuvuna

mbegu ya kawaida na ya kisasa tofauti ni bei tu mambo mengine yote ni sawa
 
Samahani mkuu, hizo 2-3m unaweza kunipa mchanganuo wake?
Kwa mfano, mimi nina shamba na liko safi tayari. Maji nimeshachimba kisima na kiko tayari, ni suala la kupandisha maji kwenye tank tuu na kumwagilia. Je, kuanzia kulima shamba, kuandaa matuta na kuendelea mpaka kuvuna itafika hiyon 2m?
mkuu inahitaji muda sn kuandaa huo mchanganuo wake wa kulima nyanya bado kuna gharama zengine huwezi kuzipanga, hatujui nyanya zitashambuliwa na ugonjwa gani na utapiga dawa gani

sawa una shamba je linafaa kupanda nyanya? udongo wake upoje? alafu shamba wala halina gharama hata upewe shamba la bure bado mbegu utanunua, bado utalima kwa trekta, utapiga shimo, utapanda, utaweka mbolea, utarudishia, utapiga madawa kwakifupi huwezi kuzikimbia gharama
 
sio milioni moja hata laki 5 unaweza kulima nyanya ukanunua mbegu za kawaida, mbolea unaweza ukuweka au usiweke madawa utapiga kidogo kwa kulipua kwakifupi hakuna utakachopata zaidi ya kupoteza muda. Ukitaka kulima vzr kwa uhakika wa mbegu bora, mbegu peke yake anafika laki 5 bado mbolea na madawa na hao vibarua watakaopanda itabidi uwalipe, wachimba mashimo nao walipwe, wapiga dawa nao walipwe.

Bora ujipange ufanye kazi ya uhakika
Kwenye swala la kumwagilia vp changamoto zake?
 
Kwenye swala la kumwagilia vp changamoto zake?
bila kuona shamba na bila kujua unapanda nyanya wakati gani siwezi kujua changamoto zake

ipo hivi ukipanda nyanya wakati wa mvua huna haja ya kumwagilia, na nyanya inahitaji maji wakati wa kupanda ikishashika haina haja ya maji labda shamba liwe kavu sn

kwenye kilimo ukifika shamba ndio unajua kila kitu lakini bila kuona shamba inakua ngumu kujua changamoto zake
 
Mkuu kwa mara yakwanza nimeshuhudia nyanya ya asila aise nibonge la nyanya
Je siwezi kuchukua nyanya zake kisha niakaotesha vip matokeo yake
Gram 10 ya asila inaweza toa miche mingapi?
Mahahaha mkuu mbegu zote za kisasa hazikamuliwi kuhusu miche ngumu kujua idadi Ila ni michache
 
Back
Top Bottom