Jifunze kilimo cha nyanya

Jifunze kilimo cha nyanya

Hongera aisee...Hii Assila ni mbegu nzur sana mno,nilishawahi kuipanda na inazaa sana,niliwahi kujaribu kupanda ndani ya heka mbili tuliweka Assila,Anna F1,Kipato .Zilianza vizur tukavuna kidogo ila changamoto ya ukame ikatukabili..tulikua tunategemea mto! ila nilijifunza kitu.
kweli kabisa mkuu assila inataka maji mengi inazaa sana alafu matunda yake makubwa
 
kweli kabisa mkuu assila inataka maji mengi inazaa sana alafu matunda yake makubwa
Sure! je ningependa kujua ulilima kwa kutegemea mto,mvua,au kisima? na haya mavuno ni ya kipindi hiki? nasikia hapa kati nyanya zilipanda bei! am sure umetusua best..
 
Sure! je ningependa kujua ulilima kwa kutegemea mto,mvua,au kisima? na haya mavuno ni ya kipindi hiki? nasikia hapa kati nyanya zilipanda bei! am sure umetusua best..
moro tunategemea mto na visima

haya mavuno sio ya msimu huu mkuu
 
Ka mkubwa.... izo nyanya zoote umevuna kwenye eneo la ukubwa gani... au matuta managap ya ukubwa gan....
 
Asilla ni mbegu nzuri hata mbeya inafanya vizuri...kipato inazaa tena matunda makubwa ila inashambuliwa sana na magonjwa,imara f1 ni nzuri pia sema haitaki stress kbs na inazaa sana .....
 
Hongereni wakulima wa nyanya, nimeona first page mambo ya mbegu naomba nichangie.

Ukulima nyanya hybrid/chotara au unalima za kawaida/opv, tambua huduma zake ni sawa, yaani kiasi cha dawa, mbolea, maji, muda wa palizi, vibarua, shamba kama la kukodi bei ni ile ile tofauti iliyopo kati ya kutumia mbegu chotara na mbegu ya kawaida ni mosi bei mbegu chotara ghali kuliko za kawaida na pili mavuno mbegu chotara ina mavuno mengi sana kuliko za kawaida na other advantage chotara inauvumilivu wa magonjwa kuliko za kawaida.

Huwa iko hivi kulima nyanya ya faida kwa asilimia Mia moja za mavuno basi asilimia 10 inatoka kwenye mbegu na asilimia 90 inatoka kwenye huduma. Hivyo unapoona mbegu chotara ghali ukanunua za kawaida tambua umeshajiandaa kupata hasara sababu huduma ni the same.

Tuondoke kwenye kulinganishiana maeneo yaani alielima pakubwa ndiyo mkulima, la! tuje kwenye kulima eneo ambalo unaweza kuhudumia vyema na unapata mavuno bora basi utafanikiwa.

Kama unalima let's say jarrah rz unapata crate 1000 kwa ekari (ndio uzao wake) na mwingine analima rio grand akapata crate 200 kwa ekari na muda Huo Huo uduma sawa sawa kote basi alielima jarrah atapata faida hata kama nyanya itauzwa elf 10 kwa crate na alielima rio grand atapata hasara hata crate likiuzwa elfu 40.
 
Kantangaze unatumia dawa gani kumdhibiti?

Nilitumia hii

41e8d86778c6eaf81b0dec12b426b4a2.jpg
 
Back
Top Bottom