Jifunze kilimo cha nyanya

Jifunze kilimo cha nyanya

naomba kujuzwa hili ni tatizo gani?

IMG_20211207_132025_111.jpg
 
Hivi ni aina gani ya ukungu huzuia vizuri kati ya linkmil, farmerzeb au nyingine tofauti
Mosi naona haukupandia mbolea yaani hukuweka DAP sababu hutupa phosphate ya kukuza mizizi na ammonium ya kutupa nitrate itupe rangi ya majani na shina lenye afya. Pia baada ya siku tatu huwa tunaishtua na CAN ili iendelee kulipa shina afya zaidi.

Pili baada ya kupanda hukupiga dawa za ukungu,huwa tunachanganya ridomil gold gm 20 kwa lita 20 za maji kisha unanyesha kwenye shina la mmea,hii husaidia kuzuia fungus kushambulia shina la mmea wako

Tatu ulipandikiza zaidi ukavuka kiwango ambacho kilikua kwenye kitalu,hivyo udongo ukagusa shina la kijani changa la mmea hii hulea tatizo la soft rot,haina dawa huwa tunaikinga kwa kupanda usawa ule ule uliokua kitaluni na pia kwa kupiga ridomil gold. Tafuta miche mingine ya kujazia sababu tiba hapo hakuna.
Ahsante
 
Sasa wakuu nipende kuwauliza jambo langu.

Kwa morogoro mashamba wanakodishaje nikimaanisha bei.

Na je vipi wanalima msimu wa mwezi wa 10, 11, 12 ili wavune kuanzia december na January kuendelea.?
 
Aisee kama bado group la nyanya mpo tafadhali niunge 0755404226
 
Back
Top Bottom