Namuchi braver
Member
- Nov 16, 2020
- 54
- 84
Vijana wengi tunaona maisha magumu sana sio kwamba hatujitumi, hapana. Ila shida ni kutaka kujilinganisha na mafanikio ya watu waliokizi umri wa utafutaji, ingawa pia wapo tunajilinganisha na rika letu, hata hivyo tunasahau historia au hali ya uchumi wa familia zao
Ninachoamini kipi? Kwangu naamini ili kufikia hatua fulani katika maisha ni lazima upitie hatua nyingi ndogo ili kufikia pakubw. Ina maana kwamba kuanza kufanya jambo kidogo kidogo mpaka kufikia lengo.
Usitamani au kutaka kuwa na gari pamoja na nyumba kwa pamoja kwa kipindi hicho ukijifananisha na mjomba au watu waliokuzidi umri kwani hata wao hawakupata katika umri wako kwa sababu nyingi zinazotutofautisha.
Hivyo vitu vyote vinahitajika, ila jiulize mzazi wako alipata vitu hivyo kwenye umri wako? Kama jibu hapan basi anza taratibu tutafikia walipo fikia wakubwa zetu na kuwazid pia.
Asante sana wakuu