Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 31,913
- 65,514
NAKUSHAURI
Watu wengi mnajinyima furaha, watu wengi pale mnapotakiwa kulia hamtaki kulia, pale mnapotakiwa kufurahia hamtaki kufurahia. Watu wengi mnakufa kwa maumivu makubwa ya moyo.
Ngoja nikufundishe kitu.
Siku ukifiwa na mtu unayempenda, lia sana, tena lia kuliko wote ikiwezekana. Usisubiri kulia baadaye, unapokaa na maumivu moyoni na hukukitoa kilio chako, ndugu yangu nakwambia tu kuna siku utajuta kwa nini hukulia kipindi hicho.
Jambo limetokea na kukufurahisha, ndugu yangu furahi, usiwe mnafiki hata kidogo, kwenye furaha usiangalie nani atakasirika kisa mimi nafurahi, nani ataumia kisa mimi nafurahi.
Hapa dunia umezaliwa peke yako, huzaliwa na mtu, hata kama ni mapacha, bado ulitoka tumboni peke yako, inapotokea unafanya jambo halafu watu kukereka, wewe fanya mpaka furaha yako itakapofika kikomo.
Watu wengi walijuta, utasikia yeye alipokutwa na mabaya mimi sikumcheka ila nilipokutwa mimi, alinicheka. Bro! Hakuna mtu anayejali furaha yako, anakuna mtu anayejali maumivu yako. Jipe furaha wewe mwenyewe, kwa nini ufe ukiwa na maumivu ya kutokuonyesha furaha kipindi ulitakiwa kuionyesha?
Mwingine leo hafurahi Yanga kukosa kombe, siku ikitokea Simba naye akikosa, mtu akifurahi ataanza kusema mimi mbona kipindi kile sikukucheka? Sasa kwani ulikatazwa kumcheka? Bro! Cheka leo, si kila siku utakwenda kucheka, kuna kipindi utakuja kulia.
Leo furaha yako unaiweka moyoni, wenzako kikifika kipindi cha kucheka furaha zao hawatoziweka moyoni, watakucheka mpaka utakasirika, na wengine wanaweza hata kujiua kisa alichekwa sana.
Bro! Amini kwenye furaha yako. Kuna mtu anaumia kisa wewe umefurahia, achana nao, mind your own business kwa kuwa hapa duniani hujaletwa kumchekesha kila mtu, hujaletwa kumfurahisha kila mtu.
Linapokuja suala la furaha, furahia kiasi kwamba kila mtu akikuangalia aseme kweli jamaa amefurahia. Linapotokea suala la kuhuzunika mpaka kulia, wewe huzunika na ulie sana mpaka watu waseme kweli jamaa ameumizwa.
Furaha yako ya leo usiifiche, kuna siku itakuja utajuta kwa nini leo hujafurahi na dunia nzima ijue kama umefurahi. Unapopata furaha ama huzuni halafu hufurahi ama kulia, moyo unahifadhi vitu, unahifadhi mambo mengi na mwisho wa siku msongo wa mawazo unakushika.
Hujawahi kumsikia mtu alitakiwa kusema jambo fulani, hakusema na mwisho wa siku akasema nasikia kuna donge zito moyoni ila nimeshindwa kulitoa wakati fulani akiwa hai. Unataka kumcheka mtu kisa amefungwa, mcheke tena sana tu kwa sababu kitakuja kipindi yeye atakucheka sana kwa ajili ya kuiponya roho yake.
Tunajiua kwa sababu ya huruma, tunajiua kwa sababu ya huu ujinga wa kuficha furaha na huzuni zetu. Majirani wametuwekea limitation kwamba hutakiwi kufanya hivi na vile kwa ajili yao, lakini wao mwisho wa siku wanakuja kufanya bila kujali hisia zako.
Bro na sista, kama umefurahi, ionyeshe dunia kwamba umefurahi, hapo unaiponya roho yako bila kujua. Usipofanya hivyo, kuna mwaka utakuja kujilaumu kwa nini hukuionyesha dunia kama umefurahi leo.
Ushauri kutoka kwa kaka yako!!