Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Nianze na salamu za mwaka huu wa 2024 kwa wanajukwaa wote,nilibanwa kidogo na shughuli nyingi mwaka huu ila sasa nimerudi tena jukwaani.

Tunaanza; Tambua kuwa nafsi ndiyo sehemu ya mtu iliyobeba hatma yake yote awapo hapa duniani. Kazi ya roho ni kutia nguvu tu vilivyopo kwenye nafsi ili mtu aweze kuishi katika kiwango chake cha maisha.

Sasa, ili uweze kufanikiwa katika haya maisha na watu wote ambao tayari wameshafanikiwa, ni lazima uwe na uwezo mkubwa wa ku control (kuendesha) nafsi za wengine ili zikutumikie kwa vipawa vilivyopo ndani yake ndipo ufanikiwe.

Namaanisha kuwa unaweza kuishi hapa duniani na ukawa unatumikia watu wengine maisha yako yote kwa nafsi yako kukamatwa na kuendeshwa na watu hao.

Hapa tunazungumzia masuala ya kiroho. Katika ulimwengu wa kiroho upande wa nuru na upande wa giza,wote huvuta watu,kuwafunga na kuwaendesha kwa namna watakavyo wao ili wao waweze kufikia hatma zao.

Tuangalie mifano kidogo, wafanyabiashara; ili bidhaa zao ziuzike lazima wavute na ku control nafsi za watu, usije ukaona unapendelea kununua bidhaa zako sehemu fulani ukafikiri ni kawaida tu!,nafsi imekamatwa hapo. Watu wengine ni wanasiasa, kwenye mipira,kwenye uongozi, kwenye kuvuta wateja kwenye taasisi na mashirika mbalimbali hususani sekta binafsi na wahubiri wakubwa.

Wote hawa wakikosa nguvu za kuvuta na ku control nafsi za watu ili ziwatumikie,kamwe hawataweza kufanikiwa!. Sasa kazi itaanzia hapa kwa kujifunza vitu wanavyotumia kuvuta na ku control nafsi za watu katika pande zote za nuru na za giza. Vitu vinavyotumika ni;

1. Kiapo (maneno yenye ahadi kamili).

2. Sadaka (fedha au chochote kwa lengo maalumu).

3. Maneno/Maombi (yenye roho ndani yake).

4. Kiwakilishi chako chochote (mfano nguo au picha).

Nitakuwa nachambua kimoja kimoja kadri muda utakavyokuwa unapatikana na ninaimani watu wengi sana watajikomboa kutoka kutumikishwa na watu wengine na watajua mengi sana na siri nyingi sana na kuwa huru kuendesha maisha yao.

NB; Hakuna nafsi yoyote ya mwanadamu isiyokuwa na thamani,kama unataka kuamini we nenda kwa Mungu au kwa shetani ukiwa hali yoyote uone kama atakukataa!,na ukifuata masharti yao kikamilifu utakuwa milionea pasipo kujali ulikuwa katika hali gani ya nafsi yako.
This is too amazing

Leo nilikuwa kwenye tafakari ya uhusiano wa nafsi na Nyakati.

Baada ya kukosa majibu na taarifa za kutosha za kujifunza kuhusu makao ya nafsi ni wapi ... je nafsi Ina ishi in the spiritual realm? Or

Okay! Okay! So baada ya kukosa hivyo vyote usiku wa Leo nikavutwa kuja kwenye forum hii kusaka Uzi wa nafsi!

Sikujua kama upo! Ila nilikuwa na Imani tu ntapata! My spirit was pushing me!

Booom! Nakutana na huu uzi!
 
UTANGULIZI SEHEMU B;MAANA YA NAFSI. Leo tunaendelea na somo baada ya upepo kutulia na wote kuishia mitini. Nafsi ni mtu halisi na ana vitu vyote vya mtu wa nje. Mtu wa nje (mwili) ni kama kivuli cha mtu wa ndani (nafsi). Vitu vikuu vinavyofanya nafsi ifanye kazi vizuri ni, Akili ambayo inabeba milango yote ya fahamu, utambuzi, fikra, maarifa; Hisia ambayo inabeba furaha, upendo, huzuni na chuki. Nafsi inaweza kuingia katika mwili wowote hata wa mnyama bila shida. Ukiona mchawi anajigeuza paka au nyoka tambua ni nafsi yake ameivalisha kwenye mwili huo. Mtoto anaweza kurithi vitu vilivyopo kwenye nafsi ya mama yake na baba yake ila roho anarithi kwa baba tu. Kazi ya roho ni kuitia nguvu nafsi ili ifanye kazi yake halisi iliyoumbiwa. Roho haiwezi kufanya kazi na nafsi iliyovurugwa maana nafsi iliwekwa iende automatic katika kazi yake. Kipawa 'nyota' cha mtu kimewekwa ndani ya nafsi na siyo rahisi akijue mpaka afuate hatua muhimu. Huwezi kuiba kipawa cha mtu maana hata shetani mwenyewe hakijui, bali ni nafsi tu ya mtu inavurugwa na kuipotezea mwelekeo na kutumikishwa kwa faida ya mtu mwingine. Nafsi inaweza kufungwa kwenye mti, inaweza kuwekwa ndani ya chupa, inaweza kufungwa chini ya bahari inaweza kufungwa ofisini au kwenye nyumba za ibada na sehemu yoyote ile kulingana na matakwa ya mfungaji na kuitumikisha kadri apendavyo. Njia rahisi sana ya kujua nafsi yako imefungiwa wapi ni kwa kupitia ndoto. Angalia unaota sana upo maeneo gani na unafanya nini. Ili unase na kuendesha nafsi ya mtu/watu kadri upendavyo inategemea sana na nguvu (roho) inayoipa nafsi hiyo nguvu. Lazima uwe na roho yenye nguvu zaidi. Na kuna vitu ambavyo nimeviorodhesha hapo juu ambavyo hutumika kukamata na kuendesha nafsi na tutavijadili mbeleni. Sasa embu jiulize kidogo itakuaje endapo unataka kufungua biashara yoyote au kuingia katika uongozi au siasa au huduma za kiroho na hauwezi kuvuta nafsi za watu!, ukweli ni kuwa hauwezi kupata watu wowote maana kunawenzako wanatumia sala au dua au uchawi kuvuta watu (nafsi). Fikiria kwenye kuoa uwe msichana au mvulana na unapendwa na wengi, kila mtu atakuvuta kwa njia yake na mwisho mwenye nguvu atashinda. Watu wengi wanachanganyikiwa kwa nafsi zao kuvutwa na watu na mwisho wanabaki katikati na kushindwa kujua waelekee wapi. Ni kama kuchukua sumaku mbili na kuweka chuma katikati na kuivuta huku na huku, chuma itacheza tu hapo katikati hadi ipate sumaku yenye nguvu zaidi. Mwisho, Nafsi haitakiwi kurudi nyuma bali inatakiwa kwenda mbele tu, ikirudi nyuma mtu atakuwa nyuma ya muda na siku zote mtu anatakiwa awe mbele ya muda ili atayarishe mazingira ya mbeleni. Na hapa ndipo wazungu wanapotushinda tu kwa kuwa mbele ya muda. Ukikomboa nafsi yako, umekomboa maisha yako na utaishi kwa uhuru wote na kwa mafanikio ya uhakika.
Mkuu endelea kutoa maarifa.
 
Back
Top Bottom